Uchaguzi 2020 CHADEMA tafuteni namna ya kulinda kura zetu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,149
33,319
Mimi Ni mpenzi wa CHADEMA wa kufa Mtu, naichukia CCM kuliko kitu chochote. Ndio kitu kinachoongoza kati ya vitu ninavyovichukia.

Lakini ikatokea CHADEMA ikashindwa kihalali kabisa bila hila wala wizi wa kura wa aina yeyote, yaani Watanzania wakaichagua CCM kwa moyo mweupe kabisa bila mashakani yeyote kwa uwingi wao Watanzania na ikathibitishwa duniani na hata Mbinguni kuwa ushindi wa CCM Ni wa halali kabisa.

Mimi Lee Van Cliff ni nani hata nikatae maamuzi ya kihalali ya Watanzania wengi? Kwangu Mimi itakua sawa tu.

Sina Tena imani na Lissu na CHADEMA.

Nimekata tamaa kabisa kwa Lissu na CHADEMA yake, sina imani kabisa, narudia tena, SINA IMANI Tena na Lissu na CHADEMA Kama wataweza kulinda MAMILIONI ya kura zetu Watanzania, tutakazo mmiminia Tundu Lissu, tutakazo mpigia Tundu Lissu, namaanisha mamilioni ya kura za Ndio kwa Lissu wa CHADEMA.
  1. Nasema hivi kwa sababu huku mitaani kila unaeongea nae habari za Uchaguzi wengi wanasema hawana hata haja ya kampeni, wao tayari walishaikata CCM na Mgombea wao,nimeongea na rafiki, zangu, jirani zangu na watu wengine ambao Ni Wana CCM na watu mbalimbali wameniambia kuwa kura zao ni kwa Lissu tu.

Sasa kwa muktadha huo siamini Kama Lissu na CHADEMA wanaweza kulinda kura zetu, nimekata tamaa kabisa juu ya Ulinzi wa mamilioni ya kura za Watanzania.

Naishauri Chadema na Lissu waombe msaada wa UN ili wake kulinda kura za Lissu maana Ni nyingi mno,ndio mgombea wa Urais kwa Tanzania kwa Tanzania Atalanta mamilioni ya kura za Ndio na kumuacha kwa mbali mshindani wake.huku mtaani watu Wana vinyongo hatari.
Subirini tu.

CHADEMA tafuteni namna ya kulinda kura zetu jamani.
 
Mbona watu bado wako pande zote,kiuna wengi wapo upande wa CCM na kuna ambao wapo upane wa CDM,huwa tunapenda sana kujivutia ngoma upande mmoja wakati tukijua kuna pande mbili.

Kubwa zaiudi ambacho sisi tunatakiwa kufanya ni kuwaonyesha wengine kwanini wanatakiwa kubadilika,hizi story nyingine zitazidi kuwafanya wale wasiotaka mabadiliko waone hakuna jipya zaidi ya maneno,mwisho watakwambia weka muziki.
 
Mbona watu bado wako pande zote,kiuna wengi wapo upande wa CCM na kuna ambao wapo upane wa CDM,huwa tunapenda sana kujivutia ngoma upande mmoja wakati tukijua kuna pande mbili.
Kubwa zaiudi ambacho sisi tunatakiwa kufanya ni kuwaonyesha wengine kwanini wanatakiwa kubadilika,hizi story nyingine zitazidi kuwafanya wale wasiotaka mabadiliko waone hakuna jipya zaidi ya maneno,mwisho watakwambia weka muziki.
Hakuna atakaye wapigia kura CCM
 
Kweli kabisa.. Tunahitaji haki itendeke hapa.. Chadema jitahidini kuokoe kura zetu...
Tar 28 twendeni na Lissu..
Kumpigia kura Magufuri ni kutafuta laana kutoka kwa vizazi vyako hapo baadae ukiwa umesombwa na tani kadhaa za udongo
 
Point ya kulinda kura ni ya mpiga kura na sio mpigiwa kura.
Kwani kura zilindwe na mpiga kura
Kwa sababu wapigiwa kura ni wachache lakini wapiga kura ni wengi na wanapatikana kila uchochoro.

Hivi mimi wewe na yule tuna jukumu la kuwachagua wagombea wote wa Chadema na kuzilinda kura.

Kumbuka kwa Tanzania kulinda kura yako ni a matter of life and death
 
Back
Top Bottom