Uchaguzi 2020 CHADEMA: Taarifa tulizo nazo zinaonyesha Kampuni yenye makada wa CCM ndiyo itachapisha karatasi za kupigia kura...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ameeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikifanya manunuzi mbalimbali ya vifaa vya Uchaguzi bila kuhusisha vyama wala Umma.

Amesema Machi 09, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kwenye vyombo vya habari zabuni ya kuitisha Kampuni za kuchapisha karatasi za kupigia kura. Katika taratibu za kawaida za kimanunuzi Tume ilipaswa kuendelea kutoa taarifa kuhusu mchakato mzima wa uteuzi wa kampuni, kueleza ni Kampuni gani zilishindanishwa na kampuni gani ilishinda mchakato huo.

Amesema Juni 30 baadhi ya vyombo vya habari viligundua kuwa kampuni ya Ren-Form CC ya Afrika Kusini ndio imeteuliwa na Tume kuchapisha karatasi za kupigia kura. Amesema vilipomuuliza Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Kaijage athibitishe taarifa hizo, hakukanusha wala kuthibitisha taarifa hizo, bali alieleza kuwa siku chache zijazo Tume ingetoa taarifa kwa umma kueleza ni kampuni gani imeteuliwa na ni kwa zabuni ya kiasi gani. Hata hivyo amesema Tume bado haijatoa taarifa yoyote.

Vilevile, Mnyika ameeleza kuwa kwa mujibu wa vyanzo vyao vya taarifa vinaeleza kuwa kampuni iliyoteuliwa kuchapisha karatasi za kupigia kura ni Jamana Printers kutoka Tanzania.

Mnyika ameitaka Tume ya Taifa kujitokeza na kueleza ni kampuni gani iliyepewa kazi ya kuchapisha karatasi za kupigia kura kwenye #Uchaguzi2020. Vilevile ameitaka Tume ieleze mchakato mzima uliyofuatwa kuchagua kampuni iliyopewa dhamana ya kuchapisha karatasi hizo.

Amesisitiza kuwa iwapo Tume imebadili kampuni ya kuchapisha karatasi za kura, kutoka taarifa ya awali ya kampuni ya Ren-Form CC mpaka Jamana Printers ya Tanzania, ieleze ni mchakato gani wa manunuzi uliofuatwa kwenye uteuzi wa kampuni ya kuchapisha karatasi hizo.

Mnyika ameeleza kuwa endapo kampuni ya kuchapisha karatasi hizo itakuwa sio ya kuaminika itahatarisha uchaguzi wa haki kwani kutakuwa na uwezekano wa kuchapisha karatasi za ziada kwa lengo ka kufanya hujuma katika uchaguzi.

Vilevile ameongeza kuwa endapo Tume itathibitisha kuwa Jamana Printers ndiyo imeteuliwa basi itoe ufafanuzi kwa Umma kwakuwa taarifa walizo nazo zinaonesha kuwa kampuni hiyo ina makada wa CCM. Pia, ameitaka Tume iwahakikishie watanzania usalama wa karatasi za kupigia kura kwenye Uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo, Mnyika amesema Tume ya Uchaguzi haijatoa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya Siasa ila imetoa orodha ya wapiga kura tu. Ameongeza kuwa daftari la kudumu la wapiga kura linakuwa na orodha ya wapiga kura ikiambatana na picha zao.

Katika kikao cha kwanza cha kitaifa cha manunuzi na logistics cha Oktoba 8, Tume ya Taifa haijaweka wazi masuala yanayo husiana na mfumo wa ujumlishaji wa matokeo. Mfumo unaoandaliwa kutumika kujumlishia matokeo kutoka kwenye majimbo hadi ngazi ya Taifa.

Aidha, Mnyika ametoa rai kwa Tume kutoa fursa kwa vyama vya siasa ya kuuona na kuhakiki mfumo huo utakaotumika kujumlishia matokeo kabla haujaanza kufundishwa kwa wasimamizi wa kura na kuanza kutumika rasmi.
 
Wapwa

Wakati mgombea uraisi wa CHADEMA akianza tena kampeni zake baada ya kutumikia kifungo cha siku 8 kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi NEC, leo tena CHADEMA kupitia katibu mkuu wake ameiomba NEC iweke wazi kampuni iliyoshinda zabuni kushapisha ballot papers na mchakato mzima wa kuipata ulivyofanyika

Tusubiria NEC watasemaje



Source : Watetezi TV

Haki huinua Taifa
 
Back
Top Bottom