CHADEMA: Taarifa kwa umma kuhusu serikali kupandisha bei ya umeme

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Taarifa kwa umma kuhusu serikali kupandisha bei ya umeme

Gazeti la Tanzania Daima Toleo na. 3280 la tarehe 26 Novemba 23 limenukuu kauli iliyotolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene wakati akizungumza na kipindi cha Kumepampazuka kilichorushwa na Redio One juu ya Serikali kupandisha bei ya umeme kama Shirika la Umeme (TANESCO) lilivyoomba.

Katika habari hiyo Simbachawene amenukuliwa akisema kwamba endapo kuna mwananchi yeyote atakayeona gharama za umeme ni kubwa ni vema akaamua kuwasha kibatari au akae giza.

Rais Jakaya Kikwete anapaswa kumwagiza Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospter Muhongo kuwaomba radhi wananchi kwa kauli hiyo iliyotolewa na Naibu Waziri Simbachawene kwa niaba ya wizara anayoiongoza.

Aidha, ni vyema Rais Kikwete kwenye hotuba yake kwa taifa ya mwisho wa mwezi huu akawaeleza wananchi iwapo uamuzi huo wa kupandisha kwa mara nyingine bei ya umeme ndio utekelezaji wa ahadi ya maisha bora aliyoitoa kwa watanzania kuanzia kwenye uchaguzi wa mwaka 2005.

Hii ni kwa sababu kupandisha bei ya umeme kuna athari ya kuchangia katika ongezeko la gharama na ugumu wa maisha kwa kuwa shughuli za uzalishaji na maisha ya kila siku zinategemea kwa kiwango kikubwa nishati.

Kauli hiyo ya Simbachawene inadhihirisha mtazamo finyu wa kisera kwa Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba mahitaji ya nishati ya umeme ni kwa ajili ya kuondoa giza ambapo mbadala wa haraka ni kibatari.

Serikali inayoongozwa na CCM inapaswa kutambua kwamba mbadala wa nishati kwenye uzalishaji, huduma za kijamii na maisha ya kila siku ya wananchi katika karne ya sasa ya sayansi na teknolojia hauwezi kuwa kibatari.

Kwa upande mwingine, umma ni muhimu ukafahamu kwamba uamuzi huu wa Serikali kupandisha bei ya umeme wakati huu ni matokeo ya kutekeleza masharti ya Benki ya Dunia ambayo Serikali ilipewa Washington DC Oktoba 2013 bila kuzingatia hali halisi ya uchumi wa nchi na ustawi wa wananchi.

Aidha, uamuzi huu ni wa kuwabebesha wananchi mzigo wa gharama za muda mrefu za ufisadi katika sekta ya nishati nchini na ubovu wa mikataba inayoendelea kutumika mpaka hivi sasa katika sekta hii nyeti.

Hata hivyo Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo alisema uongo bungeni kwa nyakati mbalimbali mwaka 2012 na 2013 nilipohoji kuhusu masuala muhimu ya nishati ambayo iwapo hatua muafaka zingechukuliwa kwa wakati zingeepusha nchi kulazimika kuongeza kwa mara nyingine gharama za umeme.

Naomba Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa arejee hotuba nilizowasilisha kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tarehe 27 Julai 2012 na 22 Mei 2013 na kutoa majibu ya kweli kwa wananchi katika masuala yote tuliyohoji kuhusu nishati.

Nakala ya Hotuba hizo zinapatikana katika tovuti ya bunge na kwenye mtandao wahttp://mnyika.blogspot.com

( Hotuba ya Julai 2012- JOHN MNYIKA: HOTUBA YA KAMBI RASMI YA UPINZANI; WIZARA YA NISHATI NA MADINI na Hotuba ya Mei 2013- JOHN MNYIKA: HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI JOHN JOHN MNYIKA (MB) KUHUSU MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA )

Udhaifu uliotajwa kwenye hotuba hizo na katika kauli za Waziri Muhongo na Naibu Waziri Simbachawene kwa nyakati mbalimbali unaweza kusababisha Matokeo Mabaya Sasa- Bad Results Now (BRN) badala ya Matokeo Makubwa (Big Results) kwenye sekta ya nishati.

Hivyo iwapo Rais kupitia hotuba yake kwa taifa mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba 2013 hataeleza hatua alizochukua kuondoa udhaifu huo; nitaeleza hatua za ziada ambazo tutachukua katika kuisimamia Serikali kunusuru uchumi wa nchi na ustawi wa wananchi kutokana na ongezeko la bei ya umeme na mapungufu mengine kwenye sekta ya nishati.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

Serikali inadharau wananchi wake sana!! Aina noma tutaonana kwenye sanduku la kura,mbizi tutapiga,majani tutakula na vibatari tutawasha!!
 
hapo kwenye "hatua za ziada" ndipo napopataka maana siamini kama serikali hii inayoongozwa na JK itaweza kufanya lolote...
 
Simbachawene amejisahau sana.. Ndo yaleyale ya masikini akipata mat.ako hulia mbwata .....!
 
Macho na maskio ya watanzania bado yapo huku

Sakata la zitto na dkt. Kitila mjumbe wa baraza kuu chadema ailipua kamati kuu:

natanguliza maombi ya usikivu mwema tunapoelekea kuimaliza siku ya leo.

katika pita pita zangu nimekutana na mjumbe mmoja wa baraza kuu la chadema akichapa tamko kali pale LAMADA HOTEL.

hebu tulipitie kwa makini sote kwa pamoja.

ama kweli sasa CHADEMA NI PIGA NIKUPIGE.

TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe .
UTANGULIZI.
Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.

MIGOGORO NDANI YA CHAMA
Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie waliotofautiana msimamo.

Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea akaachwa kidogo apumzike.

Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum, tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila aina ya majina.

Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea chaguzi za ndani ya chama.
Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.

Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.

KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU
Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke, na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (BAVICHA)

Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.

Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na Ubaguzi uliopitiliza.

Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni mwa wanachama.
Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.

Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.

Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.

Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.

Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.

MSIMAMO WANGU.

Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.

Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
(i). watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama.

(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya chaguzi za ndani ya chama .

(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama.

Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa kidini na kikabila ama kikanda.

Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.

Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.

Nawashukuru sana.

Imetolewa na ;-

Joseph Y. Patrick

+255713802226

Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa
 
jamani tanzania nishati mzigo tunaobebeshwa wa gharama na matusi kejeli kisa tumewapa kura tutafakari mara mbili mbili

La sivyo bado kazi mbichi
 
Simbachawene amejisahau sana.. Ndo yaleyale ya masikini akipata mat.ako hulia mbwata .....!
Huyo Agwe,haishangazi tunapomsikia akiwaambia waTZ ambao hawatamudu gharama mpya za umeme,ni bora tu wakawasha vibatari!

Nasema haishangazi kusikia kauli hiyo inatoka kwa mbunge wa Kinsley,Goerge Sunbathers,kwa kuwa jimbo lake ni miongoni mwa majimbo,yaliyo nyuma sana kimaendeleo,kiasi ambacho,wakazi wa huko zaidi ya asilinia 95,hawana access ya umeme!

Kwa hiyo aliposema watakaishindwa kulipia viwango vipya vya umeme,wakawashe vibatari,aliokuwa amewalenga ni wapiga kura wake,ambao majority yao,tokea wazaliwe hawajawahi kuona umeme ukiwaka ndani ya nyumba!

Kwa hiyo kwao wao,akina Solowenyo wa Kibakwe,it makes no difference,kuwa na umeme,au kutokuwa nao!!
 
Macho na maskio ya watanzania bado yapo huku

Sakata la zitto na dkt. Kitila mjumbe wa baraza kuu chadema ailipua kamati kuu:

natanguliza maombi ya usikivu mwema tunapoelekea kuimaliza siku ya leo.

katika pita pita zangu nimekutana na mjumbe mmoja wa baraza kuu la chadema akichapa tamko kali pale LAMADA HOTEL.

hebu tulipitie kwa makini sote kwa pamoja.

ama kweli sasa CHADEMA NI PIGA NIKUPIGE.

TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe .
UTANGULIZI.
Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.

MIGOGORO NDANI YA CHAMA
Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie waliotofautiana msimamo.

Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea akaachwa kidogo apumzike.

Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum, tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila aina ya majina.

Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea chaguzi za ndani ya chama.
Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.

Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.

KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU
Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke, na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (BAVICHA)

Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.

Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na Ubaguzi uliopitiliza.

Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni mwa wanachama.
Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.

Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.

Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.

Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.

Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.

MSIMAMO WANGU.

Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.

Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
(i). watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama.

(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya chaguzi za ndani ya chama .

(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama.

Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa kidini na kikabila ama kikanda.

Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.

Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia tunayoitangaza kila kukicha.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni yangu kwa Watanzania.

Nawashukuru sana.

Imetolewa na ;-

Joseph Y. Patrick

+255713802226

Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa

Kumbe wewe Joseph ndio unasababisha Chama chetu kikose nguvu huko temeke sababu ya upuuzi wakoe?
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe hayakuhusu na pia uko nje ya mada.Kuwa Mtanzania Mzalendo pigania haki za Wanyonge,kuongezeka kwa bei ya umeme maana yake watu waendelee kuharibu misitu na maendeleo vijini ndiyo yatakuwa yamekwama.Waache Wazalendo watafakari juu ya hili na hatima ya nchi bila umeme.
 
Nadhani huyu naye mamluki,na ndio maana cdm haina nguvu tmk.anatakiwa afukuzwe arudi magambani.NA KUHUSU SIMBACHAWENE NA KAULI YAKE MI NADHANI AMELEWA MADARAKA..2015 SIO MBALI HUO ULEVI WAKE UTAMTOKA.
 
Suala la umeme ukweli litasababusha maisha kupanda ghafla bin vuu bila sababu yoyote ya msingi.
 
Haya ndo mambo ya kuitisha maandamano nchi nzma maana ukipanda tu ni hatari apa yenyewe tunatoana jasho kiko wap chadema iliyokuwa inapinga kwa hali na mali haya mambo cku hiz naona mmetusahau sana
 
Mpango uliopo ni kuwatukana wananchi hadi watakapotambua kuwa CCM kweli imewachoka!
 
tatizo la sisi wabongo tumezaliwa katika ujamaa na bado tuna hizi mentality za kijamaa. huku Sweden nauli ya basi ni 20 kr ambayo ni Tshs kama 5000 kwa ka trip. sie wengine tumenunua baiskeli ili kupunguza gharama, kufanya mazoezi na kadhalika. wanacharge hela nyingi na inakubalika kwani namna wanavyo organize usafiri wao ni wapo very efficient. hasa namna mabasi na treni zinavyofuata ratiba na pia ku cover maeneo mbalimbali. Daladala za bongo tunalipa zaidi Tshs 400 na tunataka kuwe na usafiri mzuri wa daladala. hata hilo Treni la Mwakyembe kama zina hakika kama wanapata faida ila ni lazima kuwa na usafiri wa uhakika ambao ni ghari. Tatizo la TANESCO ni la kuwa na mipango mibovu na ufisadi ila all in all umeme wa uhakika kunahitajika investiment kubwa sana. na si umeme tu hata maji, barabara nk. namna ya ku invest kwa nchi masikini kama bongo ni tatizo!!! kwani wengi wanaiba umeme na pia ni wachache wanaolipa. Ndiyo maana inatakiwa wachache wanaolipa waumie!!!! ni vizuri Tanesco iuzwe tu au igawanywe ili ishikwe na watu watakao dai bill kwa kila mtu, kuzuia wizi, na kuweka viwango stahiki vya umeme vitakavyo leta umeme wa uhakika
 
Back
Top Bottom