CHADEMA: Taarifa kuhusu vikao vya tathimini na Uchambuzi baada ya Uchaguzi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU VIKAO VYA TATHMINI NA UCHAMBUZI

Katika utaratibu wake wa kujipanga na kuendelea kutekeleza mikakati ya malengo ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya kufikia lengo kuu la kushinda uchaguzi, kushika dola na kuongoza serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa na utamaduni wa kuwa na vikao vya kujitathmini na kufanya uchambuzi kila baada ya uchaguzi mkuu na kuweka mpango kazi unaopaswa kutekelezwa na chama kwa miaka mitano inayofuata.

Vikao vya namna hiyo pia vimekuwa vikifanyika kila mwanzoni mwa mwaka mpya, lengo kubwa likiwa ni kufanya tathmini na uchambuzi wa utekelezaji wa mpango kazi huo na kuweka mikakati ya utekelezaji wa vipaumbele kwa mwaka mpya husika kulingana na mpango huo.

Mapendekezo ya vikao hivyo vya kiuchambuzi na tathmini (retreats) huwasilishwa kwenye vikao vya kikatiba vya chama kwa ajili ya kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi kwa ajili ya utekelezaji wake kadri inavyoelekezwa na vikao husika katika ngazi mbalimbali za chama.

Ni vikao vya namna hii ambavyo huwakutanisha viongozi wa kisiasa, watendaji na wataalam wa masuala mbalimbali, vimekuwa moja ya nguzo muhimu za CHADEMA katika kujipanga na kuweka mikakati ya kukisuka na kukiimarisha chama kwa ajili ya kutekeleza lengo kuu la kushika dola kwa kuiondoa CCM madarakani na hatimaye kuwaongoza Watanzania kufikia matamanio ya MABADILIKO YA KWELI nchini, badala ya ‘cosmetic changes’ kama inavyofanyika sasa chini ya CCM.

Katika utaratibu huo huo ambao umeshakuwa ni utamaduni wa CHADEMA kwa miaka mingi sasa, vikao hivyo vinaendelea kufanya tathmini na uchambuzi wa mpango kazi wa mwaka 2010-2015 na kupanga kwa ajili ya 2016-2020 na kupendekeza kwa ajili ya 2016 kabla ya kuwasilisha kwenye vikao vya maamuzi kwa mwaka huu, ambavyo vitakaa kulingana na utaratibu wa kikatiba.

Ufafanuzi unaotolewa kupitia taarifa hii, utasaidia kusahihisha habari ambazo hazina ukweli zinazolenga kupotosha umma, zinazoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwa makusudi au kwa kutokujua taratibu za CHADEMA katika kupanga na kuendesha mambo yake.

Imetolewa leo Alhamis, Januari 7, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Ni vikao vya namna hii ambavyo huwakutanisha viongozi wa kisiasa, watendaji na wataalam wa masuala mbalimbali, vimekuwa moja ya nguzo muhimu za CHADEMA katika kujipanga na kuweka mikakati ya kukisuka na kukiimarisha chama kwa ajili ya kutekeleza lengo kuu la kushika dola kwa kuiondoa CCM madarakani na hatimaye kuwaongoza Watanzania kufikia matamanio ya MABADILIKO YA KWELI nchini, badala ya ‘cosmetic changes’ kama inavyofanyika sasa chini ya CCM.

Eti vikao vya mabadiliko ya Kweli!!! Mbona mnavifanyia MOSHI KILIMANJARO kwa mwenyekiti Mbowe.Hamuwezi fanyia vikao hivyo mikoa mingine zaidi ya Kilimanjaro? Mnataka pesa za wajumbe za kulala mahoteli nk zitajirishe huko huko kwa mwenyekiti tu? Kwa nini hamkufanyia hivyo vikao Mtwara au tabora?

Hadi vikao mnaendekeza ukanda wenu !! LOOOO.Hayo mabadiliko yenu ndio cosmetic
 
Eti vikao vya mabadfiliko ya Kweli!!! Mbona mnavifanyia MOSHI KILIMANJARO kwa mwenyekiti Mbowe.Hamuwezi fanyia vikao hivyo mikoa mingine zaidi ya Kilimanjaro? Mnataka pesa za wajumbe za kulala mahoteli nk zitajirishe huko huko kwa mwenyekiti tu? Kwa nini hamkufanyia hivyo vikao Mtwara au tabora?

Hadi vikao mnaendekeza ukanda wenu !! LOOOO.Hayo mabadiliko yenu ndio cosmetic

Hayakuhusu.
 
Tunataka Mbowe aondoke madarakani kwa kuondoa misingi mikuu ya chama na kukumbatia watu wanaobanwa na misingi hiyo
 
Hayakuhusu.
Yananihusu.Mimi ni mlipa kodi ambayo CHADEMA inatumia kama ruzuku.Hapo hela yangu ya Ruzuku itakuwa imeshaliwa.Bili za hoteli nk zitakuwa zimekuwa-Inflated yaani acha tu.Wajumbe watakuwa walitumia tiketi za ndege na hela za kujikimu kwa gharama za CHADEMA kuwa wanaenda Kilimanjaro kwenye kikao cha CHAMA wakati ukweli ni kuwa walienda mapumziko ya krismas na mwaka mpya wakaona waweke kikao kuhalalisha ulaji,halafu warudi klwa tiketi hizo hizo wakisingizia wanatoka kikaoni wakati walienda mapumziko.Ruzuku yangu sitaki itumike Kilimanjaro tu.Vikao viwe vinafanyika mikoa mingine pia.
 
Yehoyada mbona hufananii jina hilo!
Maswali yako ni ya kipuuzi,
Moshi kuna tatizo gani
Kufanyia kikao?
Mbona wakifanyia dar
Hujawahi kuhoji?
Ingekuwa ni vema
Kushauri wafanye mikutano kwa mzunguko
Mikoani
 
Eti vikao vya mabadiliko ya Kweli!!! Mbona mnavifanyia MOSHI KILIMANJARO kwa mwenyekiti Mbowe.Hamuwezi fanyia vikao hivyo mikoa mingine zaidi ya Kilimanjaro? Mnataka pesa za wajumbe za kulala mahoteli nk zitajirishe huko huko kwa mwenyekiti tu? Kwa nini hamkufanyia hivyo vikao Mtwara au tabora?

Hadi vikao mnaendekeza ukanda wenu !! LOOOO.Hayo mabadiliko yenu ndio cosmetic
Moshi. Kwani ni ulaya au??
Moshi si kwa mbowe
Hai ndo kwa mbowe
Mkuu kwani we ulitaka kikao kifanyike wapi??
 
Yananihusu.Mimi ni mlipa kodi ambayo CHADEMA inatumia kama ruzuku.Hapo hela yangu ya Ruzuku itakuwa imeshaliwa.Bili za hoteli nk zitakuwa zimekuwa-Inflated yaani acha tu.Wajumbe watakuwa walitumia tiketi za ndege na hela za kujikimu kwa gharama za CHADEMA kuwa wanaenda Kilimanjaro kwenye kikao cha CHAMA wakati ukweli ni kuwa walienda mapumziko ya krismas na mwaka mpya wakaona waweke kikao kuhalalisha ulaji,halafu warudi klwa tiketi hizo hizo wakisingizia wanatoka kikaoni wakati walienda mapumziko.Ruzuku yangu sitaki itumike Kilimanjaro tu.Vikao viwe vinafanyika mikoa mingine pia.
Upo sahihi mkuu. Upo informed sana.
 
Moshi. Kwani ni ulaya au??
Moshi si kwa mbowe
Hai ndo kwa mbowe
Mkuu kwani we ulitaka kikao kifanyike wapi??
Hotel za Mbowe zipo Moshi na Arusha kwa ukanda huo wa kaskazini. Kabla hujajibu comment...Soma maelezo ya mtu uyaelewe kwanza.
 
Mmmmh tatizo si kikao kimefanyika wapi ila cjaelewa dhana ya kikao kufikia kutoa taarifa kwa vyombo vya habari!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU VIKAO VYA TATHMINI NA UCHAMBUZI

Katika utaratibu wake wa kujipanga na kuendelea kutekeleza mikakati ya malengo ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya kufikia lengo kuu la kushinda uchaguzi, kushika dola na kuongoza serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa na utamaduni wa kuwa na vikao vya kujitathmini na kufanya uchambuzi kila baada ya uchaguzi mkuu na kuweka mpango kazi unaopaswa kutekelezwa na chama kwa miaka mitano inayofuata.

Vikao vya namna hiyo pia vimekuwa vikifanyika kila mwanzoni mwa mwaka mpya, lengo kubwa likiwa ni kufanya tathmini na uchambuzi wa utekelezaji wa mpango kazi huo na kuweka mikakati ya utekelezaji wa vipaumbele kwa mwaka mpya husika kulingana na mpango huo.

Mapendekezo ya vikao hivyo vya kiuchambuzi na tathmini (retreats) huwasilishwa kwenye vikao vya kikatiba vya chama kwa ajili ya kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi kwa ajili ya utekelezaji wake kadri inavyoelekezwa na vikao husika katika ngazi mbalimbali za chama.

Ni vikao vya namna hii ambavyo huwakutanisha viongozi wa kisiasa, watendaji na wataalam wa masuala mbalimbali, vimekuwa moja ya nguzo muhimu za CHADEMA katika kujipanga na kuweka mikakati ya kukisuka na kukiimarisha chama kwa ajili ya kutekeleza lengo kuu la kushika dola kwa kuiondoa CCM madarakani na hatimaye kuwaongoza Watanzania kufikia matamanio ya MABADILIKO YA KWELI nchini, badala ya ‘cosmetic changes’ kama inavyofanyika sasa chini ya CCM.

Katika utaratibu huo huo ambao umeshakuwa ni utamaduni wa CHADEMA kwa miaka mingi sasa, vikao hivyo vinaendelea kufanya tathmini na uchambuzi wa mpango kazi wa mwaka 2010-2015 na kupanga kwa ajili ya 2016-2020 na kupendekeza kwa ajili ya 2016 kabla ya kuwasilisha kwenye vikao vya maamuzi kwa mwaka huu, ambavyo vitakaa kulingana na utaratibu wa kikatiba.

Ufafanuzi unaotolewa kupitia taarifa hii, utasaidia kusahihisha habari ambazo hazina ukweli zinazolenga kupotosha umma, zinazoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwa makusudi au kwa kutokujua taratibu za CHADEMA katika kupanga na kuendesha mambo yake.

Imetolewa leo Alhamis, Januari 7, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA
 
Asante sana kwa taarifa mkuu Molemo Chadema ni chama makini kinachopanga mikakati makini wamekuwa wepesi sana kujibu tuhuma ambazo zinatolewa ambazo hazina ukweli hii inasaidia kuwaumbua wale wanatengeneza tuhuma za uwongo dhidi ya chama
 
Sasa mbona husemi kama hivyo vikao vimeshafanyika ama bado, na kama bado mbona hutaji tarehe ama kalenda ya hivyo vikao. ?
 
Back
Top Bottom