CHADEMA: Suluhu ni Mkapa kurudi Arumeru Mashariki kuomba radhi

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
SIKU moja baada ya kuwepo taarifa kuwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, anahaha kutafuta suluhu baina yake na mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere, kwa familia ya Mwalimu Julius Nyerere, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kiongozi huyo anapaswa kurudi Arumeru Mashariki na kuomba radhi mbele ya wananchi kwa uongo aliousema.

Kutokana na tuhuma hizo, CHADEMA kimewataka wakazi wa Arumeru na Watanzania kwa ujumla kuwa makini na CCM, kwani kimekuwa kikitumia mbinu zisizo halali kuendelea kutawala ikiwemo kuwarubuni, kulaghai na kusema uongo.

Akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wananchi wa Arumeru jana, meneja kampeni wa CHADEMA, Mchungaji Israel Natse, alisema kuwa kama kweli Mkapa anataka kujisafisha kwa uongo aliosema mbele ya wananchi, dawa pekee inayoweza kumsaidia ni kurudi na kuwaomba radhi.

“Unajua tunapowaambia wananchi kuwa wawe makini na CCM na viongozi wake mifano sahihi ndiyo hii…kama mwenyekiti mstaafu anaweza kusema uongo kama huo mbele za watu sasa itakuwaje kwa watendaji wa chini yake, itakuwaje kwa wanachama wa kawaida, chama hiki kimefika mwisho, hakiwezi tena kusimama mbele ya wananchi na hapa Arumeru itakuwa ni moja ya fundisho kuwa zama zao,” alisema.

Naye Vicent Nyerere amemtaka Mkapa akamwonyeshe ukoo alikozaliwa baada ya kuutangazia umma kuwa hatoki katika familia ya Mwalimu Nyerere.

“Unajua mimi nashangaa kwa mtu mzima kusema uongo mbele ya wananchi, tena kiongozi anayepaswa kuaminiwa na watu anaowaongoza. Alipofariki baba yangu ambaye alikuwa rafiki yake na Mkapa pia, alikuja nyumbani kwetu kwenye msiba…hata rambirambi alinikabidhi mimi.

“Sasa kwa kuwa kasema mimi si familia ya Nyerere, anipeleke huko kwenye hiyo familia nyingine,” alisema Nyerere.
 
kama sikosei huyo anajiita mr clean keshakimbia jimbo la arumeru, maana kwa nimjuavyo yule fisadi, hawezi kurudi na kuwaomba msamaha wana arumeru ati, lets kip an eye anyway
 
"Unajua mimi nashangaa kwa mtu mzima kusema uongo mbele ya wananchi, tena kiongozi anayepaswa kuaminiwa na watu anaowaongoza. Alipofariki baba yangu ambaye alikuwa rafiki yake na Mkapa pia, alikuja nyumbani kwetu kwenye msiba…hata rambirambi alinikabidhi mimi.

"Sasa kwa kuwa kasema mimi si familia ya Nyerere, anipeleke huko kwenye hiyo familia nyingine," alisema Nyerere.
Duh, hapo kwenye red naona Vicent anazidi kukaba koo la BWM. Na bado wakijichanganya ndiyo mwanzo wa mengi!!
 
Hii movie ipö hatua ya mwisho kwa sababu mkapa ameficha kichwa chake kwenye gamba la kobe hawezi kuomba msamaha.Atakuja mwishoni kufunga kampeni
 
"Unajua mimi nashangaa kwa mtu mzima kusema uongo mbele ya wananchi, tena kiongozi anayepaswa kuaminiwa na watu anaowaongoza. Alipofariki baba yangu ambaye alikuwa rafiki yake na Mkapa pia, alikuja nyumbani kwetu kwenye msiba…hata rambirambi alinikabidhi mimi.

"Sasa kwa kuwa kasema mimi si familia ya Nyerere, anipeleke huko kwenye hiyo familia nyingine," alisema Nyerere.

Hii nimeipenda.
 
Hawa jamaa wa CCM nawachukia sana hata wale wanaowashabikia siwapendi kabisaa
 
Haki ya mungu nazani mi nina matatizo!!! Ni hili la Vicent kuwa c mwanafamilia ya Nyerere....!! What's so special hapa hata humu JF kuwe na threads na posts nyiiiiiiiingi kuhusu issue kama hii?! Hivi ya issue ya msinbgi hapa ni kwanini Mkapa kasema Vicent si MWANAFAMILIA ya Nyerere au Mkapa amedanganya?! Kama issue ni kv amesema Vicent si mwanafamilia ya Nyerere; so what's so special hapo?! Awe mwanafamilia au siwe mwanafamilia, ni nini hapo cha kufanya media zote zione ndo jambo la kujadili kwa mapana na marefu?! Kama issue ni uongo wa Mkapa, hivi ni tangu lini Mkapa amepata kuwa mtu decent kiasi hicho hata ionekane ni big issue kwa yeye kudanganya? Kama leo hii mtu ataamua kuorodhesha mabovu ya Mkapa, hili la kusema Vicent si mwanafamilia ya Nyerere haliwezi kuwa hata katika kumi bora!
 
Anapaswa kuwataka radhi wana arumeru,familia ya Nyerere na watanzania kama kweli ana uhakika alipotosha
 
Haki ya mungu nazani mi nina matatizo!!! Ni hili la Vicent kuwa c mwanafamilia ya Nyerere....!! What's so special hapa hata humu JF kuwe na threads na posts nyiiiiiiiingi kuhusu issue kama hii?! Hivi ya issue ya msinbgi hapa ni kwanini Mkapa kasema Vicent si MWANAFAMILIA ya Nyerere au Mkapa amedanganya?! Kama issue ni kv amesema Vicent si mwanafamilia ya Nyerere; so what's so special hapo?! Awe mwanafamilia au siwe mwanafamilia, ni nini hapo cha kufanya media zote zione ndo jambo la kujadili kwa mapana na marefu?! Kama issue ni uongo wa Mkapa, hivi ni tangu lini Mkapa amepata kuwa mtu decent kiasi hicho hata ionekane ni big issue kwa yeye kudanganya? Kama leo hii mtu ataamua kuorodhesha mabovu ya Mkapa, hili la kusema Vicent si mwanafamilia ya Nyerere haliwezi kuwa hata katika kumi bora!
Wewe unaona si issue kwa Mkapa kudanganya wenzako wanaona ni issue ndio maana binadamu tuko tofauti.
 
Akome kuropoka ropoka siku nyingine.mizimu ya baba wa taifa inamuandama sasa

Ni kweli. lakini na wewe kama una tabia kama avatar yako inavyoonesha ni vizuri ukashika ushauri uliompa Mr Clean, Mkapa.
avatar50584_7.gif
 
Mzee Punch akukosea kumwita huyu jamaa wakati akiwa waziri wa elimu ya juu "Makopo"!!
 
Haki ya mungu nazani mi nina matatizo!!! Ni hili la Vicent kuwa c mwanafamilia ya Nyerere....!! What's so special hapa hata humu JF kuwe na threads na posts nyiiiiiiiingi kuhusu issue kama hii?! Hivi ya issue ya msinbgi hapa ni kwanini Mkapa kasema Vicent si MWANAFAMILIA ya Nyerere au Mkapa amedanganya?! Kama issue ni kv amesema Vicent si mwanafamilia ya Nyerere; so what's so special hapo?! Awe mwanafamilia au siwe mwanafamilia, ni nini hapo cha kufanya media zote zione ndo jambo la kujadili kwa mapana na marefu?! Kama issue ni uongo wa Mkapa, hivi ni tangu lini Mkapa amepata kuwa mtu decent kiasi hicho hata ionekane ni big issue kwa yeye kudanganya? Kama leo hii mtu ataamua kuorodhesha mabovu ya Mkapa, hili la kusema Vicent si mwanafamilia ya Nyerere haliwezi kuwa hata katika kumi bora!

Kajipange upya kupost wehu wako humu, alafu najua unajifunza kutumia macho kusikia badala ya masikio ! Kama hamna cha maana katika post za vcent Nyerere kuwa yy si mwanafamilia ya nyerere, sasa mbona naww umechangia?
 
Back
Top Bottom