CHADEMA someni maoni mitandao ya kijamii kwenye masuala yanayowahusu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,640
2,000
Nazijua fika takwimu za mitandao ya kijamii na Twitter ndo inaongoza, ila kama tukiangalia engagement ya mambo yanayowahusu basi Twitter ni ya mwisho na kama inatija yeyote basi ni kuwajaza Kiburi na huenda mkapopoteza ushawishi wenu kabisa ndani ya miaka mitatu ijayo.

Ukienda kutazama post zenye matamko ya viongozi wenu katika media outlets kila mtu anawapinga na wengi wanadhani labda hamna nia njema na Taifa ili. Na sasa inaonekana dhairi mkiwa na mtu mstarabu basi mnaanza dharau (Bila kujali ni nini unamini, Tanzania si kama USA utakubali tu mwenywkiti, na mwalimu mkuu ni watu tunaowaogopa na tunaamini wanapaswa kuheshimiwa challenging the status quo sio utamaduni wa wabongo acheni kua idealistic (Mh. Mbowe should know this better than anyone)). Watanzania si watu kama wa mataifa mengine hamna idadi kubwa ya watu wanaotaka power reshuffle, na hawafwati trends za kisiasa za watu wa mataifa mengine.

Kama mnataka kupima ratings zenu vizuri basi tazameni watu wanasemaje. Mpo kwenye decline moja kubwa sana especially kwa online community (namnajua impacts zake rights).

Mwisho: Whoever leads strategy should resign and I doubt kama hata mna idara hii. You need a team to execute this na sio maadhimio ya chama, CCM does this subconsciously but nyie mpo scattered all over the place, politics at some time ni less quantitative, sawa mnaweza kua na active members but do they believe in the movement, how many traitors have you had?

kwanini usiongelee CCM yako hawa jamaa hawana wabunge lakini mnashinda kuwaongelea😂 wewe unashida gani kama kweli una 100% ya Watanzania
 

Godo

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
336
500
Chama cha upinzani chenye maono na future nzuri ni ACT tu hao wengine ni magenge ya wafanya fujo tu.
 

Tall Guy fam

JF-Expert Member
Jan 16, 2017
860
1,000
Ukweli ni kwamba watu huwa wanapigia kura vyama vya upinzani kutokana na kuchoshwa tu na matendo ya Rais anaekuwa madarakani.

Na siyo kwamba vyama vya upinzani ni bora kuliko CCM.

CCM ingeweza kuanguka kirahisi kama mpaka leo kungekuwa na Rais yule yule hasa angekuwa kama Magu.

Hii mbinu ya kubadili marais kila baada ya miaja 10 ina tabia ya kujenga matumaini mapya kwa watu na hivyo CCM kuendelea kuwepo.

Na kibaya zaidi vyama vya upinzani vimekuwa ni mihemko, matukio, ubinafsi na agenda za ajabu ajabu.
Sababu pekee CCM inashinda uchaguzi ni kwasababu ya wizi wa kura/uchanguzi.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Sababu pekee CCM inashinda uchaguzi ni kwasababu ya wizi wa kura/uchanguzi.
CCM bado ina uwezo wa kushinda kura kwa haki kabisa nchi hii. Kama umetembea nchi hii utajua tu.

Mikoa yenye uungwaji mkubwa wa upinzani ni michache sana.

Wanawake na wazee bado ni wapiga kura waaminifu sana wa CCM.

Vijana ndio wapiga kura wa upinzani ila ni wagumu wa kupiga kura mpaka wahamasishwe sana.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,755
2,000
Chadema ni sawa na mtu alie katika hatua za mwisho za kufa. Ni lazima atape tape kujaribu kuokoa nafsi (roho) yake, lkn mwisho wa yote anakufa. Nashauri mwaka 2025 chadema wasisimamishe mgombea kwa upande wa uraisi, maana raisi Samia anatutosha na kutufaa watanzania kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.
Jamani Chadema si Magufuli alishaiua kabisa? Mbona hamueleweki?
 

Qwy

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
4,362
2,000
Io ya picha nisaidie wewe kiongozi, na mimi sio MATAGA. Nafwatilia digital trends and i just gave an honest opinion.
Hii honest opinion uliwapa CCM enzi hizi waliposema digital trends si lolote si chochote? Kwamba eti CHADEMA wanategemea digital trends ambazo haziakisi uhalisia on the ground.
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
4,517
2,000
Tatizo la chadema ni kuamini kila anayetoa mawazo tofauti nao yuko ccm. Kwa kufanya hivyo wameziba masikio kupokea ushauri.

Kwanza ieleweke kuwa denokrasia kwa nchi za kiafrika haina zaidi hata miaka 50. Kama ndivyo watu walio wengi hawaujui mfumo huu hata wakidanganywa na vyama tawala kuwa utaleta mauaji HUAMINI.
Sasa chama kama cdm kicheze karata kwa akili kubwa sio lazima mengine yatimie ktk kizazi chao, sio lazima washinde uchaguzi hivi karibuni lkn watakuwa wameweka mbegu ya baadae kwa kile wanakisimamia

Siasa za MATUSI si jadi ya Mwaafrika na ieleweke kuwa Rais anaposema kuwa "wee na kigazeti chako" ANAMAANISHA. Ipo heshima ya Kiafrika japo tutaipinga hatujawahi kuona Baba Muafrika akiwa na binti yake wanachupi tu sebuleni lkn wenzetu si jambo la ajabu.
Wenzetu si jambo la ajabu mzee (Baba) akizeeka kumpeleka nyumba za wazee atunzwe huko lkn Afrika haipo hivyo.
Ni lazima Demokrasia iendane na utamaduni wa mahali ilipo, demokrasia ikiigwa toka marekani na kuicopy ifanye kazi Tz ni upungufu wa fikra.
Lengo la Demokrasia kama ni Uhuru na Haki basi iyo ndio iwe target mengine tuchane nayo.

Tunapenda upinzani UNACHOCHEA UTENDAJI WA SERKALI iliyo madarakani
Tunachukizwa na kutumika vibaya kwa mihimili ya serkali kwa namna ZOOOTE lkn si Kwa visasi.
Viongizi wetu wote wa awamu walikuwa na mapungufu lkn yumejenga utamaduni wa kuwaheshimu.
Tunataka katiba ndio ,lkn hitaji kubwa ni UTII WA KATIBA na hili ndio tatizo wala si mapungufu yake.

Nimeamini tu kuwa as we go, hakutakuwa na Amani duniani
Its written
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,234
2,000
Jamani Chadema si Magufuli alishaiua kabisa? Mbona hamueleweki?
Firauni alikufa na kuacha masalia ya wafuasi wake kadhaa, ambao bado walikuwa wanaendeleza ufirauni mpk pale walipokuja kupotezwa kabisa na tawala zilizokuja baadae. Kwahiyo chadema ishakufa lkn yamebakia masalia ambayo tunaendelea kuyaangamiza kupitia utawala bora, sheria, hoja na baadae sanduku la kura mwaka 2025.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,755
2,000
Firauni alikufa na kuacha masalia ya wafuasi wake kadhaa, ambao bado walikuwa wanaendeleza ufirauni mpk pale walipokuja kupotezwa kabisa na tawala zilizokuja baadae. Kwahiyo chadema ishakufa lkn yamebakia masalia ambayo tunaendelea kuyaangamiza kupitia utawala bora, sheria, hoja na baadae sanduku la kura mwaka 2025.
Mara hii mmeanza kumwita Firauni? Hata kama mna chuki kwa sababu aliipendelea Chato kwa kujenga vitu visivyo na umuhimu lakini siyo vizuri kumlinganisha na Firauni. Magufuli alifanya makosa lakini nyie wapambe wake ndiye mlimpoteza njia.
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,234
2,000
Mara hii mmeanza kumwita Firauni? Hata kama mna chuki kwa sababu aliipendelea Chato kwa kujenga vitu visivyo na umuhimu lakini siyo vizuri kumlinganisha na Firauni. Magufuli alifanya makosa lakini nyie wapambe wake ndiye mlimpoteza njia.
Kosa ni la mwenyekiti wenu. Badala ya kusajili wasomi ndani ya chama yeye anasajili mateja, mashoga, wanywa viloba na gongo, na vibaka.
 

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,638
2,000
Chadema ..walitakiwa kufanya uchaguzi kwanza...

Bora Malisa ndo awe Mwenyekiti
Angalau anaweza Ku reason

Hapana mkuu.ni kweli Mbowe ameishiwa mbinu hatukatai lakini bado anastahiri kuongoza chama Maana chadema inahitaji mwenyekiti mwenye fedha otherwise muda huu tungekuwa tumeshaizika chadema.kwa maswaibu yaliyompata mbowe kuhalibiwa kila vyanzo vyake vya fedha.malisa hawezi kuhimili ile mikiki so tuseme tu mbowe bado chadema tunamhitaji sana japo kuongoza ashaishiwa mbinu.nadhani wasaidizi wanatakiwa wamsaidie sana kimbinu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom