Chadema-sio lila kiang'aacho ni dhahabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema-sio lila kiang'aacho ni dhahabu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Oct 5, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Kanzi kamedondosha habari eti baada ya kushindwa uchaguzi wa NEC-CCM hatimaye Sumayi anataka kuingia CDM. Kujiunga na chama cha siasa ni haki ya kikatiba ya kila raia wa TZ. Ila kujiunga na CDM kwa masharti ya kuwa kiongozi ni kuibaka katiba ya CDM. Nchi nyingi duniani zinaamini ili kugombea uraisi lazima uwe raia wa kuzaliwa, na nyingine zinakwenda mbali zaidi kwa kusema lazima uwe umeishi ndani ya nchi yako kwa miaka mitano kabla ya kugombea uraisi.

  Makapi ya CCM hasa yale yanayoingia CDM baada ya kutibuliwa na mafisadi wenzao huko walikotoka sioni kama ni busara kuwaahidi chochote waingiapo ndani ya CDM. Siasa za kizamani za kuhama vyma kwa ahadi za madaraka ni rushwa kubwa sana kuliko zote. Rushwa ya vyeo ndio inaangamiza Taifa letu. Wasio faa wanapewa madaraka kwa rushwa halafu wanaleta maafa mkaubwa sana kwa wananchi.

  Siamini kabisa kushindwa uchaguzi na kusaka madaraka sehemu nyingine. Kama mtu amekuwa na cheo cha waziri mkuu leo anashindwa just kanec sijui ka wilaya au mkoa kweli anaweza kushika dola?? Sio kila king'aacho nidhahabu.

  Karibuni wote Chadema ila hakuna ahadi ya cheo wala madaraka, chukua kadi vaa gwanda onyesha uwezo wa kuchapa kazi , uadilifu, wacha majungu, wacha kunung'unika wacha makundi, wacha uchu wa madaraka tumikia wananchi. CCM tunayoipigia makelele ni matokeo ya hawa viongozi walioipora nchi na kuifanya shamba la bibi.

  Tuwe waangalifu kuwapokea kina Sita kumbe ni uchu tu mwisho wa siku wanatudhalilisha.

  Sauti ya
  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Kilio changu ni kuona Ikulu inarusdisha hadhi ya kuwahudumia wananchi bila kujali hali na uduni wao.
   
Loading...