Katibu wa Chadema Mkoa wa Singida, Patrick Msuta amekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo Wilfred Kitundu na kusema: Kama alikuwa na tatizo, angekatia rufani suala hilo katika ngazi husika. hii inaonyesha ni jinsi gani upeo wake ulivyo mdogo na alivyochoka kiakili.
Uamuzi wake ni kama kutengeneza mgogoro na katika mgogoro una kujenga au kubomoa. Sasa uamuzi wake hauwezi kubomoa chama, kwani Chadema kuna watu wazuri wenye uwezo wa kukijenga chama. Chadema hakuna ilichopoteza kwa uamuzi wake.
Alichokifanya ni kama ametumia demokrasia yake kupinga uamuzi wa Kamati Kuu na ametekeleza... lakini juzi tu hapa, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa mtu ambaye hawezi siasa aache, akae kando akalime, mimi nadhani huyu anatekeleza kauli ya Rais, alisema Msuta.
Msuta, baadaye alisema kuwa uongozi wa Chadema mkoani humo hauhusiki na yaliyozungumzwa na Kitundu: Huo ni uamuzi wake yeye mwenyewe, hakuna anayehusika na uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi ya uenyekiti.
Chadema Mwanza watoa tamko
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilemela, Mwanza, Yunusi Chilongozi amesema chama chake kitawachukulia hatua wote waliohusika kutoa tamko la kuwapiga marufuku viongozi wa kitaifa, Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa na Mbowe kufika mkoani humo.
Chilongozi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Chadema, kimechoka kuchafuliwa na kundi la vijana ambao wamekuwa wakitumika kwa madhumuni na malengo yasiyofahamika na sasa kitawashtaki mahakamani.
Tuko katika maandalizi ya mapokezi ya viongozi wetu kichama mkoani Mwanza na tunalaani kauli ya Robert Gwanchele anayejiita Mwenyekiti wa Matawi ya Chadema Mkoa wa Mwanza ikiwazuia viongozi wa juu wa chama hicho kutokanyaga Mwanza.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 17 inatoa uhuru wa kila Mtanzania kutembea sehemu yoyote ya nchi ilimradi havunji sheria za nchi na waliotoa tamko la kuwazuia viongozi wao wamevunja sheria za nchi, alisema Chilongozi.
Source:Mwananchi Jumatano