CHADEMA Singida Yamshangaa Mwenyekiti aliyejiuzulu...

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu wa Chadema Mkoa wa Singida, Patrick Msuta amekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo Wilfred Kitundu na kusema: “Kama alikuwa na tatizo, angekatia rufani suala hilo katika ngazi husika.” hii inaonyesha ni jinsi gani upeo wake ulivyo mdogo na alivyochoka kiakili.


“Uamuzi wake ni kama kutengeneza mgogoro na katika mgogoro una kujenga au kubomoa. Sasa uamuzi wake hauwezi kubomoa chama, kwani Chadema kuna watu wazuri wenye uwezo wa kukijenga chama. Chadema hakuna ilichopoteza kwa uamuzi wake.


“Alichokifanya ni kama ametumia demokrasia yake kupinga uamuzi wa Kamati Kuu na ametekeleza... lakini juzi tu hapa, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa mtu ambaye hawezi siasa aache, akae kando akalime, mimi nadhani huyu anatekeleza kauli ya Rais,” alisema Msuta.


Msuta, baadaye alisema kuwa uongozi wa Chadema mkoani humo hauhusiki na yaliyozungumzwa na Kitundu: “Huo ni uamuzi wake yeye mwenyewe, hakuna anayehusika na uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi ya uenyekiti.”


Chadema Mwanza watoa tamko


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilemela, Mwanza, Yunusi Chilongozi amesema chama chake kitawachukulia hatua wote waliohusika kutoa tamko la kuwapiga marufuku viongozi wa kitaifa, Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa na Mbowe kufika mkoani humo.


Chilongozi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Chadema, kimechoka kuchafuliwa na kundi la vijana ambao wamekuwa wakitumika kwa madhumuni na malengo yasiyofahamika na sasa kitawashtaki mahakamani.


“Tuko katika maandalizi ya mapokezi ya viongozi wetu kichama mkoani Mwanza na tunalaani kauli ya Robert Gwanchele anayejiita Mwenyekiti wa Matawi ya Chadema Mkoa wa Mwanza ikiwazuia viongozi wa juu wa chama hicho kutokanyaga Mwanza.


“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 17 inatoa uhuru wa kila Mtanzania kutembea sehemu yoyote ya nchi ilimradi havunji sheria za nchi na waliotoa tamko la kuwazuia viongozi wao wamevunja sheria za nchi,” alisema Chilongozi.


Source:Mwananchi Jumatano
 
Katibu wa Chadema Mkoa wa Singida, Patrick Msuta amekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo Wilfred Kitundu na kusema: "Kama alikuwa na tatizo, angekatia rufani suala hilo katika ngazi husika." hii inaonyesha ni jinsi gani upeo wake ulivyo mdogo na alivyochoka kiakili.


"Uamuzi wake ni kama kutengeneza mgogoro na katika mgogoro una kujenga au kubomoa. Sasa uamuzi wake hauwezi kubomoa chama, kwani Chadema kuna watu wazuri wenye uwezo wa kukijenga chama. Chadema hakuna ilichopoteza kwa uamuzi wake.


"Alichokifanya ni kama ametumia demokrasia yake kupinga uamuzi wa Kamati Kuu na ametekeleza... lakini juzi tu hapa, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa mtu ambaye hawezi siasa aache, akae kando akalime, mimi nadhani huyu anatekeleza kauli ya Rais," alisema Msuta.
Which is which?
 
kuzuia kifo na mazishi ya chadema ni sawa kabisa kabisa na kuzuia mafuriko kwa viganja vya mikono
 
Tusimponde jamani asije akatufukuza kwennye nyumba yake ambayo tunatumia kama ofisi.
 
CDM tuendako si kwenyewe. Mungu ampe hekima Mbowe ili isiwe chanzo cha cha CDM kuwa historia. Tumeshapoteza focus, badala ya kusonga mbele tumeanza malumbano na kuonana wabaya. Tusiendelee kuchemsha zaidi wana chadema.
 
Lakini tuangalie na upande wa pili je ni halali mbowe kugombea peke yake ili apite bila kupingwa???
 
MSIMAMO WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA

(i)Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

(ii)Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.

(iii)Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.

(iv)
Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa kuwa asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.

(v)Tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa
Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa Chama, Kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.

MWISHO, Kutokutii maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki,Singida tunasema kuwa ''
kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA CHADEMA.''
 
cdm tuendako si kwenyewe. Mungu ampe hekima mbowe ili isiwe chanzo cha cha cdm kuwa historia. Tumeshapoteza focus, badala ya kusonga mbele tumeanza malumbano na kuonana wabaya. Tusiendelee kuchemsha zaidi wana chadema.

hata mimi kamanda wangu nimeshaanza kukata tamaa... Hivi kuna tatizo gani zitto kugombea uenyekiti..kama anajiamini angemuacha tu dogo wapambane kwenye masanduku ya kura
 
Lakini tuangalie na upande wa pili je ni halali mbowe kugombea peke yake ili apite bila kupingwa???

amewahi lini kugombea peke yake?

mbona mtindo huo umekomaaa ccm na hamsemi?

kweli nyani haoni kundule lake
 
naskia hajui kusoma kaandikiwa na mwigulu kwa Msaada wa mjinga mwampamba
 
Back
Top Bottom