habariyamujini
JF-Expert Member
- May 16, 2013
- 3,094
- 456
Ihanja; Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), kimepata pigo kubwa katika kampeni zake za kutetea kiti cha udiwani wa Kata ya Iseke, Singida Magharibi, baada ya Katibu wake wa Kata, Francis Antoni, kujiuzulu juzi na kurejea CCM, kitendo kilichokichanganya kabisa chama hicho.
Pamoja na kurejea CCM, Antoni alimkabidhi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Steven Wasira, zaidi ya kadi 350 za Chadema. Antoni alirejea CCM juzi wakati wa mkutano wa hadhara wa kuzindua rasmi kampeni za CCM katika kugombea nafasi ya udiwani wa Kata ya
Iseke, wilayani Ikungi. Aliahidi kumpigia debe mgombe wa CCM Amos Mughenyi, ili aweze kushinda kwa kishindo.
Alisema badala ya kuhimiza maendeleo CHADEMA kimejikita zaidi katika kupandikiza chuki, vurugu na maandamano yasiyokuwa na tija yo yote. Kwa upande wake, Wasira alisema kila Mtanzania sasa ametambua kuwa CHADEMA haina sera za kuwaendeleza watu na badala yake inataka kupandikiza fujo, vurugu, matusi na uchochezi.
source mkutano wa hadhara kata ya iseke na google group.