Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,115
- 39,137
Kwa sasa kila mtanzania anataka kujua nini kitafanywa na CHADEMA katika kupata wagombea wake katikaa nafasi za ubunge wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tayari bunge kupitia kwa spika wa bunge na baadaye Katibu wa bunge wameshatoa miongozo miwili, muongozo wa kwanza ni ule ulioipa CHADEMA nafasi mbili za kutoa wabunge wa Afrika mashariki kwa mara ya kwanza, na mwongozo wa pili ni kuhusu nafasi ya Mwanamke katika uteuzi.
Macho na masikio yetu sisi watanzania tunaopenda mabadiliko tunasubiri kuona jina la NUSRAT HANJE likipitishwa kwa sababu hizi....
1/Ni mtanzania mwenye jinsia ya kike.
2/Ni mwanamke jasiri na mpambanaji wa ukweli kabisa.
3/Ni mwanaCHADEMA mvumilivu sana kwa chama chake kwa kipindi chote cha maisha yake ya kisiasa.
4/Ana kidhi vigezo muhimu vya desturi za maisha ya kisiasa yanayogubika siasa za Tanzania kwa sasa (issue za Imani? Ukanda? Ukabila?)
5/Ni mwanamke, kijana, Machachari, Mwerevu, anayejua kujieleva vyema, Mdadisi na Anayejiheshimu sana katika maisha yake ya kila siku.
6/Uteuzi wake utakuwa unaifanya Tanzania kuonekana kama nchi yenye wanawake jasiri, Vijana imara, watu wanaojiheshimu, Kabila zote, Dini zote.
Nitastaajabu sana kama CHADEMA watashindwa kumteua huyu dada NUSRAT HANJE.
Binafsi ninamuunga mkono huyu Dada.