CHADEMA si chama cha wananchi, ni kikundi tu cha watu wanaotaka kushika madaraka

Ni maajabu muandika rhetorics kupitia phone keypads combinations anajaribu ku-assassinate group la wananchi walioandikishwa rasmi na kadi milioni 7 ambapo wapenzi ambao hawajaandikishwa hua ni mara mbili ya waliandikishwa making it 7+7x2=21,yaani watu milioni 21 sio wananchi?

Yaani nusu ya population ya Tanzania wanaipenda Chadema,hao si wananchi ni vyenge?According to who?
Wengi waliipenda CDM ilipokuwa ikipambania wananchi. Mfano jinsi ilivyopambania ufisadi. Hii ya leo inapambana tu kuingia madarakani.
 
Kama kungekuwa na Tume HURU tungewauliza wananchi kwenye Uchaguzi halali.
 
CCM hoyeee!CCM tupo juu sana😁😁😁
AIsuRG.jpg
 
Hiki chama ni kundi tu la watu wanaotaka madaraka. Ukiangalia ugomvi wao wote na dola, kelele zao zote karibu asilimia 90 vinahusu wao kuingia madarakani.

Huwezi kuta CHADEMA wanaingia matatani na vyombo vya dola kisa walikusanyika kutetea wakulima wanaonyonywa na vyama vya ushirika, wanaonyimwa fursa ya kutafuta masoko nje nk. Huwezi kuta wameingia matatani kwa kutetea wafanyakazi kwa vitu kama fao la kujitoa au maslahi. Hawajawahi itisha maandamano kupinga kodi kandamizi kwa wafanyabiashara.

Wao siku zote maandamano yao yanahusu fursa za kuingia madarakani. Tena afdhali kipindi cha Slaa ambapo ilionekana shida kubwa ni ufisadi, na wananchi walichoka. Slaa akaishika hoja hiyo na chama kikapata nguvu kubwa sana.

Chama kinakubali kuingiza watu hata wasioamini kwenye sera zao, lengo lao ni kushika madaraka tu. Chama hiki kibadilike. Kisimamie na kupigania hoja zinazowahusu wananchi moja kwa moja. Mfano kikijaribu kujiweka kuwa mtetezi wa wakulima, kitavuna nguvu nyingi sana. Mtu akisikia kuwa wamekamatwa kwa sababu walikuwa wakipigania unyonyaji wa wakulima wa chai au mahindi inamuingia akikini kukutetea. lakini kwa mtindo huu wa kila siku kupigania namna ya kuingia madarakani kinaweza kufa kabisa.
Chama cha siasa ni nini? Na lengo lake ninini?
Mengine msiwe mnaandika ili kuficha ujinga wenu
 
Back
Top Bottom