MIMI NI MPENZI WA CHADEMA, YAFUATAYO NI MAONI YANGU KUHUSU HALI YA KISIASA NDANI YA CHADEMA LAKINI KWANZA NATOA HADHARI KWA VIONGOZI WOTE WA KITAIFA WA CHADEMA WASIFIKIRI KUWA CHADEMA ITAWEZA KUNUSURIKA KUSAMBARATIKA ENDAPO WATAENDELEZA MCHEZO WAO WA KUIGA NA KURITHI TABIA ZAKICCM AMBAZO WENYEWE WAMEDHAMIRIA KUONDOKANA NAZO BAADA YA KUKIPOTEZEA CHAMA MVUTO, NAZO NI PAMOJA NA UROHO WA MADARAKA WA KUANZA KUJIPANGA KUGOMBEA URAIS, UBUNGE N.K MAPEMA KIASI HIKI.
Matukio ya hivi karibuni ikiwemo kauli za Zitto kuhusu maazimio ya kikao cha Chadeama kilichofanyika Morogoro, japo yey si msamaji wa chama; kauli ya msemaji wa Chadema Mhe John Mnyika kukanusha kutojua lolote kuhusu kikao cha Morogoro na taarifa zinazopatikana katika mitandao kuwa ilikuwepo "retreat" ya viongozi wa Chadema huko Morogoro; ziara ya Katibu Mkuu wa Chama mkoani DSM, peke yake madai ya kuimarisha chama huku baadhi ya majimbo yakitengwa kama vile Jimbo la Ubungo; madai kuwa Josephine anahusika na kumhujumu Halima Mdee ili agombee jimbo la Kawe n.k Matukio haya na mengione mengi yanawalazimu wanachama na wapenzi wote wa Chadema waanze kutafakari kwa kina juu ya kuwepo kwa mgogoro wa chini kwa chini ndani ya Chadema.
Kwa muda mrefu sana CCM ilikuwa na migogoro kama hii lakini ikashindwa (1) Kwanza kukiri migogoro hiyo ipo ndani ya chama (2) Kuijadili na kuchuka hatua za kufaa kumaliza migogoro hiyo in a "win" "win" situation. Baada ya hatua hizo kuchukuliwa ndio maana leo hii tunaweza kumuona Nape na Lowassa wamekaa meza moja wakishiriki mkutano mmoja wa kujenga na kuimarisha chama. Tukaona picha za Dr Kingwangwala na Bashe wakikumbatiwa mabegani mmoja kulia na mwingine kushoto mwa makada wa CCM.
Haya yote ni matunda ya jitihada za vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa CCM inabaki imara ama sivyo kuporomoka kwa CCM kama ilivyokuwa ikitazamiwa kungeweza kuyumbisha amnai ya nchi. Ndio maana ukatibu Mkuu wa CCM kakabidhiwa mwanajeshi.
Hivyo Chadema wanatakiwa kuja na counter measures za kukabiliana na CCM mpya iliyookolewa na vyombo vya dola nazo sio kurithi yale CCM waliyolazimishwa kuyaacha kama vile kupanga safu mapema n.k.
Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa "Kama sio Muungano wazanziabri wasingekuwa wanasema sisi "Wazanzibari" katika madaia yao mbali mbali na badala yake wangekuwa wanasema sisi "Waunguja" na sisi "Wapemba" Hivyo dhambi ya ubaguzi Chadema waliyofanya dhidi ya vyama vingine vya upinzani katika wakati ambao watanzania walikuwa wakitegemea mabadiliko ya ukweli kutoka Chadema inaanza kukitafuna chama hicho kama alivyosema Baba wa taifa. Na kwa bahati mbaya Chadema haina dola ya kuweza kuingilia kati kurescue hali ya mambo ndani ya chama hicho. Chadema ikiyumba inapotea moja kwa moja and another wasted opportunity to bring really change in Tanzania.
Badala ya Wazee wa Chadema akina Mtei kuukemea upande mmoja wanapaswa kuja na solution za kitaifa kama vile Chadema kushirikiana kwa dhati na vyama vingine vya upinzani. Ni jambo hili tu litakaloweza kuhakiksha kuwa Chadema inabaki moja kutokana na ukweli kwamba itawabidi viongozi na wanachama wote wa Chadema waanze kuwaza, kufikiri na kutamka sisi Chadema badala ya kuwaza, kufikiri na kutamka mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k .
Japokuwa wazo hili linaweza kuonekana kama kuondoa "identity" ya viongozi wa Chadema na Chadema kama chama, lakini faida yake ni kuzuia kuporomoka na hatimaye kufifia kwa Chadema in the long run kutokana na hali ya mambo inavyoanza kujitokeza ndani ya Chadema baada ya mika miwili ya viongozi wake wa kitaifa kuwaza, kufikiri na kutamka kama mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k; matokeo yake wamesahau kuwa Chadema ndio inayowafanya waweze kuwa hapo walipo. Pia kukubali kushirikiana kwa dhati na vyama vingine maana yake ni kukubali kushirikana na makabila, dini na tamaduni mbali mbali kitu ambacho Chadema inadaiwa kutokuwa nacho. Hapa ndipomChadema inatakiwa kuiga mazuri ya CCM kwa kufanya "SWOT ANALYSIS" na kama CCM walivyokubali rushwa ipo ndani ya CCM, Ufisadi upo ndani ya CCM, kutokuwajibika kupo ndani ya CCM. Wanazuoni wanatuasa kuwa kutambua udhaifu wako ni 50% ya kuutatua, japokuwa hata kama ni kwadanganya watanzania kuwa watajirekebisha ili kunusurika 2015.
Ni lazima nayo Chadema ijitokeze ituambie watanzania nini madhaifu yake na ya viongozi wake inayotaka kuyafanyia kazi na kuyarekebisha? Ni utoto kwa viongozi wa Chadema kujidanganya kuwa wao ni malaika hawana mapungufu. Wakumbuke kuwa watanzania ni watu wazima waliokomaa wenye uwezo wa kubaina mazuri na mabaya na kuchagua kati ya mikuki miwili bora ya kuchomwa na mkiki upi.
Chadema wakumbuke kuwa watanzania waliwajaribu kidogo 2010, ili kuwapima ni ukweli kuwa wengi wa waliowaunga mkono na kuwapigia kura ni wanaccm kutokana na kuchoshwa na hayo mambo ya mizengwe na tamaa ya madaraka.