CHADEMA shirikianeni na vyama vingine vya upinzani ama sivyo mtapotea

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
MIMI NI MPENZI WA CHADEMA, YAFUATAYO NI MAONI YANGU KUHUSU HALI YA KISIASA NDANI YA CHADEMA LAKINI KWANZA NATOA HADHARI KWA VIONGOZI WOTE WA KITAIFA WA CHADEMA WASIFIKIRI KUWA CHADEMA ITAWEZA KUNUSURIKA KUSAMBARATIKA ENDAPO WATAENDELEZA MCHEZO WAO WA KUIGA NA KURITHI TABIA ZAKICCM AMBAZO WENYEWE WAMEDHAMIRIA KUONDOKANA NAZO BAADA YA KUKIPOTEZEA CHAMA MVUTO, NAZO NI PAMOJA NA UROHO WA MADARAKA WA KUANZA KUJIPANGA KUGOMBEA URAIS, UBUNGE N.K MAPEMA KIASI HIKI.

Matukio ya hivi karibuni ikiwemo
kauli za Zitto kuhusu maazimio ya kikao cha Chadeama kilichofanyika Morogoro, japo yey si msamaji wa chama; kauli ya msemaji wa Chadema Mhe John Mnyika kukanusha kutojua lolote kuhusu kikao cha Morogoro na taarifa zinazopatikana katika mitandao kuwa ilikuwepo "retreat" ya viongozi wa Chadema huko Morogoro; ziara ya Katibu Mkuu wa Chama mkoani DSM, peke yake madai ya kuimarisha chama huku baadhi ya majimbo yakitengwa kama vile Jimbo la Ubungo; madai kuwa Josephine anahusika na kumhujumu Halima Mdee ili agombee jimbo la Kawe n.k Matukio haya na mengione mengi yanawalazimu wanachama na wapenzi wote wa Chadema waanze kutafakari kwa kina juu ya kuwepo kwa mgogoro wa chini kwa chini ndani ya Chadema.

Kwa muda mrefu sana CCM ilikuwa na migogoro kama hii lakini ikashindwa (1) Kwanza kukiri migogoro hiyo ipo ndani ya chama (2) Kuijadili na kuchuka hatua za kufaa kumaliza migogoro hiyo in a "win" "win" situation. Baada ya hatua hizo kuchukuliwa ndio maana leo hii tunaweza kumuona Nape na Lowassa wamekaa meza moja wakishiriki mkutano mmoja wa kujenga na kuimarisha chama. Tukaona picha za Dr Kingwangwala na Bashe wakikumbatiwa mabegani mmoja kulia na mwingine kushoto mwa makada wa CCM.

Haya yote ni matunda ya jitihada za vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa CCM inabaki imara ama sivyo kuporomoka kwa CCM kama ilivyokuwa ikitazamiwa kungeweza kuyumbisha amnai ya nchi. Ndio maana ukatibu Mkuu wa CCM kakabidhiwa mwanajeshi.

Hivyo Chadema wanatakiwa kuja na counter measures za kukabiliana na CCM mpya iliyookolewa na vyombo vya dola nazo sio kurithi yale CCM waliyolazimishwa kuyaacha kama vile kupanga safu mapema n.k.

Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa "Kama sio Muungano wazanziabri wasingekuwa wanasema sisi "Wazanzibari" katika madaia yao mbali mbali na badala yake wangekuwa wanasema sisi "Waunguja" na sisi "Wapemba" Hivyo dhambi ya ubaguzi Chadema waliyofanya dhidi ya vyama vingine vya upinzani katika wakati ambao watanzania walikuwa wakitegemea mabadiliko ya ukweli kutoka Chadema inaanza kukitafuna chama hicho kama alivyosema Baba wa taifa. Na kwa bahati mbaya Chadema haina dola ya kuweza kuingilia kati kurescue hali ya mambo ndani ya chama hicho. Chadema ikiyumba inapotea moja kwa moja and another wasted opportunity to bring really change in Tanzania.

Badala ya Wazee wa Chadema akina Mtei kuukemea upande mmoja wanapaswa kuja na solution za kitaifa kama vile Chadema kushirikiana kwa dhati na vyama vingine vya upinzani. Ni jambo hili tu litakaloweza kuhakiksha kuwa Chadema inabaki moja kutokana na ukweli kwamba itawabidi viongozi na wanachama wote wa Chadema waanze kuwaza, kufikiri na kutamka sisi Chadema badala ya kuwaza, kufikiri na kutamka mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k .

Japokuwa wazo hili linaweza kuonekana kama kuondoa "identity" ya viongozi wa Chadema na Chadema kama chama, lakini faida yake ni kuzuia kuporomoka na hatimaye kufifia kwa Chadema in the long run kutokana na hali ya mambo inavyoanza kujitokeza ndani ya Chadema baada ya mika miwili ya viongozi wake wa kitaifa kuwaza, kufikiri na kutamka kama mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k; matokeo yake wamesahau kuwa Chadema ndio inayowafanya waweze kuwa hapo walipo. Pia kukubali kushirikiana kwa dhati na vyama vingine maana yake ni kukubali kushirikana na makabila, dini na tamaduni mbali mbali kitu ambacho Chadema inadaiwa kutokuwa nacho. Hapa ndipomChadema inatakiwa kuiga mazuri ya CCM kwa kufanya "SWOT ANALYSIS" na kama CCM walivyokubali rushwa ipo ndani ya CCM, Ufisadi upo ndani ya CCM, kutokuwajibika kupo ndani ya CCM. Wanazuoni wanatuasa kuwa kutambua udhaifu wako ni 50% ya kuutatua, japokuwa hata kama ni kwadanganya watanzania kuwa watajirekebisha ili kunusurika 2015.

Ni lazima nayo Chadema ijitokeze ituambie watanzania nini madhaifu yake na ya viongozi wake inayotaka kuyafanyia kazi na kuyarekebisha? Ni utoto kwa viongozi wa Chadema kujidanganya kuwa wao ni malaika hawana mapungufu. Wakumbuke kuwa watanzania ni watu wazima waliokomaa wenye uwezo wa kubaina mazuri na mabaya na kuchagua kati ya mikuki miwili bora ya kuchomwa na mkiki upi.

Chadema wakumbuke kuwa watanzania waliwajaribu kidogo 2010, ili kuwapima ni ukweli kuwa wengi wa waliowaunga mkono na kuwapigia kura ni wanaccm kutokana na kuchoshwa na hayo mambo ya mizengwe na tamaa ya madaraka.
 
mkuu tatizo sio kwamba CHADEMA haitaki kushirikiana na vyama vingine, ni vyama vingine havitaki kushirikia na CHADEMA. Mf CUF na NCCR wanaamini mpinzani wao ni CHADEMA na sio CCM, we hukuona kipindi kile cha uchaguzi 2010 yule mgombea wa UPDP aliagiza kura zake apewe kikwete?
 
First lady wa CDM ana nguvu kuliko viongozi wa chama.Kumbe na yeye anataka ubunge Mdee hangalia hi mambo.Huyu lazima atakuwa anatumia madawa haiwezekani Mzee wa miaka 70 aikane familia yake
 
CHADEMA kuungana na vyama vingine ni sawa kuungana na CCM
 
mkuu tatizo sio kwamba CHADEMA haitaki kushirikiana na vyama vingine, ni vyama vingine havitaki kushirikia na CHADEMA. Mf CUF na NCCR wanaamini mpinzani wao ni CHADEMA na sio CCM, we hukuona kipindi kile cha uchaguzi 2010 yule mgombea wa UPDP aliagiza kura zake apewe kikwete?

Mchaka Mchaka unaongelea mazingira ya 2010, 2014/5 itakuwa tofauti. Jiulize ni watanzania wangapi hawakupiga kura 2010? Moja ya sababu kuu ya wao kutokujitokeza ni kutokuamini upinzani wa chama kimoja kimoja. Inabidi katika upinzania watokee wazalendo wasio weka maslahi yao mbele ndio wataweza kuanzisha mchakato endelevu wa ushirikiano wa vyama vya upinzani. Ni kwa kulijua hilo watawala wakavitengea vyama vya siasa vya upinzani vinavyoshinda kidogo Ruzuku.

Tuzungumze ukweli ni kutokana na kuweka maslahi binafsi mbele ndio maana mgombea wetu wa 2010 kabla ya kukubali kupeperusha bendera yetu aliweka sharti la kiwango cha kulipwa ili akubali kugombea.

Sasa kiongozi kama huyu wa kuweka maslahi yake mbele unategemea anaweza kuwa na ajenda ambayo inaweza kumwondoa katika nafasi yake hiyo? Vyama vingine tunavisingizia bure tu, mchawi wetu ni sisi wenyewe kwa kubaguana.

CHADEMA ishirikiane na vyama vipi vya upinzani ?

Tuache kujidanganya na overconfidence. kwani hamkumsikia Mbowe juzi akimpamba JK kwa ajili ya kujengewa barabara jimbo la Hai, ina maana kwa kumpamba hivyo Chadema imeacha kuwa chama cha upinzani?
 
Mleta mada umetumwa na magamba wenye ndoa tayari na vyama hivyo.naona unataka kutuaminisha kuwa kuna mgogoro ila nimekupuuzia coz nawe unalea mfumo wenu wa DEVIDE AND RULE
 
Tuache kujidanganya na overconfidence. kwani hamkumsikia Mbowe juzi akimpamba JK kwa ajili ya kujengewa barabara jimbo la Hai, ina maana kwa kumpamba hivyo Chadema imeacha kuwa chama cha upinzani?

Unakurupuka hujibu maswali unayoulizwa, jibu CHADEMA washirikiane na chama gani?
 
Mkuu
chama cha upinzani Tanzania ni kimoja tu yaani Chadema.

CUF haiwezi kuungana na Chadema kwa sababu kuu zifuatazo;

-CUF ina ndoa na ccm-muafaka wa siri

-CUF ni chama tawala(Zanzibar)

-CUF mpinzani wake kisiasa ni Chadema si CCM

-CUF haioni Ufisadi wa CCM kama ni tatizo.

-CUF wana sera ya serikali ya umoja Wa kitaifa kwa kushirikiana na CCM kama watashinda uchaguzi

Yote hayo si kwa maslahi ya watanzania, hayasimamii nguvu ya umma inayoongozwa na Chadema.

Kwa NCCR ndio hata usiseme, ni chama Kibaraka. Ni chama kinachotumika kuhujumu nguvu ya upinzani.
kazi hii ya hujuma ya nguvu ya umma imefanywa vizuri sana na NCCR ingawa bila mafanikio.
Tumeshuhudia mwemyekiti wa CCM akimteua Mh Mbatia kuwa mbunge kama zawadi ya kazi nzuri.

Kumbuka hii ni fadhila kubwa kwa sababu Mwenyekiti wa CCM aliwaacha hata watu wake wa karibu ndani ya chama chake

Kama we ni mwana Chadema kweli, kitu ambacho nina wasi wasi nacho kwa sababu kwenye uzi wako unaelekea kuamini hata maneno ya kizushi, sasa sema kwa hali hii Chadema itaungana na chama gani cha upinzani!
 
Hii propaganda ya CCM siku nyingi sana bado ipo!! Kutaka kuwaaminisha Watz kuwa wapinzani ni lazima waungane ndipo waishinde CCM. Not scientific at all. Ok ushirikiano wa namna gani unaotaka kushauri ambao basi unataka watu makini wafuate au kutekeleza. Au ni almuradi ushirikiano. Hoja yako inapungua uchambuzi yakinifu.

Mathalani basi waambie hao unaotaka CHADEMA waungane nao au waulize kwa nini hawakuiunga mkono CHADEMA katika kuwania urais mwaka 2005 na 2010 kama ambavyo chama hiki kilifanya kwa CUF mwaka 2000 na 1995 kwa NCCR Mageuzi.

Nitakuwekea link hapa ili tuone njia mbalimbali za kuunganisha wapinzani, prons and cons zake, kisha uje tena ujenge hoja ukiwa well informed.
 
Mchaka Mchaka

Nafuu umeniwakilisha nitakavyo kwa mdau wetu!

Nimeipenda hii post yako!

mkuu tatizo sio kwamba CHADEMA haitaki kushirikiana na vyama vingine, ni vyama vingine havitaki kushirikia na CHADEMA. Mf CUF na NCCR wanaamini mpinzani wao ni CHADEMA na sio CCM, we hukuona kipindi kile cha uchaguzi 2010 yule mgombea wa UPDP aliagiza kura zake apewe kikwete?
 
Last edited by a moderator:
MIMI NI MPENZI WA CHADEMA, YAFUATAYO NI MAONI YANGU KUHUSU HALI YA KISIASA NDANI YA CHADEMA LAKINI KWANZA NATOA HADHARI KWA VIONGOZI WOTE WA KITAIFA WA CHADEMA WASIFIKIRI KUWA CHADEMA ITAWEZA KUNUSURIKA KUSAMBARATIKA ENDAPO WATAENDELEZA MCHEZO WAO WA KUIGA NA KURITHI TABIA ZAKICCM AMBAZO WENYEWE WAMEDHAMIRIA KUONDOKANA NAZO BAADA YA KUKIPOTEZEA CHAMA MVUTO, NAZO NI PAMOJA NA UROHO WA MADARAKA WA KUANZA KUJIPANGA KUGOMBEA URAIS, UBUNGE N.K MAPEMA KIASI HIKI.

Matukio ya hivi karibuni ikiwemo
kauli za Zitto kuhusu maazimio ya kikao cha Chadeama kilichofanyika Morogoro, japo yey si msamaji wa chama; kauli ya msemaji wa Chadema Mhe John Mnyika kukanusha kutojua lolote kuhusu kikao cha Morogoro na taarifa zinazopatikana katika mitandao kuwa ilikuwepo "retreat" ya viongozi wa Chadema huko Morogoro; ziara ya Katibu Mkuu wa Chama mkoani DSM, peke yake madai ya kuimarisha chama huku baadhi ya majimbo yakitengwa kama vile Jimbo la Ubungo; madai kuwa Josephine anahusika na kumhujumu Halima Mdee ili agombee jimbo la Kawe n.k Matukio haya na mengione mengi yanawalazimu wanachama na wapenzi wote wa Chadema waanze kutafakari kwa kina juu ya kuwepo kwa mgogoro wa chini kwa chini ndani ya Chadema.

Kwa muda mrefu sana CCM ilikuwa na migogoro kama hii lakini ikashindwa (1) Kwanza kukiri migogoro hiyo ipo ndani ya chama (2) Kuijadili na kuchuka hatua za kufaa kumaliza migogoro hiyo in a "win" "win" situation. Baada ya hatua hizo kuchukuliwa ndio maana leo hii tunaweza kumuona Nape na Lowassa wamekaa meza moja wakishiriki mkutano mmoja wa kujenga na kuimarisha chama. Tukaona picha za Dr Kingwangwala na Bashe wakikumbatiwa mabegani mmoja kulia na mwingine kushoto mwa makada wa CCM.

Haya yote ni matunda ya jitihada za vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa CCM inabaki imara ama sivyo kuporomoka kwa CCM kama ilivyokuwa ikitazamiwa kungeweza kuyumbisha amnai ya nchi. Ndio maana ukatibu Mkuu wa CCM kakabidhiwa mwanajeshi.

Hivyo Chadema wanatakiwa kuja na counter measures za kukabiliana na CCM mpya iliyookolewa na vyombo vya dola nazo sio kurithi yale CCM waliyolazimishwa kuyaacha kama vile kupanga safu mapema n.k.

Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa "Kama sio Muungano wazanziabri wasingekuwa wanasema sisi "Wazanzibari" katika madaia yao mbali mbali na badala yake wangekuwa wanasema sisi "Waunguja" na sisi "Wapemba" Hivyo dhambi ya ubaguzi Chadema waliyofanya dhidi ya vyama vingine vya upinzani katika wakati ambao watanzania walikuwa wakitegemea mabadiliko ya ukweli kutoka Chadema inaanza kukitafuna chama hicho kama alivyosema Baba wa taifa. Na kwa bahati mbaya Chadema haina dola ya kuweza kuingilia kati kurescue hali ya mambo ndani ya chama hicho. Chadema ikiyumba inapotea moja kwa moja and another wasted opportunity to bring really change in Tanzania.

Badala ya Wazee wa Chadema akina Mtei kuukemea upande mmoja wanapaswa kuja na solution za kitaifa kama vile Chadema kushirikiana kwa dhati na vyama vingine vya upinzani. Ni jambo hili tu litakaloweza kuhakiksha kuwa Chadema inabaki moja kutokana na ukweli kwamba itawabidi viongozi na wanachama wote wa Chadema waanze kuwaza, kufikiri na kutamka sisi Chadema badala ya kuwaza, kufikiri na kutamka mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k .

Japokuwa wazo hili linaweza kuonekana kama kuondoa "identity" ya viongozi wa Chadema na Chadema kama chama, lakini faida yake ni kuzuia kuporomoka na hatimaye kufifia kwa Chadema in the long run kutokana na hali ya mambo inavyoanza kujitokeza ndani ya Chadema baada ya mika miwili ya viongozi wake wa kitaifa kuwaza, kufikiri na kutamka kama mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k; matokeo yake wamesahau kuwa Chadema ndio inayowafanya waweze kuwa hapo walipo. Pia kukubali kushirikiana kwa dhati na vyama vingine maana yake ni kukubali kushirikana na makabila, dini na tamaduni mbali mbali kitu ambacho Chadema inadaiwa kutokuwa nacho. Hapa ndipomChadema inatakiwa kuiga mazuri ya CCM kwa kufanya "SWOT ANALYSIS" na kama CCM walivyokubali rushwa ipo ndani ya CCM, Ufisadi upo ndani ya CCM, kutokuwajibika kupo ndani ya CCM. Wanazuoni wanatuasa kuwa kutambua udhaifu wako ni 50% ya kuutatua, japokuwa hata kama ni kwadanganya watanzania kuwa watajirekebisha ili kunusurika 2015.

Ni lazima nayo Chadema ijitokeze ituambie watanzania nini madhaifu yake na ya viongozi wake inayotaka kuyafanyia kazi na kuyarekebisha? Ni utoto kwa viongozi wa Chadema kujidanganya kuwa wao ni malaika hawana mapungufu. Wakumbuke kuwa watanzania ni watu wazima waliokomaa wenye uwezo wa kubaina mazuri na mabaya na kuchagua kati ya mikuki miwili bora ya kuchomwa na mkiki upi.

Chadema wakumbuke kuwa watanzania waliwajaribu kidogo 2010, ili kuwapima ni ukweli kuwa wengi wa waliowaunga mkono na kuwapigia kura ni wanaccm kutokana na kuchoshwa na hayo mambo ya mizengwe na tamaa ya madaraka.

Itapotea WAPI? Umesikia MIKUTANO ya CUF wanavyosema kuhusu CHADEMA? Au Katibu Mkuu wa CHAMA KIPYA cha JAMII anavyoitaka CHADEMA iache MIKUTANO ya HADHARA?

Kwanini UISHI na NYOKA NGUONI MWAKO???
 
WATANABE wazo lako ni nzuri sana hata mimi nakuunga mkono! Tatizo lako ni kuwa hujui vyama gani vya kisiasa unavyosema. Je CUF TLP au UDP? Angalia history yao na viongozi wake utapat jibu. Vyama vyote hivyo ni pro-CCM! CHADEMA hakitokaa na wanafki!
 
Last edited by a moderator:
Tuache kujidanganya na overconfidence. kwani hamkumsikia Mbowe juzi akimpamba JK kwa ajili ya kujengewa barabara jimbo la Hai, ina maana kwa kumpamba hivyo Chadema imeacha kuwa chama cha upinzani?

Tatizo hivyo viti 40 vya ubunge Chadema wanaona wameshashinda.
 
Watabane(mzee wa SWOT analysis, ha ha ha haaaaaaaa!), ninakuunga mkono ktk uchambuzi wako ila ninapatwa na wasi wasi kama kweli wewe ni "mwadilifu", maana mmhhuuuu!
 
mimi ni mwanaccm mwenye card # .......... lakini kura yangu nitaipeleka chadema 2015!
Haruhitaji miungano(coalitions) ya kinafiki.
 
Itapotea WAPI? Umesikia MIKUTANO ya CUF wanavyosema kuhusu CHADEMA? Au Katibu Mkuu wa CHAMA KIPYA cha JAMII anavyoitaka CHADEMA iache MIKUTANO ya HADHARA?

Kwanini UISHI na NYOKA NGUONI MWAKO???

Hivi ni nani kati yenu hakusikia yote viongozi wa Chadema waliyosema dhidi ya CCM na viongozi wake. Mbona walikwenda Ikulu kumuona Jk, hivi hamkumsikia juzi Mbowe wakati wa uzinduzi wa barabara za Hai; ni yule Mbowe aliyetoka nje ya ukumbi wa Bunge. This is politics and not enemity!!!!!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom