CHADEMA shirikianeni na vyama vingine vya upinzani ama sivyo mtapotea

WATANABE wazo lako ni nzuri sana hata mimi nakuunga mkono! Tatizo lako ni kuwa hujui vyama gani vya kisiasa unavyosema. Je CUF TLP au UDP? Angalia history yao na viongozi wake utapat jibu. Vyama vyote hivyo ni pro-CCM! CHADEMA hakitokaa na wanafki!

Usisahau kuwa ilipo Chadema leo iliwahi kuwepo NCCR ikashindwa kutumia nafasi hiyo, ikaja CUF ikashindwa kutumia nafasi to win the hearts and minds of majority of Tanzanians who do not vote. Kama kuwa Pro-CCM kunapimwa kwa kusifia mazuri yaliyofanywa na CCM basi hata Chadema ni Pro CCM kwa kuwa Mwenyekiti wake juzi juiz alinukuliwa akimwita JK mchapakazi. Dr Slaa hivi karibuni alinukuliwa akimsifia JK kwa kuborehs sekta ya afya wakati anafungua jambo fulani pale CCBRT ambapo Dr Slaa ni mwasisi wake.

In that sense we have no opposition in this country kama kusifia jambo zuri la chama tawala ni kuwa Pro-CCM, hiyo ni dalili za watu wasiokomaa kisiasa na kupevuka kiakili. Kama hamkusikia wala kuona ingia kwenye youtube hapo chini

Freeman Mbowe alipomfagilia JK kwa juhudi zake za kuendeleza miundombinu Tanzania - YouTube

MBOWE4.jpg


MBOWE6.jpg


MBOWE5.jpg


KAMA KUSHIKANA MIKONO NA VIONGOZI WA CCM NI KUWA PRO CCM BASI WOTE WALIOKUNYWA JUICE IKULU NA TOKEA HAPO NI KUMMWAGIA JK ,ISIFA TU NDIO PRO CCM WA KWANZA
 
Kwa staili hii ya washabiki kufanya siasa JF badala ya mitaani walipo wananchi nakuhakikishi 2015 vitabaki 10

Kwa jibu hili umeonesha sura yako halisi. You're a die hard CCM zealot.

Umeulizwa mara 100 Je ni cha(vya)ma gani unashauri CDM iwe ushirikiano nacho/vyo. Mind you CUF na NCCR tayari wana ushirikiano na CCM.

This is a failed propaganda ya CCM, ya kutaka kuonesha CDM wana uchu wa madaraka. Huwezi kufanya ushirikiano na vyama mfu na vibaraka kama vya akina Dovutwa, Mrema, Cheyo etc.
 
Hii propaganda ya CCM siku nyingi sana bado ipo!! Kutaka kuwaaminisha Watz kuwa wapinzani ni lazima waungane ndipo waishinde CCM. Not scientific at all. Ok ushirikiano wa namna gani unaotaka kushauri ambao basi unataka watu makini wafuate au kutekeleza. Au ni almuradi ushirikiano. Hoja yako inapungua uchambuzi yakinifu.

Mathalani basi waambie hao unaotaka CHADEMA waungane nao au waulize kwa nini hawakuiunga mkono CHADEMA katika kuwania urais mwaka 2005 na 2010 kama ambavyo chama hiki kilifanya kwa CUF mwaka 2000 na 1995 kwa NCCR Mageuzi.

Nitakuwekea link hapa ili tuone njia mbalimbali za kuunganisha wapinzani, prons and cons zake, kisha uje tena ujenge hoja ukiwa well informed.

uKIANZA KUONA HAYO YALIYOTAJWA HAPO CHINI UJUE CHAMA KINANZA KUFIKIA TAMATI KAMA ILIVYOKUWA KWA CCM, BAHATI NJEMA CCM WANA DOLA AMBAO VIONGOZI WAKE WANANUFAIKA SANA KWA MFUMO WA RUSHWA ULIOPO HIVYO HAWAWEZI KUIRUHUSU CCM ISAMBARATIKE WATAINGILIA KAMA WALIBYOFANYA JUZI DODOMA NA KILA MTU NA KILA KUNDI KURUDI KUNDINI. NINYI CHADEMA MKIANZA KUSAMBARATIKA NANI ATAWARUDISHA KUNDINI?
NJI PEKKE YA KUKWEPA KUSAMBARATIKA NI KUJENGA UMOJA WA KITAIFA WA UPINZANI AMBAPO BADALA YA WANANCHADEMA KUSTRATEGISE AGAINST ONE ANOTHE WATASTRATEGISE AGAINST THE OTHER LOT. USHAURI HUU ALITOA BABA WA TAIFA. KAMA HAMNA HABARI WENYE AKILI NDANIA YABCHADEMA WASHAJUA NINI KINAENDELEA NA WAMEANZA KUJIJENGA BINAFSI KWA WATAWALA. NINYI WAPIGA DEBE KALAGA BAO!!!

[h=2]Re: DKT. SLAA ziarani ukaguzi uhai na ujenzi wa chama Dar Es Salaam[/h]
UZURI WA KIKAO CHA LEO PALE MWEMBE YANGA NILIKUWEPO TENA MEZA KUU
BABU ANAFANYA ZIARA YA KUTENGENEZA MTANDAO WA KE WA KICHAMA
BABU ANATENGENEZA UONGOZI WAKE(CHAIN OF COMMAND YAKE)

ANAPANDIKIZA UONGOZI USIO TAKIWA NDANI YA CHAMA,MGOGORO UNAOFUKUTA TEMEKE NADHANI IPO SIKU BABU ATARUDI KWA MCHUMBA WAKE AKIWA HOI

LEO WAZIWAZI ANAMLAZIMISHA MZEE URIO(HUYU NI MZEE ALIYEJENGA JENGO LA OFISI ZA CHAMA PALE TEMEKE-MWEMBE YANGA) ANAMLAZIMISHA AONDOKE KWENYE CHAMA KISA AMESHAZEEKA

SWALI:::DAR SLAA WEWE SI UPO KWENYE KOMA???VERY SAD NIMEONA LEO ALIVYOKONGOROKA AFYA YAKE,SIJAJUA MCHEZO GANI JOSEPHINE ANAUFANYA KWA BABU.


ZIARA YAKE HIYO TUTASIKIA MENGI HASA IKIFIKIA KULE MAENEO YA KAWE KWNEYE JIMBO LA HALIMA MDEE AMBAYE YUPO KWENYE UGOMVI MKALI SANA BAADA YA BABU KUNYIMWA PENZI NA HALIMA
BABU AMEUNDA ZENGWE AKISAIDIANA NA JANET YULE DIWANI WA KAWE ILI WAPANDIKIZE MAJUNGU NA FITINA KWA HALIMA ASIKUBALIKE NDANI YA CHAMA
I MEAN ANACHOKIFANYA BABU NI KUBOMOA CHADEMA NA KUJENGA CHADEMA YAKE BINAFSI

HALI HIYO YA HALIMA MDEE KUHALIBIWA JIMBONI KWAKE ILIJIDHIHIRISHA PALE BI.JOSEPHINE ALIPOWAANDAMANISHA WANAWAKE HADI MAKAO MAKUU YA KATIBU MKUU KWA MADAI KWAMBA HAWAMTAKI HALIMA MDEE(Nadhani Dr.slaa analo jibu,Tumain makene unalifahamu hatakama utakataa hapa)
SWALI HALIMA MDEE NA UJASIRI WAKE WOTE ULE WA KUKITETEA CHAMA LEO DR.SLAA ANAMUUNDIA ZENGWE AFUKUZWE????? ETI MWAKA 2015 BI.JOSEPHINE AGOMBEE KAWE.

NARUDI HAPA TUKESHE
 
wewe hujielewi.hivyo vyama vingine vinakufa sambamba na mlezi wao ccm sasa cdm kama chama kinachojipanga kutwaa dola kinawezaje kujiweka karibu na vyama vuinavyokufa?
 
wewe hujielewi.hivyo vyama vingine vinakufa sambamba na mlezi wao ccm sasa cdm kama chama kinachojipanga kutwaa dola kinawezaje kujiweka karibu na vyama vuinavyokufa?

Kwa taarifa yako CDM ya 2010 siyo ya sasa 2012 na mvuto wake unazidi kupungua kutokana na viongozi wake kutengeneza safu na mitandao ya kupambana wao wenyewe badala ya kupambana matatizo ya wananchi. Wabunge wengi hawaonekani katika majimbo yao Dr Slaa ameshindwa kabisa kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha majimbo na Katazyote zilizopigia kura CDM zinzkuwa kama Karatu badala yake amegeuka kiranja wa kufukuza madiwani
 
CHADEMA ishirikiane na vyama vipi vya upinzani ?

Swali lako zuri ndugu ataje chama. Pia ushauri wake kwa viongozi wa cdm ukiachana na lakuungana ni mzuri, hivyo viongozi mzingatia kwani mkituuzi tutawaacha mara moja angalieni watu tulivyo iludisha kata ya mlangali kundini! Hivyo tunawaomba muwe makini tunataka ukombozi wa kweli wa tz
 
Ni lazima nayo Chadema ijitokeze ituambie watanzania nini madhaifu yake na ya viongozi wake inayotaka kuyafanyia kazi na kuyarekebisha? Ni utoto kwa viongozi wa Chadema kujidanganya kuwa wao ni malaika hawana mapungufu. Wakumbuke kuwa watanzania ni watu wazima waliokomaa wenye uwezo wa kubaina mazuri na mabaya na kuchagua kati ya mikuki miwili bora ya kuchomwa na mkiki upi.

Chadema wakumbuke kuwa watanzania waliwajaribu kidogo 2010, ili kuwapima ni ukweli kuwa wengi wa waliowaunga mkono na kuwapigia kura ni wanaccm kutokana na kuchoshwa na hayo mambo ya mizengwe na tamaa ya madaraka.


Mkuu nakubaliana na wewe ka maelzo yako haya,lakini nakusikitikia kwa sababu utapewa za uso humu ndani leo mpaka utajiona hufai humu ndani,tena utapewa na hao hao wancdm wenzako,inaniuma sana.Hawa jamaa hawataki kuona ama kusikia ukweli na hasa hapa ambapo nimeweka red mkuu!



 
uKIANZA KUONA HAYO YALIYOTAJWA HAPO CHINI UJUE CHAMA KINANZA KUFIKIA TAMATI KAMA ILIVYOKUWA KWA CCM, BAHATI NJEMA CCM WANA DOLA AMBAO VIONGOZI WAKE WANANUFAIKA SANA KWA MFUMO WA RUSHWA ULIOPO HIVYO HAWAWEZI KUIRUHUSU CCM ISAMBARATIKE WATAINGILIA KAMA WALIBYOFANYA JUZI DODOMA NA KILA MTU NA KILA KUNDI KURUDI KUNDINI. NINYI CHADEMA MKIANZA KUSAMBARATIKA NANI ATAWARUDISHA KUNDINI?
NJI PEKKE YA KUKWEPA KUSAMBARATIKA NI KUJENGA UMOJA WA KITAIFA WA UPINZANI AMBAPO BADALA YA WANANCHADEMA KUSTRATEGISE AGAINST ONE ANOTHE WATASTRATEGISE AGAINST THE OTHER LOT. USHAURI HUU ALITOA BABA WA TAIFA. KAMA HAMNA HABARI WENYE AKILI NDANIA YABCHADEMA WASHAJUA NINI KINAENDELEA NA WAMEANZA KUJIJENGA BINAFSI KWA WATAWALA. NINYI WAPIGA DEBE KALAGA BAO!!!

Re: DKT. SLAA ziarani ukaguzi uhai na ujenzi wa chama Dar Es Salaam

UZURI WA KIKAO CHA LEO PALE MWEMBE YANGA NILIKUWEPO TENA MEZA KUU
BABU ANAFANYA ZIARA YA KUTENGENEZA MTANDAO WA KE WA KICHAMA
BABU ANATENGENEZA UONGOZI WAKE(CHAIN OF COMMAND YAKE)

ANAPANDIKIZA UONGOZI USIO TAKIWA NDANI YA CHAMA,MGOGORO UNAOFUKUTA TEMEKE NADHANI IPO SIKU BABU ATARUDI KWA MCHUMBA WAKE AKIWA HOI

LEO WAZIWAZI ANAMLAZIMISHA MZEE URIO(HUYU NI MZEE ALIYEJENGA JENGO LA OFISI ZA CHAMA PALE TEMEKE-MWEMBE YANGA) ANAMLAZIMISHA AONDOKE KWENYE CHAMA KISA AMESHAZEEKA

SWALI:::DAR SLAA WEWE SI UPO KWENYE KOMA???VERY SAD NIMEONA LEO ALIVYOKONGOROKA AFYA YAKE,SIJAJUA MCHEZO GANI JOSEPHINE ANAUFANYA KWA BABU.


ZIARA YAKE HIYO TUTASIKIA MENGI HASA IKIFIKIA KULE MAENEO YA KAWE KWNEYE JIMBO LA HALIMA MDEE AMBAYE YUPO KWENYE UGOMVI MKALI SANA BAADA YA BABU KUNYIMWA PENZI NA HALIMA
BABU AMEUNDA ZENGWE AKISAIDIANA NA JANET YULE DIWANI WA KAWE ILI WAPANDIKIZE MAJUNGU NA FITINA KWA HALIMA ASIKUBALIKE NDANI YA CHAMA
I MEAN ANACHOKIFANYA BABU NI KUBOMOA CHADEMA NA KUJENGA CHADEMA YAKE BINAFSI

HALI HIYO YA HALIMA MDEE KUHALIBIWA JIMBONI KWAKE ILIJIDHIHIRISHA PALE BI.JOSEPHINE ALIPOWAANDAMANISHA WANAWAKE HADI MAKAO MAKUU YA KATIBU MKUU KWA MADAI KWAMBA HAWAMTAKI HALIMA MDEE(Nadhani Dr.slaa analo jibu,Tumain makene unalifahamu hatakama utakataa hapa)
SWALI HALIMA MDEE NA UJASIRI WAKE WOTE ULE WA KUKITETEA CHAMA LEO DR.SLAA ANAMUUNDIA ZENGWE AFUKUZWE????? ETI MWAKA 2015 BI.JOSEPHINE AGOMBEE KAWE.

NARUDI HAPA TUKESHE

Dahhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!! Hii ni hatari na hasa kwa watu tunaowaamini,hata hivyo sitaki kuliamini hili kwa sasa,Labda Mwita Maranya,Pompoo,na wakina Makene mnaweza kulisema hili walau kidogo kwa ufafanuzi?!
 
MIMI NI MPENZI WA CHADEMA, YAFUATAYO NI MAONI YANGU KUHUSU HALI YA KISIASA NDANI YA CHADEMA LAKINI KWANZA NATOA HADHARI KWA VIONGOZI WOTE WA KITAIFA WA CHADEMA WASIFIKIRI KUWA CHADEMA ITAWEZA KUNUSURIKA KUSAMBARATIKA ENDAPO WATAENDELEZA MCHEZO WAO WA KUIGA NA KURITHI TABIA ZAKICCM AMBAZO WENYEWE WAMEDHAMIRIA KUONDOKANA NAZO BAADA YA KUKIPOTEZEA CHAMA MVUTO, NAZO NI PAMOJA NA UROHO WA MADARAKA WA KUANZA KUJIPANGA KUGOMBEA URAIS, UBUNGE N.K MAPEMA KIASI HIKI.

Matukio ya hivi karibuni ikiwemo
kauli za Zitto kuhusu maazimio ya kikao cha Chadeama kilichofanyika Morogoro, japo yey si msamaji wa chama; kauli ya msemaji wa Chadema Mhe John Mnyika kukanusha kutojua lolote kuhusu kikao cha Morogoro na taarifa zinazopatikana katika mitandao kuwa ilikuwepo "retreat" ya viongozi wa Chadema huko Morogoro; ziara ya Katibu Mkuu wa Chama mkoani DSM, peke yake madai ya kuimarisha chama huku baadhi ya majimbo yakitengwa kama vile Jimbo la Ubungo; madai kuwa Josephine anahusika na kumhujumu Halima Mdee ili agombee jimbo la Kawe n.k Matukio haya na mengione mengi yanawalazimu wanachama na wapenzi wote wa Chadema waanze kutafakari kwa kina juu ya kuwepo kwa mgogoro wa chini kwa chini ndani ya Chadema.

Kwa muda mrefu sana CCM ilikuwa na migogoro kama hii lakini ikashindwa (1) Kwanza kukiri migogoro hiyo ipo ndani ya chama (2) Kuijadili na kuchuka hatua za kufaa kumaliza migogoro hiyo in a "win" "win" situation. Baada ya hatua hizo kuchukuliwa ndio maana leo hii tunaweza kumuona Nape na Lowassa wamekaa meza moja wakishiriki mkutano mmoja wa kujenga na kuimarisha chama. Tukaona picha za Dr Kingwangwala na Bashe wakikumbatiwa mabegani mmoja kulia na mwingine kushoto mwa makada wa CCM.

Haya yote ni matunda ya jitihada za vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa CCM inabaki imara ama sivyo kuporomoka kwa CCM kama ilivyokuwa ikitazamiwa kungeweza kuyumbisha amnai ya nchi. Ndio maana ukatibu Mkuu wa CCM kakabidhiwa mwanajeshi.

Hivyo Chadema wanatakiwa kuja na counter measures za kukabiliana na CCM mpya iliyookolewa na vyombo vya dola nazo sio kurithi yale CCM waliyolazimishwa kuyaacha kama vile kupanga safu mapema n.k.

Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa "Kama sio Muungano wazanziabri wasingekuwa wanasema sisi "Wazanzibari" katika madaia yao mbali mbali na badala yake wangekuwa wanasema sisi "Waunguja" na sisi "Wapemba" Hivyo dhambi ya ubaguzi Chadema waliyofanya dhidi ya vyama vingine vya upinzani katika wakati ambao watanzania walikuwa wakitegemea mabadiliko ya ukweli kutoka Chadema inaanza kukitafuna chama hicho kama alivyosema Baba wa taifa. Na kwa bahati mbaya Chadema haina dola ya kuweza kuingilia kati kurescue hali ya mambo ndani ya chama hicho. Chadema ikiyumba inapotea moja kwa moja and another wasted opportunity to bring really change in Tanzania.


Badala ya Wazee wa Chadema akina Mtei kuukemea upande mmoja wanapaswa kuja na solution za kitaifa kama vile Chadema kushirikiana kwa dhati na vyama vingine vya upinzani. Ni jambo hili tu litakaloweza kuhakiksha kuwa Chadema inabaki moja kutokana na ukweli kwamba itawabidi viongozi na wanachama wote wa Chadema waanze kuwaza, kufikiri na kutamka sisi Chadema badala ya kuwaza, kufikiri na kutamka mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k .

Japokuwa wazo hili linaweza kuonekana kama kuondoa "identity" ya viongozi wa Chadema na Chadema kama chama, lakini faida yake ni kuzuia kuporomoka na hatimaye kufifia kwa Chadema in the long run kutokana na hali ya mambo inavyoanza kujitokeza ndani ya Chadema baada ya mika miwili ya viongozi wake wa kitaifa kuwaza, kufikiri na kutamka kama mimi Zitto,Mbowe,Slaa,Mnyika n.k; matokeo yake wamesahau kuwa Chadema ndio inayowafanya waweze kuwa hapo walipo. Pia kukubali kushirikiana kwa dhati na vyama vingine maana yake ni kukubali kushirikana na makabila, dini na tamaduni mbali mbali kitu ambacho Chadema inadaiwa kutokuwa nacho. Hapa ndipomChadema inatakiwa kuiga mazuri ya CCM kwa kufanya "SWOT ANALYSIS" na kama CCM walivyokubali rushwa ipo ndani ya CCM, Ufisadi upo ndani ya CCM, kutokuwajibika kupo ndani ya CCM. Wanazuoni wanatuasa kuwa kutambua udhaifu wako ni 50% ya kuutatua, japokuwa hata kama ni kwadanganya watanzania kuwa watajirekebisha ili kunusurika 2015.

Ni lazima nayo Chadema ijitokeze ituambie watanzania nini madhaifu yake na ya viongozi wake inayotaka kuyafanyia kazi na kuyarekebisha? Ni utoto kwa viongozi wa Chadema kujidanganya kuwa wao ni malaika hawana mapungufu. Wakumbuke kuwa watanzania ni watu wazima waliokomaa wenye uwezo wa kubaina mazuri na mabaya na kuchagua kati ya mikuki miwili bora ya kuchomwa na mkiki upi.

Chadema wakumbuke kuwa watanzania waliwajaribu kidogo 2010, ili kuwapima ni ukweli kuwa wengi wa waliowaunga mkono na kuwapigia kura ni wanaccm kutokana na kuchoshwa na hayo mambo ya mizengwe na tamaa ya madaraka.

Tatizo wasaliti wengi ndugu, yaani hakuna wa kumwamini hapo
 
Wewe ndugu hakuna umuhimu wa kuungana vyama vya upinzani au unalako jambo waambie michezo yenu tunaifahamu. Kuna hasara zaidi ya kushirikiana vyama kuliko faida.Ya kwanza vyama vingi vingine havina ufuasi wa kutosha ili kutengeneza mtandao kama ilionao chadema. Unaweza kuona chama kama CUF ni zanzibar Zaidi na Wilaya ya Kilwa. Pili vyama vingi vya siasa vipo pale ili kuisaidia CCM,iendelee kutawala.Tatu ukiunganisha vyama na mkashinda kutakuwa na ugomvi mkubwa wa kutekeleza sera na kutakuwa na migogoro baina ya vyama vilivyoshinda katika kugawana madaraka.Tuliona Kenya Wakati NARC ilivyoingia madarakani Kibaki na washirika wake wakina Odinga na Najib Balala, Kalonzo Msyoka Na wengine ikabidi Serikali ivunjwe.Nne vyama vingine havina Resources wala wanachama wenye uwezo wa kuvichangia kwaiyo viko choka mbaya, vinaweza kutembelea mgongo wa CDM.Cha muhimu ni kwa wananchi kuua vyama NGO kwa kujenga vyama viwili tu na hii inawezekana kwa kuvinyima kura vyama vingine utitiri. Na asikudanganye mtu CDM inaweza ikashirikiana na CUF lakini bado isipewe kura za wafuasi wa CUF. Sijapata kuona wafuasi wa chama cha Upinzani waliomchukia Mgombea WA CDM Kama wa CUF. CDM inaweza kabisa kushinda bila muungano wa ushirikiano na Vyama vingine. Bakili Muluzi wa Malawi alimshinda Kamuzu Banda kwa Chama cha UDF, bila muungano, Fredrick Chiluba alimshinda Kenneth Kaunda bila muungano.Michael chilufya Satta alimshinda Rupia Banda bila Muungano akiwa na PF party.Kwaiyo waaambie vyama dhaifu ndio waungane. CDM hapana. Dhaifu ndio huwa wanaungana ili kumpiga mwenye nguvu.
 
Angalau Mwimbuke tunaweza kujadili kuliko hao lot wengine

"Kuna hasara zaidi ya kushirikiana vyama kuliko faida.Ya kwanza vyama vingi vingine havina ufuasi wa kutosha ili kutengeneza mtandao kama ilionao chadema. Unaweza kuona chama kama CUF ni zanzibar Zaidi na Wilaya ya Kilwa"


Kumbuka kuwa watanzania ni watu ambao toka tupate uhuru tumezoeshwa "spoon feeding" tumejengewa uvivu wa kusoma na kutafuta habari na badala yake tukajengewa mfumo wa kulishwa habari hata kama ni za uongo, wengi wetu huziamini. Hii limelifanya taifa hili kupoteza historia yake ya mapambano ya kudai Uhuru baada ya wajanja wachache kulisha wenzao habari potofu kuhusu harakati za kutafuta uhuru na habari hizo potofu zikafundishwa hadi mashuleni kwa lengo la kupoteza historia rasmi ya harakati za kudai uhuru kwa maslahi ya kundi hilo.

Mkakati huu hata CDM imeutumia sana dhidi ya CUF kuhusu Serikali ya umoja wa kitaifa.

CCM ndio bingwa wa mkakati huu wa kulisha umma habari potofu, na mara nyingi CCM wameiweza Chadema kwa kutumia Mkakati huu kuulisha umma habari potofu kuwa
Chadema ni chama cha kikabila, cha kidini n.k Na habari hizi zimekuwa very damaging kwa CDM labda kama hamfanyi utafiti na tathmini ya katika kukubalika kwake. Feedback ya wananchi wengi ni kuwa kweli CDM wamesoma, wanajua sheria na kujenga hoja lakini ukabila na ukiristo. Kama ni kweli au la mimi sijui lakini hata 2014/5 CCM watatumia strategy hii kuimaliza Chadema tena. Lakini tuseme ukweli baadhi ya propaganda zinamvaa mtu kisawasawa. Hivi kama wengi wetu tungekuwa waislamu halafu "Padre" hata kama ni mstaafu agombee urais tungempa kura kweli? Halafu katika kampeni wananchi waambiwe kuwa Padre huyo kastaafu kiujanja tu anataka kuigeuza nchi iwe ya Kikiristo, hapo mgombea huyo si kamalizika kama baadhi ya wagombea na vyama wanavyomalizwa kwa kuitwa Mafisadi au CCM B tu.

Hivyo njia pekee ya kunusuru upinzani dhidi ya mtambo wa kupika propaganda wa CCM ni kushirikiana ambapo utakuta watu wa makabila, dini mbali mbali wakifanya kazi pamoja kwa lengo moja. Vile vile kwa mara ya kwanza watanzania watahamisika kwani kama watanzania walivyoichoka CCM pia watanzania wengi wamevichoka vyama vya Upinzani kimoja kimoja vinavyoibuka kipya kila msimu kutokana na mikakati maalum iliyowekwa na CCM.

Ushirikianao wa Vyama vya Upinzani utawaletea watanzania hamasa kubwa ya kushirkia upya katika siasa na kujitokeza kupiga kura, shauri lenu nyie cheleweni cheleweni hadi CCM ijiamarishe upya kama mtaweza kuitoa. Hivi sasa CCM ni mbogo aliyejeruhiwa, ukikaa vibaya anakumaliza moja kwa moja.


"Pili vyama vingi vya siasa vipo pale ili kuisaidia CCM,iendelee kutawala"
Hao wanaokataa kuunganisha vyama huku wakitumbua kodi za watanzania Milioni 400 kila mwezi ndio hao wapo hapo kwa ajili ya kuisaidia CCM kushinda. Viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema wasifikiri kuwa wao wana uhuru wa moja kwa moja wa kujiamulia mambo wanavyotaka kwa gharama za watanzania wote. Tunajua katika hili mtajitetea kama CCM kuwa Sheria ndio inasema hivyo.

Wakati tunaiunga mkono Chadema 2010 tulitegemea itakuwa pro-active na mara kwa mara kuitisha kura za maoni namna wapenzi wote tunavyotaka Chadema kiendeshwe ili kukipa sura ya kitaifa. Lakini kinachotokea sasa ni tofauti kabisa sawa kabisa na CCM-Rais ndie Mwenyekiti wa Chama; Chadema Mkuu wa Upinzani ndio Mwenyekiti wa Chama. CCM mawaziri ni wajumbe wa Halmashauri/Kamati Kuu; Chadema wabunge wajumbe wa Kamati Kuu na Halmsahauri Kuu ya Chadema n.kSasa hapo nani atampima mwingine? Ndio maana Chadema imeanza kuchoka mapema kuliko tulivyotarajia kutokana na ukweli hamna new thinking; wale wale wanaokuwa pamoja Dodoma kwa miezi kadhaa ndio hao hao wanaokuwa pamoja makao makuu ya chama. Hamna jipya!!!


"Tatu ukiunganisha vyama na mkashinda kutakuwa na ugomvi mkubwa wa kutekeleza sera na kutakuwa na migogoro baina ya vyama vilivyoshinda katika kugawana madaraka.Tuliona Kenya Wakati NARC ilivyoingia madarakani Kibaki na washirika wake wakina Odinga na Najib Balala, Kalonzo Msyoka Na wengine ikabidi Serikali ivunjwe".
Huo wewe unaoita ugomvi ndio constructive criticism inayofanya nchi ya Kenya kupata Katiba murua inayowatema wala Rushwa kila siku. Utaona hapa Katiba Tanznaia itachakachuliwa na hakuna lolote la maana litakalofanyika. na Hali itaendelea kuwa business as usual hii ni kwa sababu ya ubinafsi wa watu kama Chadema. Tazama Fly Overs, Bandari Treni za kwenda kazi na kuka maradufu kwa uchumi wa Kenya vyote vimewezekana chini ya Serikali hii ya vyma kushirikina


"Nne vyama vingine havina Resources wala wanachama wenye uwezo wa kuvichangia kwaiyo viko choka mbaya, vinaweza kutembelea mgongo wa CDM"
Hizo ni kauli za kufuru mwaka 2009, mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu Chadema nayo ilikuwa choka mbaya nakumbuka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 nilipigiwa simu na bwana moja ambaye sasa ni mheshimiwa ili niwalipe mawakala wa Chadema waliosimamia uchaguzi huo katika kata ninayoishi.

Hata 2010 Chadema ilikuwa Choka mbaya hata katika baadhi ya majimbo hapo mjini Dar ambapo ilibidi tupitishe bakuli kwa kwenda mbele kutoka kwa kila mtaka mabadiliko ili mgombea tuliyekuwa tukimuunga mkono ashinde. Na alishinda.


"Na asikudanganye mtu CDM inaweza ikashirikiana na CUF lakini bado isipewe kura za wafuasi wa CUF. Sijapata kuona wafuasi wa chama cha Upinzani waliomchukia Mgombea WA CDM Kama wa CUF"

Sababu za wanachama wa CUF kumchukia mgombea wa CDM nimeshazieleza hapo juu. Ni propaganda za CCM kuwa huyo "Padre anataka kugeuza nchi iwe ya Kikiristo". Hapo CCM wameshamaliza kazi kwa kufanikiwa kujenga uadui kati ya CDM na CUF vyama viwili vyenye nguvu kubwa. Lakini nakuhakikishia kuwa iwapo viongozi wetu wa vyama hivi viwli watakuwa wazalendo na kukubali kushirikiana, hicho kitakuwa ni kimbunga cha kutosha kuiondoa CCM madarakani.
Tatizo la viongozi wa CDM na wanaCDM wengi ni wachanga katika siasa hawatambui mtaji wa kipekee CUF inaoushikilia wa 50% ya kura za Zanzibar. Kwa katiba hii ya Tanzania ya sasa na zijazo CUF isi there to stay kutokana na mtaji huu. Hawa ndio wanaojua siasa. Walipoona wananchi wanaonyesha dalili za kuchoka hali ya kukosa amani kwa kipindi kirefu wakakubali kuwapa wananchi likizo kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Chadema licha ya kujifanya wasomi inashindwa hata kufanya survey ni kwanini wananchi hawajitokezi kupiga kura ili waweze kujirekebisha to thata direction


"Kwaiyo waaambie vyama dhaifu ndio waungane. CDM hapana. Dhaifu ndio huwa wanaungana ili kumpiga mwenye nguvu"

Kwa mtu anayejua siasa kati ya Chadema na CUF ni kipi chama dhaifu Kitaifa? Ni Chadema kilichoshindwa kuwaandaa wananchi wake kulind kura za urais Mwaka 2010, wapenzi walilinda kura za wabunge wao tu na kuacha system kuchakachua kura za Dr Slaa. Lakini kutoka na kuw makini CUF wamekuwa wakifanikiwa kulinda kura zao za urais Zanzibar hadi zichakachuliwe kwa mtutu wa bunduki kila mtu akishuhudia.

Kutokana na CUF kuwa wakomavu katika nynanja ya siasa walifanya siasa huku Tanzania bara na kubaini watu wa bara hawana uzalendo na uchungu na nchi yao ndio maana wamewekeza huko Zanzibar ambako wana 50% ya kura zote. Lini uliwahi kusikia mpinzani Zanzibar kauza shahada yake ya kupigia kura?.Pamoja an umaskini wote uliopo Pemba lini uliwahi kusikia mpinzani kapokea fulana, khanga, sukari, mafuta ya kura n.k toka CCM kwa ajili ya kukipigia kura?. Ndio maana CUF kwa Zanziba na Pemba huweza kutoa idadi ya kura zao kabla hazijapigwa na matokeo kuonyesha kuwa walikuwa sahihi kwa asilimi kubwa sana.


"CDM inaweza kabisa kushinda bila muungano wa ushirikiano na Vyama vingine. Bakili Muluzi wa Malawi alimshinda Kamuzu Banda kwa Chama cha UDF, bila muungano, Fredrick Chiluba alimshinda Kenneth Kaunda bila muungano.Michael chilufya Satta alimshinda Rupia Banda bila Muungano akiwa na PF party"
Tatizo la Tanzania bara karibu wananchi wote ni mafisadi
kutengenezwa na CCM, wanatumia kuliko mapato yao hivyo huwezi kuwalinganisha na nchi ulizotaja. Nchini Zambia Chiluba alikuwa mtu kutoka vyama vya wafanyakazi ndio maana akaweza kushinda. Tazama vyama vyetu vya wafanyakazi vilishachakachuliwa toka tupate uhuru, viongozi wao wapo maofisini kuendesha ufisadi wa michango ya wanachama wao. Hata viongozi hao wa vyama vya wafanyakazi Tanzania kama walivyo viongozi wa vyombo vya usalama hawataki CCM itoke madarakani kwa kuwa wanaedesha ufiasdi katika nafasi zao.

USHAURI WA BURE


Sasa ni miaka miwili toka Chadema iwe Chama Kikuu cha Upinzani, kipindi hiki kinatosha kwa kujipanga na sasa tunataka kuona Chama chenye sura ya Chama Kikuu cha Upinzani kwa maana ya maneno na vitendo vifafanane.

Hakuna kitu kinashusha heshma ya Chadema
kama upuuzi wa Dr Slaa kuendelea kutumia Chadema kuhalalisha ufuska. Awali wote hatukuifahamu vizuri issue ya Dr Slaa/Josephin/Rose Kamili Lakini hivi karibuni Mahakama imetamka kuwa DR Slaa na kesi ya kujibu katika Shauri lilofunguliwa na Mhe Rose Kamili kwa kuwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya 1971, Mahakama ilisema "Ndoa itahesabika kuwa ipo kama Mwanaume na Mwamnamke waliishi pamoja kwa miaka miwili".

Baada ya kauli hii ya Mahakama wenye akili
tunamtarajia mtu mwenye busara za kiurais shauri hili na Mke wake halali Mhe Rose Kamili nje ya Mahakama na nje ya Chadema ili kunusuru heshima ya Chadema. Weakness kama hizi ni hatari sana kwa uhai wa chama tena kwa mtu anayetaka tumkabidhi madraka makubwa kabisa katika nchi hii. Kama anashindwa kuongoza Mama zetu wawili tu, ataweza vipi kuongoza taifa?

Nakaribisha matusi yenu Aluta Continua Tumechoka na Ubabaishaji!!!!!

 
Hii propaganda ya CCM siku nyingi sana bado ipo!! Kutaka kuwaaminisha Watz kuwa wapinzani ni lazima waungane ndipo waishinde CCM. Not scientific at all. Ok ushirikiano wa namna gani unaotaka kushauri ambao basi unataka watu makini wafuate au kutekeleza. Au ni almuradi ushirikiano. Hoja yako inapungua uchambuzi yakinifu.

Mathalani basi waambie hao unaotaka CHADEMA waungane nao au waulize kwa nini hawakuiunga mkono CHADEMA katika kuwania urais mwaka 2005 na 2010 kama ambavyo chama hiki kilifanya kwa CUF mwaka 2000 na 1995 kwa NCCR Mageuzi.

Nitakuwekea link hapa ili tuone njia mbalimbali za kuunganisha wapinzani, prons and cons zake, kisha uje tena ujenge hoja ukiwa well informed.

Nimegundua Makene unapalilia ajira tu hapo ulipo. Makene unaniruhusu niweke wazi dongo ulilomrushia Dr. Slaa juzi tukiwa pale school of journalism and mass comm. ya UDSM? Niyaanike madongo yale? Ulisema Dr. ni dikte.....? halafu ni nani tena?.
 
Nimegundua Makene unapalilia ajira tu hapo ulipo. Makene unaniruhusu niweke wazi dongo ulilomrushia Dr. Slaa juzi tukiwa pale school of journalism and mass comm. ya UDSM? Niyaanike madongo yale? Ulisema Dr. ni dikte.....? halafu ni nani tena?.
taratiiibu na upumbavu nao unaanza kujitokeza..
 
Back
Top Bottom