CHADEMA: Serikali inaendesha Operation ya kuhamisha watu kwa nguvu Ngorongoro

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU SERIKALI KUENDESHA OPERESHENI YA KUWAHAMISHA KWA NGUVU WANANCHI WILAYA YA NGORONGORO

Kwa Muda mrefu sasa pamekuwa na mgogoro baina ya Serikali na wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro wanaoishi katika vijiji 14 ambao Serikali inawataka wahame kwenye ardhi yao ya asili na wahamie Mkoa wa Tanga ,Wilaya ya Handeni.

Wananchi hao wanapinga kuhamishwa kwenye ardhi yao ya asili, na katika kupinga huko waliamua kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika Masshariki,. Shauri ambalo linategemewa kutolewa uamuzi mwezi huu 22 Juni,2022.

Wakati wananchi wakisubiri uaamuzi wa Mahakama, Serikali imeamua kutumia nguvu Kwa kupeleka Jeshi la Polisi na silaha za Moto kwenda kuweka mipaka na kuwataka wananchi hao kuhama katika vijiji vyao.

Katika kuthibitisha matumizi ya nguvu ambayo yanafanywa na Jeshi la Polisi , Madiwani 8 wa Kata pamoja na 2 wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngorongoro.

Wenyeviti na watendaji wa Kata na vijiji kutoka vijiji 14 kuna taarifa kwamba wamenyanganywa mihuri ambayo ni kitendea kazi muhimu katika majukumu Yao.

Aidha, Leo Ijumaa tarehe 10 Juni,2022 kumekuwepo taarifa kwamba Polisi wametumia risasi za Moto na mabomu ya machozi kuwakabili wanakijiji hao na wapo ambao wamejeruhiwa na kuna taarifa ya kuwa kuna Raia wamepoteza maisha!

Tunatoa mwito wa hatua zifuatazo zichukuliwe na vyombo vinavyohusika ili kuliepusha Taifa letu kuingia kwenye machafuko na hata hatari ya kutumbukia kwenye mauaji ya kimbari ( Genocide) kama ifuatavyo;

1. Serikali iache matumizi ya nguvu,vitisho na ubabe katika wakati huu ambao wanataka kuwahamisha wananchi katika Wilaya hiyo. Serikali itambue kuwa imesaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa ya kulinda na kuheshimu Haki za Binadamu, hivyo wazingatie sheria za nchi na mikataba ya Kimataifa.

2. Serikali itambue kuwa wananchi hawa Wana Haki Yao ya asili ya kuishi katika maeneo hayo pamoja na kuwa wanalindwa na sheria ya ardhi ya vijiji , hivyo katika Muda wote sheria isimamiwe kikamilifu.

3. Serikali iheshimu utawala wa sheria na hasa utii wa Mahakama, watambue kuwa kuna shauri lipo Mahakamani, hivyo wasubiri uamuzi wa Mahakama, kamwe wasiingilie Uhuru wa Mahakama.

4. Serikali iwaachie huru viongozi wote wa wananchi ambao inawashikilia ili wakaendelee na wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na kujenga uchumi wa Taifa .

5. Tunamtaka Spika wa Bunge Tulia Ackson atambue kuwa Bunge ndio chombo cha wananchi na kinawajibika kuwalinda na kuwatetea wakati wote. Hivyo aache kuwa upande wa Serikali na aache kuwatisha wananchi ambao wanatoa taarifa kutoka Loliondo, badala yake atumie Mamlaka yake kama mhimili Kwa mujibu wa sheria na kanuni za Bunge kuunda Kamati teule ya kufuatilia sakata hili na kutoa taarifa yake Bungeni ili ijadiliwe na Bunge liweze kuazimia.

Tunamkumbusha kuwa yalipotokea mauaji ya Raia yaliyofanywa na Askari wanyamapori Bunge liliunda Kamati teule na ambayo ripoti yake ilipelekea Mawaziri kadhaa kuondolewa Madarakani, hivyo aache kuwa sehemu ya Serikali na atumie Mamlaka yake kuutafuta ukweli Kwa Maslahi ya Taifa.

6. Tunatoa mwito kwa vyombo vya habari vyote pamoja na asasi za kiraia kuendelea kufuatilia sakata hili na kutoa taarifa bila upendeleo. Aidha, tunaitaka Serikali na vyombo vyake waache kuvitisha na badala yake wafuatilie usahihi wa taarifa hizo Kwa ustawi wa Taifa letu.

Mwisho tunalaani Kwa nguvu zote matumizi makubwa ya nguvu na uvunjifu wa Haki za Binadamu unaoendelea kufanywa na Serikali na vyombo vyake katika Wilaya ya Ngorongoro.

John Mrema- Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje

Imetolewa Leo Ijumaa tarehe 10 Juni, 2022.
 
Duh...!. kwanini mpaka sasa nafasi ya Tumaini Makene bado haijapata a competent replacement?!, sio kila mtu anaweza kuongea!.
P
Kesi ya Mbowe ulikaa kimya,Ngoro Ngoro kimya,binafsi naamin sio kwamba hujui ila Kuna upande unaegemea au ndo diameter officer?Sasa mtu katoa hoja badala ya kuchangia au kukaa kimya wewe unamshambulia mtu,sasa ndo nini

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Kuna mengi yamejificha Mgogoro huu wa Ngorongoro

Tuuangalie kwa jicho la tatu ....I have been there for almost 5 years...UZEMBE RUSHWA UWAJIBIKAJI ...trans boundaries watch dogs.....watu kujipatia pesa juu yawatu....KUJIFICHA KWA KUTUMIA VIVULI VINAVYO FANANA etc

Ref Majambazi ya Kisomali enzi hizo na Sonjo conflict
 
kuna mengi huyu bwana bila kumstop haraka alikuwa ana mwaga mbonga
IMG_7437.jpg
 
Hajawahi kutokea Waziri mkuu Mwongo kama huyu wa awamu hii halafu Mwislamu .
 
Serikali iwaachie mara moja iliowakamata bila masharti yeyote.

Na kuacha kuvunja sheria za kimataifa za kuwapa uhuru wananchi kuishi wanakotaka.
 
TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU SERIKALI KUENDESHA OPERESHENI YA KUWAHAMISHA KWA NGUVU WANANCHI WILAYA YA NGORONGORO

Kwa Muda mrefu sasa pamekuwa na mgogoro baina ya Serikali na wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro wanaoishi katika vijiji 14 ambao Serikali inawataka wahame kwenye ardhi yao ya asili na wahamie Mkoa wa Tanga ,Wilaya ya Handeni.

Wananchi hao wanapinga kuhamishwa kwenye ardhi yao ya asili, na katika kupinga huko waliamua kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika Masshariki,. Shauri ambalo linategemewa kutolewa uamuzi mwezi huu 22 Juni,2022.

Wakati wananchi wakisubiri uaamuzi wa Mahakama, Serikali imeamua kutumia nguvu Kwa kupeleka Jeshi la Polisi na silaha za Moto kwenda kuweka mipaka na kuwataka wananchi hao kuhama katika vijiji vyao.

Katika kuthibitisha matumizi ya nguvu ambayo yanafanywa na Jeshi la Polisi , Madiwani 8 wa Kata pamoja na 2 wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngorongoro.

Wenyeviti na watendaji wa Kata na vijiji kutoka vijiji 14 kuna taarifa kwamba wamenyanganywa mihuri ambayo ni kitendea kazi muhimu katika majukumu Yao.

Aidha, Leo Ijumaa tarehe 10 Juni,2022 kumekuwepo taarifa kwamba Polisi wametumia risasi za Moto na mabomu ya machozi kuwakabili wanakijiji hao na wapo ambao wamejeruhiwa na kuna taarifa ya kuwa kuna Raia wamepoteza maisha!

Tunatoa mwito wa hatua zifuatazo zichukuliwe na vyombo vinavyohusika ili kuliepusha Taifa letu kuingia kwenye machafuko na hata hatari ya kutumbukia kwenye mauaji ya kimbari ( Genocide) kama ifuatavyo;

1. Serikali iache matumizi ya nguvu,vitisho na ubabe katika wakati huu ambao wanataka kuwahamisha wananchi katika Wilaya hiyo. Serikali itambue kuwa imesaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa ya kulinda na kuheshimu Haki za Binadamu, hivyo wazingatie sheria za nchi na mikataba ya Kimataifa.

2. Serikali itambue kuwa wananchi hawa Wana Haki Yao ya asili ya kuishi katika maeneo hayo pamoja na kuwa wanalindwa na sheria ya ardhi ya vijiji , hivyo katika Muda wote sheria isimamiwe kikamilifu.

3. Serikali iheshimu utawala wa sheria na hasa utii wa Mahakama, watambue kuwa kuna shauri lipo Mahakamani, hivyo wasubiri uamuzi wa Mahakama, kamwe wasiingilie Uhuru wa Mahakama.

4. Serikali iwaachie huru viongozi wote wa wananchi ambao inawashikilia ili wakaendelee na wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na kujenga uchumi wa Taifa .

5. Tunamtaka Spika wa Bunge Tulia Ackson atambue kuwa Bunge ndio chombo cha wananchi na kinawajibika kuwalinda na kuwatetea wakati wote. Hivyo aache kuwa upande wa Serikali na aache kuwatisha wananchi ambao wanatoa taarifa kutoka Loliondo, badala yake atumie Mamlaka yake kama mhimili Kwa mujibu wa sheria na kanuni za Bunge kuunda Kamati teule ya kufuatilia sakata hili na kutoa taarifa yake Bungeni ili ijadiliwe na Bunge liweze kuazimia.

Tunamkumbusha kuwa yalipotokea mauaji ya Raia yaliyofanywa na Askari wanyamapori Bunge liliunda Kamati teule na ambayo ripoti yake ilipelekea Mawaziri kadhaa kuondolewa Madarakani, hivyo aache kuwa sehemu ya Serikali na atumie Mamlaka yake kuutafuta ukweli Kwa Maslahi ya Taifa.

6. Tunatoa mwito kwa vyombo vya habari vyote pamoja na asasi za kiraia kuendelea kufuatilia sakata hili na kutoa taarifa bila upendeleo. Aidha, tunaitaka Serikali na vyombo vyake waache kuvitisha na badala yake wafuatilie usahihi wa taarifa hizo Kwa ustawi wa Taifa letu.

Mwisho tunalaani Kwa nguvu zote matumizi makubwa ya nguvu na uvunjifu wa Haki za Binadamu unaoendelea kufanywa na Serikali na vyombo vyake katika Wilaya ya Ngorongoro.

John Mrema- Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje

Imetolewa Leo Ijumaa tarehe 10 Juni, 2022.
Kwa hiyo CHADEMA mnataka kuiaminisha Dunia kwamba kuna Genocide Loliondo?

Je kabla ya kuja na andiko hili kutoka Ufipa Street Kinondoni.

Kuna muwakilishi yeyote wa chadema aliyefika eneo la tukio na kujiridhisha na tuhuma zenu kwa serikali.
Kabla ya kuandika tamko ambalo kiuhalisia limejaa habari za kuambiwa.
 
Back
Top Bottom