Chadema:Serikali iandae upinzani kuingia Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema:Serikali iandae upinzani kuingia Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtwana, Oct 24, 2012.

 1. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  SERIKALI imetakiwa kuandaa mfumo wa kikatiba utakaowezesha chama cha upinzani kuongoza iwapo kile kinachotawala kitaondolewa madarakani.Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipokuwa akihutubia mikutano ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata za Mpapa, wilayani Momba na Myovizi, Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya.

  Alisema kutokana na vuguvugu la siasa za mabadiliko zinazoendelea nchini, ni wakati mwafaka nchi ikawa na mfumo wa kikatiba na sheria kwa ajili ya kusimamia mabadiliko ya uongozi kufanyika kwa amani ili kuepusha nchi kuingia katika vurugu na mkanganyiko wa kisiasa.

  Mbowe alisema ingawa hiyo inaweza kuonekana kuwa ni dhana mpya, kutokana na umuhimu wake kwa ajili ya mustakabali mwema wa Taifa, ni vyema Watanzania wakaanza kuitafakari.
Alitola mifano wa Ghana ilivyopitia misukosuko kutoka utawala wa Jerry Rawlings kwenda chama cha upinzani cha Rais John Kufour.

  Akiwanadi wagombea wa Chadema katika maeneo hayo, Mbowe alisema ni hatari kwa nchi kama Tanzania ambayo sasa inapitia kwenye wimbi kubwa la mabadiliko, kukosa mfumo huo wa kuhakikisha mabadiliko ya mpito kutoka utawala wa Serikali moja kwenda nyingine yanafanyika kwa amani na kulinda masilahi ya nchi bila vurugu.

  "Ni muhimu sana kuwa na sheria itakayohakikisha 'transition' (kipindi cha mpito) kutoka Serikali ya chama fulani kwenda chama kingine au Serikali moja kwenda Serikali nyingine, kufanyika kwa amani na kwa kuhakikisha masilahi ya umma na nchi yanazingatiwa," alisema na kuongeza:

  "Lazima tuepuke hali kama hiyo. Wenzetu wale (Ghana) walijifunza, walipoingia madarakani wakaamua kutunga sheria ya kusimamia ‘transition period' kutoka uongozi wa Serikali moja kwenda nyingine."

  "Watanzania wanaweza kujiuliza kwa nini Marekani inachukua siku 72 kwa Rais kuapishwa na kukabidhiwa rasmi mamlaka ya kuongoza nchi tangu achaguliwe? Ni kwa sababu kuna vitu vya muhimu sana vya kusimamiwa na kufanyiwa kazi kabla utawala mpya haujakabidhiwa Ikulu."

  Mbowe alisema hapa nchini upo mfano mzuri wa madhara ya kukosekana kwa sheria ya namna hiyo ya kusimamia kipindi hicho cha mpito.

  Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alidai kwamba sehemu ya mabilioni ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) yalihamishwa kutokana na kukosekana kwa mfumo huo.

  Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema wakati Marekani inachukua takriban siku 72 tangu uchaguzi na uongozi mpya kukabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi, Tanzania inachukua wastani wa saa 48 pekee, akisema hali hiyo ni hatari kwa nchi kwani, kuna masuala ya msingi ambayo yanahitaji muda wa kutosha katika kufanya makabidhiano kutoka Serikali moja kwenda nyingine.

  "Ni wakati mwafaka kuanza kufikiria kuwa na mfumo huu wa kikatiba na kisheria. Huwezi kutumia saa 48 tangu uchaguzi kufanyika kumkabidhi Rais mpya madaraka. Kwanza kwa muda huo nani anasimamia kikamilifu rasilimali za umma, nini hatma ya watumishi wa umma. Kuna masuala ya majeshi, nyaraka za siri na kila kitu, vitu ni vingi. Wenzetu walio makini na nchi zao wanajua umuhimu wa masuala kama haya. Wanapata muda wa kufanya 'orientation' (uelewa wa mazingira), alisema Mbowe na kuongeza:

  "Ndiyo maana hapa kuna wakati watumishi wa Serikali wakaamua tu kuikumbatia CCM hata kama nao wameichoka, kwa sababu wanakuwa hawajui hatma yao ni nini kwenye Serikali au uongozi mpya, baada ya uchaguzi.

  "Ghana katika kipindi hicho cha mpito kutoka Serikali moja hadi nyingine wameweka utaratibu wa mamlaka inayoongozwa na mtu ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa anasimamia rasilimali zote, nyaraka zote, zinakuwa zimeandikishwa, zinajulikana zikoje."
  Alisema lazima hatari hiyo izuiliwe kwa kuwa wakati Serikali mpya ilivyoingia Ghana, waliokuwepo madarakani walichoma moto nyaraka muhimu na kuharibu vitu, kitendo kilichosababisha Serikali iliyoingia madarakani kuhangaika kuanza upya.

  Alisema kutokana na hali kama hiyo ni lazima wananchi waanze kudai mfumo huo kwani hivi sasa Katiba na sheria ziko kimya kitu kinachoweza kusababisha siku moja mtu akakabidhi ukuta wa Ikulu tu kukiwa hamna kitu ndani.
  "Mfumo huo utahakikisha 'smooth exit' yaani wanaoondoka au anayeondoka aondoke kwa amani. Kwa sasa hakuna 'mechanism' (mfumo) yoyote ile, hakuna utaratibu, hakuna sheria, Katiba iko kimya. Tunataka 'smooth exit', 'smooth entry' (Kutoka kwa amani, kuongia kwa amani)."

  "Watumishi wa umma wawe na uhakika wa kuwepo kwa Serikali, bila hivyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko kwa sababu tu watawala waliokuwepo hawataki kuondoka."

  Mwenyekiti huyo yuko kwenye ziara ya kuwanadi wagombea udiwani wa chama hicho katika kata mbalimbali za Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Njombe na Iringa, katika uchaguzi mdogo unaohusisha kata 29 nchini ambao umepangwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,628
  Trophy Points: 280
  na hii sheria inahitajika haraka sana kwa sababu 2015 ccm inatoka madarakani so twahofia wanaweza choma nyaraka muhimu za epa, madini na majengo ya serikali. mia
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mmmmm, kazi ipo.
   
 4. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .... Kweli nimeamini viongozi wa CHADEMA huwa hawakurupuki na huja na hoja mbadala kuonyesha umakini wao na uzalendo wao kwa Taifa letu.
  Kwa hali jinsi ilivyo hawa CCM wanaweza wakapuuzia, ila wapewe masharti kama baadhi ya nyaraka hazitaonekana wajiandae kufikishwa MAHAKAMANI.
   
 5. baba juniho

  baba juniho Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nimeipenda hii, ss hawa ndo viongozi tunaowataka wenye mawazo ambayo hata baba wa Taifa akiwa kama mwanafilosofia hakuweza kuwaza hili labda hakupata nafasi ila kwa hali ilivyo ss haya ayasemayo Mbowe ni ya msingi sana maana hata ikitokea CCM ikashindwa inaweza ikang'ang'ania madarakani asee Big up
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Serikali au umma?
   
 7. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  goood advice
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umma unaweza kuuandaa upinzani kuingia ikulu, halafu serikali wakawa hawako tayari kuruhusu upinzani.
  Kumbuka maneno ya Makamba kuwa watanzania hata wakiichagua chadema kuongoza nchi, mshindi atatangazwa wa ccm!
   
 9. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  100% the Guy is very right. Kuna dalili zote kuwa uchaguzi mkuu 2015 chama kilchoko madarakani kitafail na hivyo kuweza kutumia mwanya kumanipulate mambo yote ya kimsingi ikiwa ni pamoja na Documents zote za Kesi za EPA na Zingine Zinazosubiriwa na Wanzania baada ya utawala mpya 2015 na kuzifikisha mahakani. Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia kwa hiyop OJA ya Mweshimiwa MBOWE na tungeomba wazo hili lichukuliwe kwa uzito wa aina yake bila kuzingatia limetoka upande gani ktk siasa hizi za vyama vingi.
  Ikumbukwe siku za mwisho mwisho wa utawala wa mweshimiwa MKAPA ndio watanzania tulilizwa na wajanja wachache na mpaka leo hii maumivu yale tunayasikilizia na familia zetu wakati fedha zimefichwa Uswiss na kwingineko duniani.
   
 10. l

  lukme Senior Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa ccm wezi ni lazima wajiandae kuondoka. we are tired
   
 11. josam

  josam JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  This is a very very very valid thinking! Let us all take this as a serious issue which needs to be actioned at asap! On this matter, we should put aside political interest and aim for the nation benefits.

  I suggest to be tabled at next parliament session.

  Excellent!!, the next will be welldone job for member of parliament.
   
 12. b

  blueray JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  cha msingi kuwe na utaratibu mzuri wa makabidhiano ya serikali iliyopo na inayoingia, lakini nyaraka za siri! hizi sidhani kama utaweza kuzipata kwa sababu hata tunapojadili hlli leo sidhani kama bado zipo. hata wao kwa wao Hakuna anayemwamini mwenzake, kila mtu anatembea na nyaraka zake!
   
 13. m

  mnovatus JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Very true! Hao majamaa wa WAOEM wanaweza wakaleta mizengwe wakishindwa uchaguz!
   
 14. w

  wamwala Senior Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndio maana nasema kila siku kuwa CDM ni kila kitu kwa mustakabali wa nchi ya Tz. big up Mbowe kwa mawazo mazuri saaanaaaaaaaaaaaaa
   
 15. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hakuna kazi hapo,2015 ni mabadiliko tu
   
 16. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hii ni muhimu sana, wakati wa upigaji kura nchi ikabidhiwe kwa Jaji Mkuu an jopo lake.
   
Loading...