Chadema: Serikali haijawa wazi kuhusu tuhuma za silaha haramu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Serikali haijawa wazi kuhusu tuhuma za silaha haramu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by John Mnyika, Dec 20, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Released Exclusively through JF, for immediate quotation-


  TAMKO KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

  TAARIFA YA KURUGENZI YA MAMBO YA NJE YA CHADEMA KWA SERIKALI NA WATANZANIA KUHUSU RIPOTI YA KUNDI LA WATAALAMU WA UMOJA WA MATAIFA YATOLEWA

  • CHADEMA tunahimiza watanzania kuipitia ripoti ya UN ambayo imetafsiriwa na kuchambuliwa katika lugha ya kiswahili.
  • “Tuchafuke tusafishe tujisafishe: kujadili ni uzalendo wa kutetea maslahi ya taifa”-Mkurugenzi wa Mambo ya Nje (CHADEMA), John Mnyika
  • Waziri Mwinyi atoe tamko la kujibu Tuhuma toka ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN zizazohusu Ulinzi na Jeshi:


  Taarifa inatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuhamasisha umma kupitia taarifa ya awali iliyotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili kuhusu Ripoti ya UN inayopatikana kupitia www.chadema.or.tz ili kuendeleza mjadala wa umma kuhusu ripoti husika.

  Aidha kupitia Kurugenzi ya Mambo ya Nje inatoa mwito kwa Serikali kuweza kutoa tamko kuhusu hatua zilizofikiwa za maandalizi ya taarifa ya Serikali kuhusu ripoti ya UN. Hii ni kwa sababu siku chache zimebakia kwa serikali kuwasilisha ripoti yake kwa Umoja wa Mataifa huku mpaka sasa serikali haijawasiliana na wananchi ama walau wawakilishi wa wananchi kupata maoni yao ili kujenga msimamo wa pamoja kama taifa kuhusu yaliyoibuliwa na ripoti husika.

  Tunatoa mwito pia kwa Umoja wa Mataifa (UN) nao ukayatafakari masuala yaliyomo kwenye taarifa yetu ya awali wakati inapojiandaa kuipitia Taarifa ya Serikali ya Tanzania kuhusu Ripoti husika ambayo serikali kupitia kwa Balozi wake wa Kudumu kwenye Umoja wa Mataifa (Dr Mahiga) imetangaza kwamba itawasilisha mwezi huu wa Disemba mwaka 2009. Watanzania na Umoja wa Mataifa(UN) wazingatie kuwa maoni hayo ya Serikali inayoongozwa na CCM si msimamo wa Watanzania wote kwa kuwa si wananchi, wala vyama vyao, wala wawakilishi wao(kwa maana ya wabunge wa kambi zote) wamehusishwa katika kuandaa ripoti husika. Hivyo, Watanzania na hata Umoja wa Mataifa, unapaswa kuzingatia kuwa mjadala kuhusu ripoti hii unapaswa kuendelea ili Taifa la Tanzania lipate msimamo wa pamoja kuhusiana na ripoti husika; ili wawakilishi wetu kwenye UN wakazungumze matakwa ya watanzania badala la maoni yao binafsi ama ya serikali inayoongozwa na chama kimoja ndani ya mfumo wa vyama vingi. Ni muhimu nikarudia pia kutoa rai niliyoitoa awali kwamba ripoti ya Kikundi cha wataalamu kilichoundwa na UN ipaswa pia kujadiliwa muktadha wa Orodha ya Mafisadi (list of shame) iliyotolewa na CHADEMA.

  Aidha ikumbukwe kuwa tunakubaliana na hoja kwamba Serikali ya Tanzania imechafuliwa katika Ripoti hiyo ya UN kwa baadhi ya viongozi wake, ama raia wake kutajwa kwa namna moja au nyingine katika ripoti hiyo; aidha serikali yenyewe kama taasisi imechafuliwa kwa kuonyeshwa kwamba haitekelezi kikamilifu maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo serikali yetu ni mwanachama. Lakini nchi ya Tanzania kama taifa, na watu wake wote kwa ujumla wake; hawajachafuliwa. Kama Nchi ya Tanzania, na wananchi wake wote wakatoa kauli ya pamoja ya kuwatetea watu wachache ndani na nje ya serikali waliotajwa katika kashfa hii; hapo ndipo tutakapochafuka wote kwa ujumla wake. Lakini kama Nchi yetu, na watu wake; tukakubaliana kuchukua hatua ya kusafisha uchafu unaoichafua sisi na taifa letu; ni wazi tutasafishika na heshima ya taifa letu itaendelea kulindwa na kujilinda kote duniani.

  Kwa kutumia lugha ya picha; ni kama vile nchi yetu ni mtaro; sasa mtaro unaweza kuwa na uchafu, ukipiga kelele kwamba hakuna uchafu wakati uchafu unaonekana basi utaonekana una utamaduni wa uchafu ndio maana unaona ni jambo la kawaida kuwa kwenye mazingira ya uchafu; wewe ni mchafu. Lakini ukichukua hatua ya kuingia ndani ya mtaro, na zana zako za kusafishia; utachafuka kidogo, utaweza kusafisha mtaro, utatoka na utajisafisha. Mtaro utabaki safi, na wewe utabaki safi; na wewe na mtaro wako wote mtakuwa safi na kuitwa wasafi.

  Kadhilika kwa Tanzania, mjadala huu kuhusu uchafu iliotolewa na ripoti ya UN unapaswa kuendelea ili tuujue vizuri uchafu wenyewe wakati wa mjadala huu tutaonekana kuwa tuna uchafu lakini tutaweza kuingia tukachafuka kidogo tukausafisha na nchi yetu itabaki ikiwa safi na sisi wenyewe tutathibitika mbele ya jamii ya kimataifa kuwa ni wasafi na hatupendi uchafu na unapojitokeza tunachukua hatua za kuuondoa.
  Hivyo, tunatoa taarifa hii kwa tahadhari kubwa ya kizalendo kwa kuwa najua suala hili linagusa kwa namna au nyingine vyombo vyeti na masuala tete yanayoelekezwa kwa nchi yetu yanayogusa jeshi, polisi, usalama wa taifa, chama tawala, serikali yake, na viongozi wake. Mambo tunayoyaandika yanagusa genge la mafisadi na watumiaji vibaya wa madaraka; wengine wakiwa ni wafanyabiashara, wengine wakiwa ni viongozi, wengine wakiwa ni wahalifu waliokubuhu na waasi wenye kufanya mauaji.

  Katika mukatadha huo, ni muhimu kwa wananchi kuendelea kupuuza kauli za wenye kueneza uchochezi kwamba CHADEMA iache siasa zenye kuichafua Tanzania; eti itangulize ‘uzalendo’. Wananchi wajiulize ni nani anaichafua Tanzania; kati ya waliofanya ufisadi na/ama kutumia madaraka vibaya na kuitumbukiza Tanzania katika kashfa kama hizi za usafirishaji wa silaha na utoroshaji wa madini kutoka maeneo yenye vita vya wenyewe kwa wenyewe au mtu anayetaka mjadala kuhusu suala hili ili utoke msimamo wa pamoja wa wazalendo wote wenye kukerwa na mambo hayo ili kulirudisha taifa kwenye mkondo unaostahili wenye kulinda heshima ya Tanzania kitaifa na kimataifa?

  Hawa wangetaka kutanguliza maslahi ya pamoja ya Tanzania wasingekurupuka kutoa kauli ya serikali ya CCM bila kushirikisha umma wa watanzania ama wawakilishi wa wananchi. Viongozi wa serikali hawana haki ya kusema kwa niaba ya watanzania katika masuala tata bila kupata maoni yetu au ya kambi yetu bungeni. Wananchi tuwaambie wazi watu kama hao kwamba; kila wanachokisema ni msimamo wao na serikali ya chama chao au taasisi zao; hakiwakilishi msimamo wa watanzania wote.

  Waambie wazi kuwa kama wanataka watanzania tusivuane nguo hadharani; walio kwenye mamlaka ; kabla ya kutoa kauli, walau waombe maoni ya wawakilishi wa wananchi au taasisi zinazowakilisha wananchi; diplomasia iliyokomaa inatambua umuhimu wa maridhiano baina ya viongozi kabla ya kutoka hadharani katika masuala tete ya kitaifa. Tuko tayari kwa majadiliano kama watanzania kuhusu suala hili ili tutoke na msimamo wa pamoja kama taifa. Kuhoji uzalendo wa wanaotaka watanzania waliotajwa kwenye ripoti ya Kikundi cha Wataalamu kilichoundwa na UN ni sawa na kuwatetea mafisadi ama waliotumia vibaya madaraka yao waliotuhumiwa kwenye ripoti husika.

  Ikumbukwe kuwa tuhuma za Tanzania kujihusisha na vita vya DRC zilianza toka wakati taifa hili linaasisiwa. Tofauti ya watawala wa sasa ni kwamba uongozi wa Nyerere ulikuwa unasema wazi kuwa unasaidia waasi, na UN inajua. Lakini wakati ule walioitwa waasi ni wazalendo waliokuwa wakipambana dhidi ya watawala wa kidikteta ambao walikuwa ni makuwadi wa ubeberu na ukoloni mamboeleo katika Afrika. Sera ya wakati huo ya mambo ya nje ya Tanzania ilikuwa ni kuleta ukombozi Afrika nzima (hata ikiwa ni kwa kuunga mkono vita vya msituni) na kueneza umajumuhi wa kiafrika (Pan Africanism).

  Serikali ya sasa ipo tofauti; kwanza haina msimamo endelevu; pili, sera yake ya mambo ya nje haieleweki; tatu, masuala ya sasa ya usafirishaji wa silaha ama utoroshaji wa madini toka maeneo yenye vita ambao yanasemwa kuwa yanafanywa na serikali ama watanzania yanahusu zaidi miradi binafsi ya watu ambayo wanaindesha kwa ama kuzitumia taasisi za kiserikali au kuruhusu mianya kwa kutowajibika kusimamia utawala wa sheria ikiwemo kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo nchi yetu imetia saini.

  Hivyo wapenda demokrasia na maendeleo ndani na nje ya Tanzania wanapaswa kuunga mkono rai tuliyoitoa Disemba Mosi, 2009: Kwamba wazalendo wote, waliokerwa na Tanzania ‘kuchafuliwa’ na ripoti hiyo ya Kikundi cha Wataalamu wa UN, wanapaswa kuwashinikiza watanzania wote wanaoishi Dar es salaam, Kigoma na kote duniani ambao wametajwa kwenye taarifa hiyo kwa majina yao; wajitokeze kutoa kauli za kusafisha majina yao, tukiridhika na hoja zao, katika utetezi wao; basi na sisi tutajiunga katika kundi la kuwatetea na kuwasafisha. Viongozi na taasisi za serikali zilizotajwa kwa namna moja au nyingine katika taarifa hiyo iwe kwa majina au kwa matukio zijitokeze kuelezea kutajwa kwao; tukiridhika na maelezo yao na vielezo vyao, tutajiunga katika kazi ya kizalendo ya kuwatetea na kuwasafisha. Na hii isiwe kwa taarifa ya UN pekee; iwe pia Orodha ya Mafisadi, katika vipengele vinavyohusiana na Kampuni za Meremeta, Tangold, Deep Green nk.

  Kosa kubwa la Wizara ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa katika sakata hili ni kufikiri kwamba yenyewe tu ndiyo inayowajibika kulitolea ufafanuzi na taarifa kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na Kundi la wataalamu lililoundwa na UN. Narudia tena kumuomba Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwashinikiza Mawaziri wengine ambao sekta zao zimeguswa kutoa kauli za kujibu ama kufafanua hoja zilizoibuliwa ndani ya ripoti hiyo, ambayo tayari Wizara ya Mambo ya Nje ameshafanya kosa la kisiasa la kuitumbukiza serikali kwenye malumbano mapema kwa kuliibua suala hili na kuituhumu UN kabla hata Tanzania kufafanua ama kujieleza kwenye Kamati ya Vikwazo. Kwa kuanzia ni muhimu kwa Wizara ya Mambo ya Usalama wa Raia na ile ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa zikatoa maelezo na vielelezo kuhusu suala hili. Hivyo, mawaziri wanaopaswa kufutia kutoa kauli ni: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Hussein Mwinyi na Waziri wa Usalama wa Raia; Lawrence Masha.


  Ikumbukwe kuwa Wizara ya Ulinzi ilishatoa kauli fupi ya kukanusha tu kwa ujumla bila kujibu hoja kwa hoja. Hatahivyo, pamoja na kuwa natambua kwamba ni muhimu kwa Jeshi letu, kutunza siri za mikakati yetu ya kijeshi. Wizara ya Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa ina wajibu wa kutoa kauli za ufafanuzi; na awasilishe maelezo na vielelezo ili serikali ipeleke UN yenye kujibu maswali yafuatayo: Je, kwa kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania Burundi ambaye alikuwa ni mmoja wa majenerali wa jeshi, namba yake ya simu imetajwa kutumika kuwasiliana na waasi; JWTZ haina sera ya kuendelea kuwatumia maafisa wake waandamizi wa jeshi wanaoitwa wastaafu, wanaotumwa kwenye nchi zenye vita kama ilivyo DRC kuweza kufanya kwa barokoa ya ubalozi majukumu yanayoyofanana na uambata wa kijeshi? (Millitary attacheship). Kama hivyo ndivyo, wizara inaweza kutuambia ni mawasiliano gani ya kijeshi yalikuwa yakifanyika baina ya namba ya simu ya balozi wetu na makamanda wa vikundi vya waasi DRC hususani FDLR na maswahiba wao ndani FARDC? Kwa kuwa mabalozi wetu kuwasiliana na vikundi vya waasi katika nchi ambazo serikali yetu inatambua serikali zake za kiraia ni jambo lisilokubalika na halina uhusiano wowote na ‘siri kuu za jeshi’ wala ‘maslahi ya taifa’; kwanini nini serikali isituleze mawasiliano yaliyokuwa yakiendelea kama inavyotuhimiwa kwenye ripoti ya kundi la Wataalamu lililoundwa na UN? ( Ni muhimu kwa Waziri Mwinyi kutoa tamko hivi sasa kwa kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania Burundi ameshaondoka katika Ubalozi husika na hana tena kinga kamili ya Kibalozi. Je uamuzi wa Rais Kikwete kuteua Balozi Mpya wa Tanzania Burundi hivi karibuni unauhusiano wowote na kutajwa kwa jina la balozi wa Zamani katika ripoti ya UN?).

  Kwa kuwa silaha za kivita ni kubwa, sio ndogo kama sindano kiasi kwamba zinaweza kupita bila kuonekana; Wizara ya ulinzi inazielezeaje tuhuma ya silaha kupitishwa Tanzania ambazo zimeelezwa na Kundi la Wataalamu wa UN kwa maelezo na vielelezo? Wizara inaweza kulieleza taifa silaha hizo zimekwenda nchi gani na kwa makubaliano gani ya kijeshi? Mwisho, kwa kuwa Kamati ya Vikwazo ya UN kuhusu DRC iliundwa toka mwaka 2004; pamoja na kuwa ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN imegusia zaidi miaka ya 2007 mpaka 2009; Wizara inazizungumziaje taarifa zilizozagaa katika mitandao mbalimbali zinazohusisha Meremeta, Tangold; Deep Green na makampuni mengine yaliyosajiliwa kwa majina ya vigogo wa serikali ya awamu ya tatu ambayo yanatajwa kuhusika na biashara haramu za silaha na utoroshaji wa madini toka maeneo yenye vita; kampuni ambazo mojawapo serikali imesema kwamba inahusika na JWTZ? Izingatiwe kuwa CHADEMA ilishaweka msingi wa taarifa hizo kwenye orodha ya mafisadi iliyotolewa 15 Septemba 2009.


  Masuala haya na mengine mengi zaidi nikayoyachambua kadiri siku zinavyokwenda yanapaswa kujadiliwa na wananchi ama wawakilishi wao; ili tuweze kutoka na msimamo wa pamoja. Pia UN na Kundi la Wataalamu wake kuiuliza serikali itoe maelezo ya kina wakati wa mapitio ya taarifa husika. Ni utaratibu wa kawaida kwamba ufuatiliaji kama huu uliofanywa kwa kuwa ulihusu Tanzania; serikali itapewa fursa kuandika ripoti ya nchi (country report) kufafanua mambo ambayo yametajwa kabla ya kamati ya vikwazo kufanya maamuzi yake ama kuikubali ripoti husika na mapendekezo yake ama kutoa maelekezo mbadala ya kutaka uchunguzi zaidi katika maeneo ambayo Kundi la Wataalamu limeeleza katika ripoti yake kuwa uchunguzi wake bado haujamilika. Inashangaza kwamba serikali inatumia nguvu kubwa, kubeza ripoti hii na kutishia wanahabari wasiendelee kuandika wakati ripoti imeweka bayana kwamba uchunguzi bado haujakamilika; serikali itaweka wapi uso wake kama uchunguzi zaidi ukaibua uchafu zaidi?“Tuchafuke tusafishe tujisafishe: kujadili ni uzalendo wa kutetea maslahi ya taifa”


  Imetolewa leo tarehe 20 Disemba, 2009 Mkoani Tanga; Tanzania:
  John Mnyika
  Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa
  0754694553

  Taarifa ya Awali kuhusu Ripoti ya UN inapatikana kwa kubonyeza hapa: http://www.chadema.or.tz/tamko/tamko.php?id=30   
 2. Companero

  Companero Platinum Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  This is indeed a shadow Ministry of Foreign Affairs!
   
 3. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  TAARIFA AWALI YA KURUGENZI YA MAMBO YA NJE YA CHADEMA
  KWA
  SERIKALI NA WATANZANIA
  KUHUSU
  RIPOTI YA KUNDI LA WATAALAMU WA UMOJA WA MATAIFA

  UTANGULIZI:

  “Tuchafuke tusafishe tujisafishe: kujadili ni uzalendo wa kutetea maslahi ya taifa”, hii ni kauli yetu rasmi leo Disemba 7 mwaka 2009. Itakumbukwa kuwa Disemba Mosi, 2009 nilifanya mkutano na wanahabari na kuitoa hadharani ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN kuhusu yanayojiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) katika maeneo ya vita. Ripoti hiyo inatathmini utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa(UN) kuhusu suala hilo na inatuhumu nchi, taasisi na watu mbalimbali kuhusika kwa namna moja au nyingine katika utoroshaji wa madini na usafirishaji wa silaha haramu kwenda maeneo hayo mambo ambayo yanachangia mauaji, ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria ya kimataifa kwa ujumla. Katika mkutano huo na waandishi wa habari nilieleza kwamba umma wa watanzania unapaswa kujadili ripoti husika ili kuweza kutoka na msimamo wa pamoja kama taifa kuhusu maudhui ya ripoti hiyo yanayoitaja nchi yetu, taasisi zetu ama baadhi ya watanzania. Katika mkutano huo na wanahabari tuliahidi kuyatoa maudhui ya ripoti hiyo hatua kwa hatua, katika lugha ya Kiswahili pamoja na kuibua maeneo ya kutafakariwa kama sehemu ya kuchangia kuwezesha mjadala wa umma kuhusu ripoti husika.

  Leo tarehe 7 Disemba 2009 kupitia taarifa hii rasmi ya awali toka kurugenzi ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa ya CHADEMA, napenda kuwasilisha kwa umma tafsiri ya kwanza na uchambuzi wa awali wa maudhui ya ripoti hiyo ya Kundi la Wataalamu wa UN kwa ajili ya kusambazwa, kusomwa na kutafakariwa na serikali na watanzania kwa ujumla. Aidha ni muhimu Umoja wa Mataifa (UN) nao ukayatafakari masuala haya wakati inayapitia Moani ya Serikali ya Tanzania kuhusu Ripoti husika ambayo serikali kupitia kwa Balozi wake wa Kudumu kwenye Umoja wa Mataifa (Dr Mahiga) imetangaza kuwa itayawasilisha leo tarehe 7 Disemba 2009. Watanzania na Umoja wa Mataifa(UN) wazingatie kuwa maoni hayo ya Serikali inayoongozwa na CCM si msimamo wa Watanzania wote kwa kuwa si wananchi, wala vyama vyao, wala wawakilishi wao(kwa maana ya wabunge wa kambi zote) wamehusishwa katika kuandaa ripoti husika. Hivyo, Watanzania na hata Umoja wa Mataifa, unapaswa kuzingatia kuwa mjadala kuhusu ripoti hii unapaswa kuendelea ili Taifa la Tanzania lipate msimamo wa pamoja kuhusiana na ripoti husika; ili wawakilishi wetu kwenye UN wakazungumze matakwa ya watanzania badala la maoni yao binafsi ama ya serikali inayoongozwa na chama kimoja ndani ya mfumo wa vyama vingi. Ni muhimu nikarudia pia kutoa rai niliyoitoa awali kwamba ripoti ya Kikundi cha wataalamu kilichoundwa na UN ipaswa pia kujadiliwa muktadha wa Orodha ya Mafisadi (list of shame) iliyotolewa na CHADEMA.

  Izingatiwe kuwa Ripoti kikundi cha wataalamu wa UN inaitaja Tanzania ama baadhi ya watanzania kuhusika kwa namna moja au nyingine kuwezesha biashara haramu ya silaha kwenda maeneo ya vita DRC na ujangili wa madini toka maeneo hayo; madini ambayo yametapakaa damu ya mauji wa raia wasio na hatia katika maeneo yenye vita vya wenyewe kwa wenyewe (Blood Minerals). Matukio ndani ya ripoti hii yametokea hivi karibuni, katika kipindi cha utawala wa Rais wa awamu ya nne, kupitia serikali ya chama cha Mapinduzi; Jakaya Mrisho Kikwete hususani kati ya mwaka 2006 mpaka 2009.

  Wakati wa upande mwingine, Orodha ya Mafisadi inataja ushiriki wa serikali na viongozi wake katika makampuni tata kama Meremeta, Tangold, Deep Green Finnance na mengineyo ambayo yamekuwa yakihusishwa na biashara ya utoroshaji wa dhahabu toka maeneo yenye vita. Ukitazama filamu ya Darwins Nighmare, unaweza kupata picha ya uhusiano baina ya biashara hii na nyinginezo na biashara haramu ya silaha. Taarifa zote mbili: ya Kundi ya Wataalamu wa UN na Orodha ya Mafisadi, tumeziweka kwenye mtandao wa www.chadema.or.tz ili watanzania bila kujali itikadi wazijadili taarifa hizi kwa mustabali mwema wa Taifa letu.

  Mkutano wangu na wanahabari, nikiwa ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa CHADEMA kumjibu Waziri wa Serikali ya CCM anayeongoza wizara ya sekta yangu, na uamuzi wa kutangaza kwamba suala hili lijadiliwe na umma wa watanzania na wawililishi wa wananchi; ni muhimu tuendelee na mjadala; ili tutoke na msimamo wa pamoja kama watanzania badala ya msimamo wa serikali ya CCM ambao unajaribu kufunika kombe mwanaharamu apite bila kujali kwamba mficha maradhi kifo kitamuumbua.

  Nakubaliana na hoja kwamba Serikali ya Tanzania imechafuliwa katika Ripoti hiyo ya UN kwa baadhi ya viongozi wake, ama raia wake kutajwa kwa namna moja au nyingine katika ripoti hiyo; aidha serikali yenyewe kama taasisi imechafuliwa kwa kuonyeshwa kwamba haitekelezi kikamilifu maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo serikali yetu ni mwanachama. Lakini nchi ya Tanzania kama taifa, na watu wake wote kwa ujumla wake; hawajachafuliwa. Kama Nchi ya Tanzania, na wananchi wake wote wakatoa kauli ya pamoja ya kuwatetea watu wachache ndani na nje ya serikali waliotajwa katika kashfa hii; hapo ndipo tutakapochafuka wote kwa ujumla wake. Lakini kama Nchi yetu, na watu wake; tukakubaliana kuchukua hatua ya kusafisha uchafu unaoichafua sisi na taifa letu; ni wazi tutasafishika na heshima ya taifa letu itaendelea kulindwa na kujilinda kote duniani.

  Kwa kutumia lugha ya picha; ni kama vile nchi yetu ni mtaro; sasa mtaro unaweza kuwa na uchafu, ukipiga kelele kwamba hakuna uchafu wakati uchafu unaonekana basi utaonekana una utamaduni wa uchafu ndio maana unaona ni jambo la kawaida kuwa kwenye mazingira ya uchafu; wewe ni mchafu. Lakini ukichukua hatua ya kuingia ndani ya mtaro, na zana zako za kusafishia; utachafuka kidogo, utaweza kusafisha mtaro, utatoka na utajisafisha. Mtaro utabaki safi, na wewe utabaki safi; na wewe na mtaro wako wote mtakuwa safi na kuitwa wasafi.

  Kadhilika kwa Tanzania, mjadala huu kuhusu uchafu iliotolewa na ripoti ya UN unapaswa kuendelea ili tuujue vizuri uchafu wenyewe wakati wa mjadala huu tutaonekana kuwa tuna uchafu lakini tutaweza kuingia tukachafuka kidogo tukausafisha na nchi yetu itabaki ikiwa safi na sisi wenyewe tutathibitika mbele ya jamii ya kimataifa kuwa ni wasafi na hatupendi uchafu na unapojitokeza tunachukua hatua za kuuondoa.
  Hivyo, naandika waraka huu kwa tahadhari kubwa ya kizalendo kwa kuwa najua suala hili linagusa kwa namna au nyingine vyombo vyeti na masuala tete yanayoelekezwa kwa nchi yetu yanayogusa jeshi, polisi, usalama wa taifa, chama tawala, serikali yake, na viongozi wake. Mambo ninayoandika pia yanagusa genge la mafisadi na watumiaji vibaya wa madaraka; wengine wakiwa ni wafanyabiashara, wengine wakiwa ni viongozi, wengine wakiwa ni wahalifu waliokubuhu na waasi wenye kufanya mauaji.

  Katika mukatadha huo, ni muhimu kwa wananchi kupuuza kauli za wenye kueneza uchochezi kwamba CHADEMA iache siasa zenye kuichafua Tanzania; eti itangulize ‘uzalendo’. Wananchi wajiulize ni nani anaichafua Tanzania; kati ya waliofanya ufisadi na/ama kutumia madaraka vibaya na kuitumbukiza Tanzania katika kashfa kama hizi za usafirishaji wa silaha na utoroshaji wa madini kutoka maeneo yenye vita vya wenyewe kwa wenyewe au mtu anayetaka mjadala kuhusu suala hili ili utoke msimamo wa pamoja wa wazalendo wote wenye kukerwa na mambo hayo ili kulirudisha taifa kwenye mkondo unaostahili wenye kulinda heshima ya Tanzania kitaifa na kimataifa?

  Hawa wangetaka kutanguliza maslahi ya pamoja ya Tanzania wasingekurupuka kutoa kauli ya serikali ya CCM bila kushirikisha umma wa watanzania ama wawakilishi wa wananchi. Viongozi wa serikali hawana haki ya kusema kwa niaba ya watanzania katika masuala tata bila kupata maoni yetu au ya kambi yetu bungeni. Wananchi tuwaambie wazi watu kama hao kwamba; kila wanachokisema ni msimamo wao na serikali ya chama chao au taasisi zao; hakiwakilishi msimamo wa watanzania wote.

  Waambie wazi kuwa kama wanataka watanzania tusivuane nguo hadharani; walio kwenye mamlaka ; kabla ya kutoa kauli, walau waombe maoni ya wawakilishi wa wananchi au taasisi zinazowakilisha wananchi; diplomasia iliyokomaa inatambua umuhimu wa maridhiano baina ya viongozi kabla ya kutoka hadharani katika masuala tete ya kitaifa. Tuko tayari kwa majadiliano kama watanzania kuhusu suala hili ili tutoke na msimamo wa pamoja kama taifa. Kuhoji uzalendo wa wanaotaka watanzania waliotajwa kwenye ripoti ya Kikundi cha Wataalamu kilichoundwa na UN ni sawa na kuwatetea mafisadi ama waliotumia vibaya madaraka yao waliotuhumiwa kwenye ripoti husika.

  Ikumbukwe kuwa tuhuma za Tanzania kujihusisha na vita vya DRC zilianza toka wakati taifa hili linaasisiwa. Tofauti ya watawala wa sasa ni kwamba uongozi wa Nyerere ulikuwa unasema wazi kuwa unasaidia waasi, na UN inajua. Lakini wakati ule walioitwa waasi ni wazalendo waliokuwa wakipambana dhidi ya watawala wa kidikteta ambao walikuwa ni makuwadi wa ubeberu na ukoloni mamboeleo katika Afrika. Sera ya wakati huo ya mambo ya nje ya Tanzania ilikuwa ni kuleta ukombozi Afrika nzima (hata ikiwa ni kwa kuunga mkono vita vya msituni) na kueneza umajumuhi wa kiafrika (Pan Africanism).

  Serikali ya sasa ipo tofauti; kwanza haina msimamo endelevu; pili, sera yake ya mambo ya nje haieleweki; tatu, masuala ya sasa ya usafirishaji wa silaha ama utoroshaji wa madini toka maeneo yenye vita ambao yanasemwa kuwa yanafanywa na serikali ama watanzania yanahusu zaidi miradi binafsi ya watu ambayo wanaindesha kwa ama kuzitumia taasisi za kiserikali au kuruhusu mianya kwa kutowajibika kusimamia utawala wa sheria ikiwemo kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo nchi yetu imetia saini.

  Hivyo wapenda demokrasia na maendeleo ndani na nje ya Tanzania wanapaswa kuunga mkono rai tuliyoitoa Disemba Mosi, 2009: Kwamba wazalendo wote, waliokerwa na Tanzania ‘kuchafuliwa’ na ripoti hiyo ya Kikundi cha Wataalamu wa UN, wanapaswa kuwashinikiza watanzania wote wanaoishi Dar es salaam, Kigoma na kote duniani ambao wametajwa kwenye taarifa hiyo kwa majina yao; wajitokeze kutoa kauli za kusafisha majina yao, tukiridhika na hoja zao, katika utetezi wao; basi na sisi tutajiunga katika kundi la kuwatetea na kuwasafisha. Viongozi na taasisi za serikali zilizotajwa kwa namna moja au nyingine katika taarifa hiyo iwe kwa majina au kwa matukio zijitokeze kuelezea kutajwa kwao; tukiridhika na maelezo yao na vielezo vyao, tutajiunga katika kazi ya kizalendo ya kuwatetea na kuwasafisha. Na hii isiwe kwa taarifa ya UN pekee; iwe pia Orodha ya Mafisadi, katika vipengele vinavyohusiana na Kampuni za Meremeta, Tangold, Deep Green nk.

  Kosa kubwa la Wizara ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa katika sakata hili ni kufikiri kwamba yenyewe tu ndiyo inayowajibika kulitolea ufafanuzi na taarifa kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na Kundi la wataalamu lililoundwa na UN. Wakati umefika sasa wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwashinikiza Mawaziri wengine ambao sekta zao zimeguswa kutoa kauli za kujibu ama kufafanua hoja zilizoibuliwa ndani ya ripoti hiyo, ambayo tayari Wizara ya Mambo ya Nje ameshafanya kosa la kisiasa la kuitumbukiza serikali kwenye malumbano mapema kwa kuliibua suala hili na kuituhumu UN kabla hata Tanzania kufafanua ama kujieleza kwenye Kamati ya Vikwazo. Kwa kuanzia ni muhimu kwa Wizara ya Mambo ya Usalama wa Raia na ile ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa zikatoa maelezo na vielelezo kuhusu suala hili. Hivyo, mawaziri wanaopaswa kufutia kutoa kauli ni: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Hussein Mwinyi na Waziri wa Usalama wa Raia; Lawrence Masha.

  Tuhuma toka ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN zizazohusu Ulinzi na Jeshi:

  Ikumbukwe kuwa Wizara ya Ulinzi ilishatoa kauli fupi ya kukanusha tu kwa ujumla bila kujibu hoja kwa hoja. Hatahivyo, pamoja na kuwa natambua kwamba ni muhimu kwa Jeshi letu, kutunza siri za mikakati yetu ya kijeshi. Wizara ya Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa ina wajibu wa kutoa kauli za ufafanuzi; na awasilishe maelezo na vielelezo ili serikali ipeleke UN yenye kujibu maswali yafuatayo: Je, kwa kuwa Balozi wa Tanzania Burundi ambaye alikuwa ni mmoja wa majenerali wa jeshi, namba yake ya simu imetajwa kutumika kuwasiliana na waasi; JWTZ haina sera ya kuendelea kuwatumia maafisa wake waandamizi wa jeshi wanaoitwa wastaafu, wanaotumwa kwenye nchi zenye vita kama ilivyo DRC kuweza kufanya kwa barokoa ya ubalozi majukumu yanayoyofanana na uambata wa kijeshi? (Millitary attacheship). Kama hivyo ndivyo, wizara inaweza kutuambia ni mawasiliano gani ya kijeshi yalikuwa yakifanyika baina ya namba ya simu ya balozi wetu na makamanda wa vikundi vya waasi DRC hususani FDLR na maswahiba wao ndani FARDC? Kwa kuwa mabalozi wetu kuwasiliana na vikundi vya waasi katika nchi ambazo serikali yetu inatambua serikali zake za kiraia ni jambo lisilokubalika na halina uhusiano wowote na ‘siri kuu za jeshi’ wala ‘maslahi ya taifa’; kwanini nini serikali isituleze mawasiliano yaliyokuwa yakiendelea kama inavyotuhimiwa kwenye ripoti ya kundi la Wataalamu lililoundwa na UN? Kwa kuwa silaha za kivita ni kubwa, sio ndogo kama sindano kiasi kwamba zinaweza kupita bila kuonekana; Wizara ya ulinzi inazielezeaje tuhuma ya silaha kupitishwa Tanzania ambazo zimeelezwa na Kundi la Wataalamu wa UN kwa maelezo na vielelezo? Wizara inaweza kulieleza taifa silaha hizo zimekwenda nchi gani na kwa makubaliano gani ya kijeshi? Mwisho, kwa kuwa Kamati ya Vikwazo ya UN kuhusu DRC iliundwa toka mwaka 2004; pamoja na kuwa ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN imegusia zaidi miaka ya 2007 mpaka 2009; Wizara inazizungumziaje taarifa zilizozagaa katika mitandao mbalimbali zinazohusisha Meremeta, Tangold; Deep Green na makampuni mengine yaliyosajiliwa kwa majina ya vigogo wa serikali ya awamu ya tatu ambayo yanatajwa kuhusika na biashara haramu za silaha na utoroshaji wa madini toka maeneo yenye vita; kampuni ambazo mojawapo serikali imesema kwamba inahusika na JWTZ? Izingatiwe kuwa CHADEMA ilishaweka msingi wa taarifa hizo kwenye orodha ya mafisadi iliyotolewa 15 Septemba 2009.

  Tuhuma toka ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN zizazohusu Usalama wa Raia:
  Tarehe 2 Disemba 2009 Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa Tanzania haihusiki kwa namna yoyote ile katika kashfa ya kuwapatia silaha waasi wa serikali za mataifa mengine kama ilivyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari. Mratibu wa Udhibiti wa Silaha hapa nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Dominick Hayuma, amesema kuwa taarifa za Kundi la Wataalamu lililoteuliwa na UN hazina ukweli wowote. Amesema kuwa Tanzania ina uhusiano mkubwa na serikali za nchi jirani na ndiyo maana majeshi ya polisi katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika na zile za kusini mwa Afrika (SADC) zinashirikiana katika masuala ya operesheni kwa lengo la kudhibiti kwa pamoja vitendo vya kihalifu. Amesema kuwa kuna baadhi ya mashirika ya ndani na nje ya nchi wanakusanya taarifa za uongo kwa lengo la kujipatia fedha ama kuleta uchochezi baina ya nchi moja na nyingine.
  Nichukue fursa hii kuwatahadharisha wataalamu wetu wa polisi kutokuingizwa kutoa kauli za kisiasa katika mambo yanayostahili maelezo na vielelezo. Ni vizuri zikatolewa kauli za kisera kuhusu masuala hayo; ushahidi wa kuingia ama kutoka kwa silaha za kijeshi katika nchi yetu uko wazi hata kwa wananchi waoishi katika mikoa ya mpakani na nchi za eneo la maziwa makuu. Wananchi ni muhimu wawatake polisi ambao tunawalipa kwa kodi zetu, wakae mbali na mijadala ya kisera na ya kisiasa ili kutenganisha kati ya jeshi na propaganda za wanasiasa. Tabia hii ya kutumwa na viongozi wa CCM ndio ambayo inafanya Polisi wetu kushiriki katika kuiba kura na kuhujumu wapinzani wakati wa uchaguzi. Polisi wetu wajue kwamba mishahara midogo wanayolipwa na maslahi duni wanayoyapata ni matokeo ya uongozi mbovu wa serikali hiyo hiyo ya CCM inayofanya waweke pembeni maadili ya taaluma zao; na kuitetea na hata kuipigania nyakati za uchaguzi. Hivyo, polisi ikae mbali na mapambano ya kisiasa baina ya vyama, ikiwemo mapambano ya hoja kwa ajili ya kupata msimamo wa pamoja wa watanzania. Polisi ibaki na jukumu la kusimamia sheria na kuhakikisha kwamba utawala wa sheria unazingatiwa badala ya kukanusha tu bila maelezo na vielelezo ripoti ya Kundi la wataalamu wa UN ambayo imewataja kwa majina watanzania wanatuhumiwa kuvunja sheria lakini polisi haijawakamata mpaka sasa.

  Ni muhimu kwa Wizara ya Usalama wa Raia hususani kupitia kwa Waziri Lawrence Masha ikitoa tamko ikiwemo kutoa maelekezo kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwachunguza watu wote na taasisi zote za Tanzania zilizotuhumiwa kwenye ripoti hiyo likiwemo jeshi la polisi lenyewe. Wizara ya Usalama wa Raia ijibu maswali na kufafanunua masuala yafuatayo, ikiwemo kwa kutoa maelezo na vielelezo kwa Umoja wa Mataifa kwamba: Je, taarifa ya kwamba polisi waliizunguka meli inayotuhumiwa katika ripoti hiyo ya Kundi la Wataalamu wa UN anaizungumziaje? Je, polisi hao walikuwa wa nchi gani? Kama ni watanzania walikwenda kufanya nini kwa maelekezo ya nani? Aidha ripoti ya Kundi la Wataalamu, inataja kwamba yapo maduka ya masonara yaliyokuwa yananunua madini yaliyotoroshwa kutoka DRC? Na kwamba kwa maelezo ya mmojawapo wa wamiliki wa maduka yaliyotajwa kwenye taarifa hiyo alidai kwamba kuna wakati ambapo idara ya uhamiaji iliwahi kuendesha msako dhidi ya wafanyabiashara hao? Je, serikali inayazungumziaje madai hayo? Je, serikali yake iko tayari kuwachunguza raia wote wa kigeni wanaotajwa kwenye ripoti hiyo wanaoishi mpaka sasa Dar es salam, Kigoma na kwingineko katika nchi yetu? Je, Wizara yake inamzungumziaje raia wa DRC aliyetajwa katika ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN kwa jina la Bande Ndagundi, ambaye anatuhumiwa kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 27 anayejishughulisha na biashara zinazohusiana na masuala ya kijeshi? Je, Waziri Masha au wawakilishi toka Wizara yake wamewahi kuwasiliana na mtu huyo anayedaiwa kuendelea kuishi Dar es salaam? Ni muhimu kwa Wizara hususani Waziri husika kutoa kauli kuhusu mtu huyu kwa kuwa imeelezwa kwa uwazi ikiwemo kwa yeye mwenyewe kusema kwenye barua zake ikiwemo ile ya tarehe 17 July 2009 kuwa ana mawasiliano ya karibu na viongozi wa juu wa serikali, polisi, jeshi na chama tawala.

  Umoja wa Mataifa utoe ufafanuzi kuwezesha mjadala

  Tunatambua kwamba Umoja wa Mataifa (UN) umetoa kauli kwamba ripoti ile ‘sio rasmi’ na kwamba ‘wako tayari kuishirikisha Tanzania katika kuifanyia mapitio ripoti husika’. Na kwamba ripoti hiyo isihusishwe moja kwa moja na Sekretariati ya Umoja wa Mataifa, na Mashirika yake; hatuna tatizo na kauli hizi. Hivyo, watanzania, wanahabari na wachambuzi; wanapaswa kuendelea kuinukuu na kuirejee ripoti hiyo kuwa ni ripoti rasmi kabisa na ya mwisho ya Kundi la Wataalamu iliyoundwa na UN; ripoti hii inaweza kubadilika tu, ikiwa aliyepewa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwazo (Sanctions Committee) atajadiliana na wajumbe wake na kutoa ripoti mbadala. Ama ataipandisha juu zaidi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN Security Council) ambalo ndio chombo chenye mamlaka ya kutoa maazimio kuhusu masuala hayo. Tulitarajia kauli kama hii ya ukomavu wa kidiplomasia toka kwa umoja wa mataifa. Kauli hii ya kisiasa yenye kuendana na nadharia ya ‘ukila na kipofu usimshike mkono’ inasadifu maudhui ya Mkataba wa Kuundwa kwa umoja wa Mataifa (UN Charter), Tamko kuhusu Haki za Binadamu(UDHR)- kama vile UN imeamua kuipa serikali ya Tanzania haki ya kusikilizwa. Kauli hii inaendana pia na Mkataba wa Vienna; ambao Serikali iliutumia kulipotosha Bunge kwa kutoa karipio kali kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa kutokuingilia ‘mambo ya ndani’ ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kauli ambayo iliicha uchi serikali ya Tanzania kuhusu dhamira yake ya kutaka wabaki wenyewe; kwa dhamira ambayo inastahili kuhojiwa.

  UN ikiwemo ofisi ya Umoja wa Mataifa hapa Tanzania chini ya mpango wao wa kufanya kazi kwa pamoja kama familia(One UN Programme) inapaswa kuzitafsiri kwa pamoja kauli hizi za serikali ya CCM. UN inabidi itambue kwamba serikali ya CCM ya leo sio ile ya Mwalimu Nyerere ya ukweli na uadilifu. Hivyo UN, inapotafakari matukio ya sasa irejee na matukio ya nyuma, kwani ni UN hii hii imekuwa ikiisifia kupindukia serikali ya CCM kwa demokrasia; imekuwa ikutuma waangalizi wa uchaguzi(Elections Observers) wake na kutangaza chaguzi kuwa huru na haki. Matokeo yake CCM ya kina Membe, imekuwa ikibaki yenyewe; waangalizi wa UN huja mwishoni, na huja maeneo machache; sehemu kubwa ya nchi CCM inabaki yenyewe ikisimamia uchaguzi wenyewe kupitia Tume isiyo huru ya uchaguzi ambayo Makamishna wake wanateuliwa na serikali hiyo hiyo inayoshiriki uchaguzi. Lakini mbaya zaidi; tume hiyo haina watendaji wake huru katika ngazi za kata na majimbo, inatumia watendaji wa serikali walioteuliwa moja kwa moja na serikali yenyewe kama watendaji wa kata na wakurugenzi wa halmashauri. Tume haizingatii kuwa watendaji hawa wamekuwa wakipewa maelekezo na Mawaziri hao hao wa serikali kabla ya uchaguzi kwamba atayeachia eneo lake liende upinzani atakuwa amepoteza ajira yake aliyoteuliwa. Matokeo yake ni CCM kushinda kwa kishindo na hivyo kuwa na hodhi (monopoly) ya chama kimoja bungeni; na hivyo kupunguza uwezo wa kambi ya upinzani kuiwajibisha serikali kikamilifu. Hivyo, wakati tunatafakari ripoti ya Kikundi cha Wataalamu kilichoundwa UN; ni wasaa pia wa UN Tanzania kupitia UNDP kuongeza kasi ya kuisimamia serikali kutekeleza marekebisho ya kisheria na kitaasisi ya kuwezesha uchaguzi wa 2010 kuwa huru na haki. Hii ni kupitia programu yake ya kusimika demokrasia (deepening democracy program) na kusimamia vizuri mfuko wa uchaguzi wa mwaka 2010 (UN Basket Fund for Elections).

  Kwa upande mwingine kupitia waraka huu, naiomba tena Ofisi ya Umoja wa Mataifa hapa nchini (UN Tanzania) itoe tamko tena kufafanua yafuatayo kwa kuwa kauli ya UN inaweza kutafsiriwa vibaya na Serikali ama wasioitakia mema Tanzania kufunika mjadala kuhusu ripoti ya Kundi la Wataalamu lililoundwa na UN yenyewe kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa maazimio rasmi kabisa ya UN hio hio ambayo Tanzania ni moja ya nchi wanachama.

  UN ijibu maswali na kufafanua masuala yafuatayo: Mosi; Je, Kikundi cha Wataalamu kilichoundwa na UN haikuwasilisha ripoti ya mwisho kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwazo iliyoundwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa azimio namba 1533 la mwaka 2004 ambalo serikali ya Tanzania inalitambua? Pili; kundi kazi hilo halikupewa jukumu na Umoja wa Mataifa kufuatilia kama nchi wanachama zimetimiza aya ya 5 ya azimio namba 1807 la mwaka 2008 la Baraza la Usalama ambalo limezitaka nchi wanachama za UN ikiwemo Tanzania kuitaarifu kabla (inadvance) kuhusu kusafirishwa kwa silaha na mambo yanayohusiana nayo kwa ajili DRC au msaada wa, ushauri au mafunzo yanayohusiana na operesheni za kijeshi? Je, ni kwa kiasi gani Tanzania imetekeleza azimio hilo kwa kulingisha kati ya taarifa za serikali na tafiti huru zinazofanyika ikiwemo hii ya Kundi la Wataalamu lililoundwa na Umoja wa Mataifa wenyewe.

  Je, Umoja wa Mataifa haukulipa Kundi hilo la Wataalamu jukumu la kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika ambao ni kinyume na aya ndogo 4(d)(e) na (f) ya Azimio namba 1857 la mwaka 2008 la Baraza la Usalama? Je, ni kwa kiasi gani Tanzania au watanzania wametajwa kushiriki katika vitendo hivyo kwa kurejea taarifa ambazo Tanzania imekuwa ikizitoa ukilinganisha na ripoti ya Kundi la Wataalamu lililoundwa na UN ambalo limeeleza kwamba kuna vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vimefanyika ambavyo ni kinyume na sheria ya kimataifa ya ubinadamu(International Humanitarian Law).

  UN imesema kwamba iko tayari kuishirisha serikali ili kuisuka upya ripoti husika. Sina tatizo na kauli hii ya UN pia; imetolewa kidiplomasia. Kauli hii haifuti ukweli kuwa ripoti ya mwisho ya Kundi la Wataalamu wa UN imeshatolewa na imeshasambaa; namna ya kuepuka tuhuma zilizotolewa na ripoti ya awali ambayo serikali imeamua kuziita za kizushi zenye nia mbaya ya kuichafua Tanzania. Tafsiri ya kauli hii ya serikali ya Tanzania ni kuwa UN iliunda timu ya wataalamu wa uzushi, wenye nia mbaya ya kuichafua Tanzania: haya ni matusi kwa UN na tuhuma nzito kwa wataalamu hao kwa ubinafsi wao na taasisi wanazoziwakilisha katika kazi hiyo. Haitarajiwi kwamba Kundi la Wataalamu na hata UN yenyewe kwamba wataicha kauli hiyo kupita bila kutolewa kauli. Lazima wote waungane kuweka wazi; tatizo linaweza lisiwe kufilisika kitaalamu kwa UN; kundi lake la wataalamu na taasisi zao; tatizo ni udhaifu wa kimaadili wa serikali inayotawaliwa na CCM ambao wako tayari kuweka pembeni taaluma zao na wataalamu wao. Na kutoa kauli za kihuni ambazo hazistahili kutolewa katika medani ya diplomasia; tena kuhusu UN, chombo kinachounganisha mataifa yoye duniani ambacho kila kinapotoa taarifa za kuisifia serikali hiyo hiyo; viongozi wa serikali hiyo hiyo wamekuwa wakiisifu kwa utalaamu wake na wataalamu wake wanaofanya tafiti hizo. Halafu wanatulazimisha tutangaze kwamba kauli hiyo ya serikali ni ya kulinda ‘maslahi ya taifa’; Serikali ifafanue ni maslahi gani hayo ya taifa anayoyalinda kwa kauli hiyo ya ajabu?

  HITIMISHO

  Masuala haya na mengine mengi zaidi nikayoyachambua kadiri siku zinavyokwenda yanapaswa kujadiliwa na wananchi ama wawakilishi wao; ili tuweze kutoka na msimamo wa pamoja. Pia UN na Kundi la Wataalamu wake kuiuliza serikali itoe maelezo ya kina wakati wa mapitio ya taarifa husika. Ni utaratibu wa kawaida kwamba ufuatiliaji kama huu uliofanywa kwa kuwa ulihusu Tanzania; serikali itapewa fursa kuandika ripoti ya nchi (country report) kufafanua mambo ambayo yametajwa kabla ya kamati ya vikwazo kufanya maamuzi yake ama kuikubali ripoti husika na mapendekezo yake ama kutoa maelekezo mbadala ya kutaka uchunguzi zaidi katika maeneo ambayo Kundi la Wataalamu limeeleza katika ripoti yake kuwa uchunguzi wake bado haujamilika. Inashangaza kwamba serikali inatumia nguvu kubwa, kubeza ripoti hii na kutishia wanahabari wasiendelee kuandika wakati ripoti imeweka bayana kwamba uchunguzi bado haujakamilika; serikali itaweka wapi uso wake kama uchunguzi zaidi ukaibua uchafu zaidi?“Tuchafuke tusafishe tujisafishe: kujadili ni uzalendo wa kutetea maslahi ya taifa”   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bro upo sawa hapo?
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Selous

  Siko sawa. Ni kosa la uchapaji, ni mwaka 2007 si 2009. Tuendelee na mjadala

  JJ
   
 6. M

  Mikefe Member

  #6
  Feb 19, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama ni kweli kinachokuuma ni nini wewe mla mbwa.
   
 7. M

  Mikefe Member

  #7
  Feb 19, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bwana Mnyika wewe katafute mbwa kama kitoweo chako. Ni nini kinachokuuma.Kama ni biashara serikali imepata chochote zip ur stinky big mouth.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata kama uko kazini unaweza kuwa na lugha za kistaarabu kidogo kwa sababu hata ukitukana matusi sidhani kama yatasaidia kitu zaidi ya kujidhalilisha bure
   
Loading...