CHADEMA sasa kula sahani moja na mawaziri watatu wa JK hadi kieleweke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA sasa kula sahani moja na mawaziri watatu wa JK hadi kieleweke

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 22, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba


  Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeiagiza sekretariat yake kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kutokana na kauli anayodaiwa kuitoa kwamba chama hicho kinafadhiliwa na mataifa ya nje kufanya maandamano.

  Msimamo huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Alikuwa akitoa taarifa kuhusu uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam.

  Mbowe alisema hatua hiyo ilifikiwa baada ya CC kupokea na kujadili kwa umakini tathmini ya maandamano yaliyofanyika Kanda ya Ziwa, pamoja na matamko yaliyotolewa na viongozi wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

  "Viongozi hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Mawaziri Bernard Membe, Stephen Wasira, Sophia Simba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati.

  "Mambo mawili yanajitokeza katika kauli zao, kwamba maandamano ya Chadema yanahatarisha amani ya nchi kwa kuchochea wananchi kuitoa serikali iliyopo madarakani kwa njia ya maandamano," alisema.

  Mbowe alisema Simba anadaiwa kusema kwamba, Chadema kinafadhiliwa na mataifa ya nje kufanya maandamano hayo.

  Alisema kwa sababu hiyo, chama chake kitamwandikia barua waziri huyo kikitaka athibitishe nchi iliyotoa fedha kwa chama hicho, siku fedha hizo zilipotolewa na kiasi cha fedha hizo.

  Alisema endapo Simba atashindwa kufanya hivyo, chama chake kitampeleka mahakamani ili iwe ni fundisho kwa wengine wasije wakaongea maneno ya kukichafua chama hicho bila sababu za msingi.

  Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kwamba Chadema wamemtaka Waziri wa Nishati ma Madini, William Ngeleja, kuwajibika kisiasa kwa kujiuzulu kwa kuwa amepoteza sifa za kushikilia nafasi aliyonayo kwa kushindwa kusimamia sekta ya umeme kwa ufanisi kutokana na tatizo hilo kuwa sugu nchini.

  Kuhusu mabomu yaliyolipuka Gongolamboto, Mbowe alisema Chadema inaendelea kumhimiza Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi, awajibike kisiasa kwa kujiuzulu, kutokana na kushindwa kuchukua hatua thabiti katika kuhakikisha kuwa milipuko ya mabomu katika kambi za jeshi haijirudii.
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kelele za mlango hizo ambazo hazimfanyi mwenye nyumba kukosa usingizi.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,867
  Trophy Points: 280
  Hafif inaweza kuonekana ni kelele ila walichosema hao mawaziri walikuwa na lengo la kuiua chadema

  same techniques walitumia kuua CUF, waliposema inachukua misaada toka Oman, leo hii wanasema Chadema inachukua misaada toka abroad.Kosa kubwa ni kuwa wametamka ujerumani na hawakusema Italy! waliogopa!

  Kinachofanyika sasa ni kutoa taarifa kwa nchi wahisani wote na kibaya zaidi nchi waliotaja ni wafadhili wakubwa wa CCM na serikali yake, reactions za chini chini zimeanza kujionyesha kwa nchi wahisani

  Maamandano ya CDM hayakufikia hatua ya kusema wanataka CCM itokea madarakani. walichofanya CCM ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu za kutoa maoni yao!

  Yes chadema must deal with these three people specifically, NA KWA taarifa tu ni kuwa wakikomaa nao, hawa jamaa hawana support ya chama chao. watajishtukia wako peke yao, pity!

  cdm ikirudi nyuma na kufanya maneno tu kama kawaida yenu, kwa namna moja wamekiumiza chama na image yenu itakuwa kama hawa jamaa walivyosema.SIKU ZOTE HUWA NASEMA KUMBUKENI WAPIGA KURA, wengi hawana uwezo wa kujua hizi propaganda na kutenga makapi yapi na mchele upi! mkifikiri kila mtu anawaza kama nyie ,mmeliwa

  hawa watatu lazima jasho liwatoke, kwa hili I wish you the best
   
 4. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hahahahahahahhhhhaaaaaaaaaaaaaaaz!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Nimekushtukia uko kotekote weye,unakula na kupuliza weye.una lako jambo shehe.utafanikiwa tuu lakini jaribu bahati yako.mwenye macho haambiwi tazamo ati.mwenye maskio haambiwi sikia ati.lakini wewe ni kiboko kama antivirus flani hivi!!!.........subiri nakuja.....naenda comfortable room.

  Kashaga-[FONT=&quot]MacAfee-Antivirus 2011[/FONT]
  Mr-mak-[FONT=&quot]Kaspersky Antivirus 2011[/FONT]
  Nduka-[FONT=&quot]Avira AntiVir Personal 2011[/FONT]
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mna bahati sana wenzetu kwani hapo ukibanwa tu .................. ooooooh zilikuwa satanic verses!
   
 6. m

  masaiti Senior Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tumekwisha mshutukia, kuna watu wamemtuma na anawatumikia

   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Naomba kuuliza tu ndugu mtoa mada, ningependa unijulishe kuna vyama vya siasa Tanzania vingapi? na viongozi wakuu wa hivyo vyama ni wangapi? maana wewe umepoteza mwelekeo kila siku hapa thread zako utadhani ni mcheza tokomile ngoma ya Mkwere, hoja zako ni CHADEMA ukibadili ni Dr Slaa, au ndio maelekezo ya huyo aliyekupa modem na anaekulipia internet bundle hayo ndio maelekezo yake. basi kama anaikaguwa kazi yake aliyokutuma humu ni sifuri kabisa yaani kwa kifupi hamna kitu, nyinyi ndio mesababisha vichwa makini kujiweka pembeni JF kwa ajili ya vithread vyenu vya kikasuku, maana huna hoja zaidi ya Zitto Kabwe, Dr Slaa na Chadema. THINK BIG YOUNG MAN.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Leo rusha roho wapi? Wapambe kwa mipasho hamjambo, mnamzidi hata JK !!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu hiyo ni kuflu huyu jamaaa hamzidi JK hata kidogo JK mtoto wa mipasho bwana weeee!
  kelele za mlango single yake
  vyama vya msimu!
  Mmezidi ubabe!
  siijui DOWANS!
  Ukila lazima Uliwe!
  NK
  jk bigwa wa mipasho wewe huyo kibaraka wake hana kitu!
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Toka watoe tamko ni siku zimepita sasa,sijui wamefikia wapi!

  Hawa viumbe hawatakiwi kuachwa wapumue kabisa yani,mbavu mbavu
   
 11. w

  wheel-spiner Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni kundi la loosers..... ktk huu umbea hawachomoki...walizoea bungeni kukomaa na wapinzani na kuwaona wakichomoka kwa ushindi nao wakaingia...Sasa sijui watachomoka vipi na kesi ikiingia mahakamani si rais wala wapambe wake(oh mawaziri) watachomoka.

  Mbaya zaidi hawajui kuwa wakizidi bwatuka kwa woga wanawafundisha wananchi kufikiri kwa staili hiyo...then dr. Akiamua mgeuza Kikwete Gaddafi. Watalia sana. uzuri wa mataifa ya magharibi siku hizi ni kuwa wanataka raia waseme tuu.Kuwa hatumtaki....halafu wamwite mwizi Hela Zinarudi Halafu waseme Anashitaka kwa Ocampo..anapelekwa...halafau yanatokea haraka sana haya mambo. THANK CCM FOR GIVING IN CHADEMA SMART IDEAS
   
 12. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Started by Kashaga.

  Haaaa!!!!!!! Haaaaaaaaaa!
   
 13. Q

  QALQAL MARTIN Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  'Propaganda huwa zipo' lakini hili la hao mawaziri siyo propaganda. embu tukumbuke historia inatuambia nini,wakati uchaguzi mkuu 2000 ccm walileta propaganda km hizi dhidi ya cuf yafuatayo yalisemwa: cuf ni chama cha kidini, kigaidi(ikumbukwe Osama anawika) kama haitoshi siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa polisi akatangaza cuf wameingiza nchi kontena la silaha bila ufafanuzi wowote baada ya siku kadhaa tuliambiwa lililokamatwa lina visu, tukaonyeshewa visu vyenye alama za bendera ya cuf, kwa chama makini hizi propaganda hazikubaliki walipaswa kwenda mahakamani kujisafisha mbele ya umma. Hakika hata vurugu za Zanzibar huku bara hasa maeneo ya vijijini tuliona kuwa serikali ilikuwa sahihi kutokana na taarifa zilizokuwepo awali, kwa matiki hiyo cuf wanapaswa kujilaumu kwa kutokuwajibika....MUHIMU TUJADILI NINI MAANA YA PROPAGANDA, MIPAKA YAKE...
   
 14. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Hujui Kuwa Vyama vya Siasa Vipo ili Kupaza sauti za kelele??? Kuna siku mwenye nyumba atakosa Usingizi tu
  Nasikitika kujua kuwa na wewe ni Mtanzania!
   
 15. A

  Ame JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Ninavyo wafahamu CCM sasa hivi watakuja na deal babu kubwa na kuwa entice baadhi ya wabunge wa CDM na mara hao wanagawanyika na kujikuta hawako pamoja tena na mchezo unakuwa umeisha. CDm please dont disapoint the public juweni kuwa peoples power is more than nuclear power mkifanikiwa kuiteka.
   
 16. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Shairi la dr. Slaa

  [FONT=&quot]Jina langu ni Slaa, mzee mwenye balaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Watu wanishangilia, kwa zangu nyingi hadaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Nawadanganya kwa nia , napeta mwanangu shaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Niacheni nijisifieeee[/FONT]

  [FONT=&quot]Sifa nitawatajia, hadi hapa kufikia[/FONT]
  [FONT=&quot]Umalaya ndio njia, kuu niliyotumia [/FONT]
  [FONT=&quot]Wake zenu nachukua, ma-first lady kua[/FONT]
  [FONT=&quot] Niacheni nijisifieeee[/FONT]

  [FONT=&quot]Ya pili niwatajie, sifa niloshikilia [/FONT]
  [FONT=&quot]Muongo niliyepea, mchochezi na mmbea[/FONT]
  [FONT=&quot]Haya yanisaidia, wafuasi wamejaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Niacheni nijisifiee[/FONT]

  [FONT=&quot]Na wivu umenijaa, kwa JK hasaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Raisi aweje kua? Mkwere huyu kichaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Nitaanzisha balaa, nchi tushindwe kukaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Niacheni nijisifiee[/FONT]

  [FONT=&quot]Bado ninategemea, ushindi nitachukua[/FONT]
  [FONT=&quot]Kanisa naegemea, litanibeba kwa nia [/FONT]
  [FONT=&quot]Ndimi dakta theologia, Wilbroad Slaa[/FONT]
  [FONT=&quot]Niacheni nijisifieee  [/FONT]

   
Loading...