Chadema sasa ipo tayari kuongea na serikali...........

The Citizen halimilikiwi na CCM..mmliki wake ni Nation Media Group ya Kenya, ambayo inamilikiwa na His Highness Aga Khan
Mistake acknowledged....................
 
Haki raia wa Tanzania imeporwa na wageni hili si jambo la kuficha tena mpaka sasa.Lazima tuwe wawazi bila hivyo wasomi wa Tanzania watakuwa wakulaumiwa mpaka mwisho.

Wageni wapi hao tena?
 
Serikali wao wapo tayari kwa CHADEMA kufuata taratibu za kiserikali na sio wao wanavyotaka. Na mbowe ameisha sema wao hawasemi uchaguzi urudiwe na wala Slaa atangazwe kuwa Rais. Hii ina maana kuwa wameisha kubali kuwa JK ndio Rais. Na hapa maneno ya JK yanaanza kutimia kuwa' WATAKWENDA WATARUDI KWAKE KWANI YEYE NDIO MWENYE MAMLAKA YA KUWATIMIZIA HAYO WAYATAKAYO'

Wewe ni nani alikuambia kuwa chadema hawamtambui kikwete?? bona mnakuwa hamuelewi vitu vizuri mnakur
 
Serikali wao wapo tayari kwa CHADEMA kufuata taratibu za kiserikali na sio wao wanavyotaka. Na mbowe ameisha sema wao hawasemi uchaguzi urudiwe na wala Slaa atangazwe kuwa Rais. Hii ina maana kuwa wameisha kubali kuwa JK ndio Rais. Na hapa maneno ya JK yanaanza kutimia kuwa' WATAKWENDA WATARUDI KWAKE KWANI YEYE NDIO MWENYE MAMLAKA YA KUWATIMIZIA HAYO WAYATAKAYO'

Acha unafiki wako Sisi wananchi tunauwezo wa kuamua tufanye nini na si JK kama unavyofiki ndo maana toka Alhamisi jioni hadi leo CCM na viongozi wake wanalalama kwa kuwa wanajua wananchi wengi wanaikubali chadema na kuiamini.

Najua wengi wenu CCM mnajidanyanya kwa kelele wakati mnajua wakatiwa kampeni zilitumika Tsh. ngapi kuleta mpiga kura mmoja ile hali kwa chadema na CUF watu wanaenda wenyewe na wanatoa pesa za nauli kwa wagombea wa Chadema.

Mungu wajalie nguvu viongozi wa chadema.
 
Serikali wao wapo tayari kwa CHADEMA kufuata taratibu za kiserikali na sio wao wanavyotaka. Na mbowe ameisha sema wao hawasemi uchaguzi urudiwe na wala Slaa atangazwe kuwa Rais. Hii ina maana kuwa wameisha kubali kuwa JK ndio Rais. Na hapa maneno ya JK yanaanza kutimia kuwa' WATAKWENDA WATARUDI KWAKE KWANI YEYE NDIO MWENYE MAMLAKA YA KUWATIMIZIA HAYO WAYATAKAYO'

Msichakachue habari kwa maslahi yenu. Chadema haimtambui rais kupitia mchakato uliomtangaza. Chadema iliingia kwenye uchaguzi ikijua kuwa rais akishatangazwa hakuna sheria inayorusu kupingwa. Hili la pili ni tofauti na kutomtambua kutokana na mchakato mbovu. Wamefanya hivyo kivitendo na mafanikio makubwa. Hapo ndiyo maana kila upande unatafuta ncha (convergence point) kwa kuainisha issues.

"Wakienda watarudi" wapi? Kwani Kikwete ukiondoa kuhutubia bunge atashiriki vikao vya kawaida vya bunge? Jibu ni hapana watakutana wapi na wabunge wa chadema tena na kwa sababu gani?

Tatizo linalojitokeza ni ufahamu duni wa baadhi ya watu ambao wamejazwa ushabiki wa vyama vyao.

Mimi namshukuru sana Mungu kwa pande zote kutafakari mstakabali wa kuainisha matatitizo ya msingi ya taifa letu bila ushabiki. Hoja nani kashinda nani kashindwa haziwezi kutoweka kwenye nyoyo za watu. Lakini misinigi ya hiyo hoja ni ushabiki. Ushindi ni mstabali wa taifa kuelekea kwenye neema ya uchumi, amani ya kweli na maendeleo yanayokidhi mahitaji ya kila Mtanzania.

JK licha ya uraisi wa NEC ni mwanadamu aliye na fahamu timamu kuwa kuna tatizo la msingi, pia anajua gharama inayomkabili akicheka cheka tu na tatizo lililopo bila kuchukua hatua yo yote.

Sisi wanajamvi nashauri tujikite kuwasaidie viongozi wetu kuona mantiki ya mstakabali wa taifa iwe kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimataifa.

Ujumbe wa CHADEMA kutoka wakati wa hotuba ya rais umefika na umeanza kuzaa matunda.
 
Nadhani CHADEMA wako kwenye move nzuri mpaka sasa,hawajakosea mahali popote.wasiojua sheria na katiba ndo wanaoropoka hovyo humu.
Ila kazi tunayo ya kuhakikisha tunawaelimisha watu wote ambao Katiba na Sheria ya Tanzania inawapiga chenga na ndio walio wengi sana Tanzania.
Shida kubwa imeanza kwenye kujua HAKI YA KILA RAIA.
Haki raia wa Tanzania imeporwa na wageni hili si jambo la kuficha tena mpaka sasa.Lazima tuwe wawazi bila hivyo wasomi wa Tanzania watakuwa wakulaumiwa mpaka mwisho.

Sidhani kama tatizo liko kwa wasomi,tatizo ni waroho wa madaraka ndio wanaotukwamisha na kutupeleka katika njia isiyo sahihi kwa maslahi yao.
 
Waongee nini na serikali? Si waend wakaongee bungeni, serikali ya ccm sasa hivi iko bize katika kutimiza majukumu yake, haina time, wangoje bunge lijalo au wapayuke humu JF.
 
Jambo limekuwa jambo lenye maana Hapa naona kabisa ujumbe umefika na joto inapanda na kushuka kwa wahusika cha msingi sio nani atakwenda kwa nani azungumze nae ila ni nani ana Baraka za watanzania wengi kutuongoza kwa vitendo hilo ndilo lililopo wengine wengi humu wapiga debe tuu hakuna la maana zaidi ya kuchanganya watu mwenye hoja ya msingi na wananchi wakamwamini ndie atajulikana ubabe una mwisho wake hata mohamed ally alifika mwisho mobutu alifika mwisho chama cha upinzani kanu Kenya kilifika mwisho viongozi wababe wengi walifikia mwisho wa ubabe wao na ulazima wa wao kuongoza sasa sisi tufikie mahali tukubali nchi yetu sote tukubaliane na kutokubaliwa na wengi na tuendeleze kujenga nchi THE CHANGE IS COMING GUYZ WATCH OUT.
 
Tatizo la Chadema ni kutotafuta ushauri wa kisheria juu ya tafsir sahihi ya Ibara ya Na. 41(5) ambayo imeitaka NEC kuhakikisha inafuata taratibu zote zilizoainishwa kwenye sheria ya uchaguzi wakati wanamtangaza Raisi ili Mahakama au chombo kinginecho kiweze kuzuiwa kuwa kuhoji matamshi ya NEC ya kumtangaza Raisi..........................

Mimi ninaanza kuwa na wasiwasi wa kuwa huenda chadema hawana ushahidi wa kuhoji NEC kama kweli ilifuata au haikufuata sheria ya uchaguzi katika kumtangaza JK kuwa Raisi na ndiyo maana wanagwaya kwenda mahakamani
Ruta,
Ni nani anatuhumiwa kuiba? Alitumia kitengo gani, kulingana na tuhuma? Sasa unajua urefu wa mkono wa idara hiyo? then unawapelekea ushahidi?

Doesn't make sense to me to go to the court!
 
Waongee nini na serikali? Si waend wakaongee bungeni, serikali ya ccm sasa hivi iko bize katika kutimiza majukumu yake, haina time, wangoje bunge lijalo au wapayuke humu JF.
Would you use your brain even for few minutes?
You are intelligent than that!
 
CHADEMA! tuko nyuma yenu, tunaimani saana na wabunge wa CHADEMA wanasheria wako na wamebobea hawawezi kukurupuka tu kuna hoja nzito ndani yake, wananchi iliyobaki tuwaombee kwa Mungu awape hekima na busara ya kuweza kutoa kile kilichobora na sahihi tunachotaka ukweli na haki itendeke, watanzania sasa wameamka, sio wale waliokuwa usingizini eti! sio watu wakuburuzwa!
pamoja na kuchakachua matokeo, Mungu yupo, hakuna asichoona! na ukweli utajidhihirisha siku si nyingi! May God protect you all!

Mbunge ni mwakilishi wa mwanachi katika jimbo husika, sasa kama wewe (mbunge)umeingia kimabavu kwa ajili ya pesa yako, sijui utawakilisha nini bungeni!!
Nawahurumia wananchi wenye wabunge waliojipeleka wenyewe madarakani, kama Segerea, Kahama, Buchosa na huko mtwara.
Naomba Mungu ukweli uonekane, wanachi wapate wabunge wa kuwawakilisha kwa matakwa yao wenyewe
Madam Jane N.
 
Tatizo la Chadema ni kutotafuta ushauri wa kisheria juu ya tafsir sahihi ya Ibara ya Na. 41(5) ambayo imeitaka NEC kuhakikisha inafuata taratibu zote zilizoainishwa kwenye sheria ya uchaguzi wakati wanamtangaza Raisi ili Mahakama au chombo kinginecho kiweze kuzuiwa kuwa kuhoji matamshi ya NEC ya kumtangaza Raisi..........................

Mimi ninaanza kuwa na wasiwasi wa kuwa huenda chadema hawana ushahidi wa kuhoji NEC kama kweli ilifuata au haikufuata sheria ya uchaguzi katika kumtangaza JK kuwa Raisi na ndiyo maana wanagwaya kwenda mahakamani kwa visingizio vya katiba Ibara ya 41(7) ndiyo kikwazo kwao.................kama kweli wana matokeo yote kutoka vituoni na ambayo yalitangazwa na Wasimamizi wa majimbo nchi nzima na NEC hawakuyafuata katika kumtangaza JK kuwa ni Raisi na hivyo kukiukwa Ibara ya 41 (5) ya katiba yetu........hivi ni nini kinawazuia kwenda mahakamani......wakati matokeo ambayo hayawezi kuchunguzwa na Mahakama ni yale tu ambayo yametangazwa kwa kuzingatia Ibara nzima ya 41 na hii Ibara ndogo ya 41(5) imo?

Hawa chadema are playing with us but the question has to be for how long?

CCM haiheshimu maamuzi ya Mahakama, kwenda mahakamani ni kupoteza muda, hapa issue ni kuonyesha umma wa watanzania na jumuia za kimataifa kwamba tuna Katiba dictator, na msg imeshatumwa na kufika kisawasawa. Kama CCM wangeheshimu uamuzi wa Mahakama basi uchaguzi huu tungeshuhudia wagombea binafsi.
 
Back
Top Bottom