CHADEMA samehe yaishe

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Kama ilivyo kwa nchi nyingine kama za Ulaya, Marekani, Asia na Afrika zilizoendelea, Tanzania pia tunahitaji chama tawala kama CCM na vyama vya upinzani kama Chadema, CUF, NCCR, TLP,..... vyenye nguvu ili kuchagiza sera mbovu za vyama tawala na kuchochea maisha yenye ahueni kwa wananchi. Hivyo watanzania kwasasa tunaihitaji Chadema na CCM pamoja kama ilivyo kule Marekani wanavyohitaji Democrat na Republican pamoja, Uingereza wanavyohitaji Labour na Conservative kwa wakati mmoja, Ujerumani wanavyohitaji CDU, SDP na SSU na kwingineko kwingi kwenye maendeleo ya kweli.

Wananchi wengi hawana haja na vyama vya siasa ila wanachohitaji ni maisha bora, na maisha bora hayawezi kuletwa na chama kimoja tu kinachotawala, lazima kuwe na vyama shindani ambavyo vina uwezo wa kuingia Ikulu wakati wowote kama chama tawala kitakosea ama kuzembea katika kuwaletea maisha yenye unafuu wananchi wote wa dini, elimu, rangi, umri, afya zote, na ngazi zote toka vijijini hadi mijini. Hii ina maana kuwa watanzania wote tunaihitaji CHADEMA yenye nguvu hata kama haiko Ikulu. Chama tawala kinapokuwa kinajirekebisha kwa kuogopa chama kingine kisije kikawabwaga kwenye chaguzi mbalimbali wanaonufaika ni watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa wala za dini. Hata viongozi wa chama tawala mmoja mmoja nao pia huwa wananufaika na uwepo wa vyama vya upinzani vyenye nguvu kwakuwa hata wao pia wanao ndugu, majirani na marafiki waliotawanyika nchi nzima ambao wanahitaji maisha yenye nafuu pia ambayo hawawezi wote kuyapata kutoka kwao hata kama wao ni viongozi wa chama tawala. Hivyo, kuleta mtafaruki kwa vyama vya upinzani ili visiimarike ni kuwakosea wapwa zako, binamu, shangazi, wajomba, dada, kaka, baba mdogo, wajukuu, mashemeji na watanzania wote kwa ujumla ambao wanahangaika kupata maisha nafuu ndani ya nchi yao.

Kambi ya Zitto imekiri kuhusika na waraka ule wa siri wenye lengo la kuuangusha uongozi halali wa chadema, kosa kama hili ni kosa hata kama lingekuwa limetokea kwa vyama vya CCM, Democrat, Republican, Labor, Conservative, Jubilee, CDU, SSU, SDP, n.k. Tusimung'unye maneno hapa, Zitto na wenzake wamekosea, wamewakosea viongozi wenzao wa chadema, wanachama na watanzania wote kwa ujumla wanaonufaika kwa nja moja au nyingine na uwepo wa vyama vingi nchini.

Kinachotakiwa Zitto na wenzake wenye waraka ule wasimame jukwaani na kuomba radhi kwa kilichotokea, na watanzania wawe tayari kuwasamehe, kisha tutawafuatilia nyendo zao kila kona kila dakika. Ninaimani wanaonufaika na vyama vingi wako wengi kuanzia vijijini hadi mijini, mitaani hadi Ikulu, sungusungu hadi JWTZ, na vyombo mawasiliano vyote, watakosa kwa kujifisha tu. Watumie njia za wazi kutaka mabadiliko CHADEMA wataungwa mkono tu na wapenda demokrasia ndani ya chama. Kutenda kosa sio kosa ila kurudia kosa. Ujenzi wa vyama vya upinzani sio jambo rahisi hata nyakati zile za utawala wa Warumi na wakoloni, wapo watu wamepoteza maisha, mali, muda, wake, waume, watoto, damu, kupigwa, na kubezwa, kushitakiwa na kutiwa gerezani. Kuvihujumu vyama vya upinzani kwa aina na sababu yoyote ile ni kujihusisha na dhambi kubwa ambayo itagharimu historia ya maisha yako, familia na uko wako mzima.

Ana maana na heri ya mtu yule aliyepanda mti mmoja tu wa kivuli utakaoishi zaidi ya miaka 100 kuliko mtu mwenye mabilioni ya hela haramu asiyeweza kuishi nayo hata kwa miaka 30 mingine.

Inshallah chadema itaendelea kusimama na kuendelea kufanya kazi ya checks and balance kati ya watawala na watawaliwa
 
Mkuu, naona huitakii mema CHADEMA, yapo makosa ya kusameheana hasa haya ya ki-utendaji, lakini kosa la USALITI ni hatari sana.

Mtu akila nyama ya mtu hawezi kuacha, ataendelea tu - By J.K.Nyerere.
 
Back
Top Bottom