Mbowe na CHADEMA mnataka kumkwamisha Rais Samia kwakuwa amewalegezea kidogo?

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Friends and Enemies,

Mbowe na CHADEMA wanataka kutupeleka wapi Tena? Je, ni kweli kwamba walishazoea ile hali ya kupelekwa kibabe na mwendazake na wameikumbuka kisha wameanza kutingisha kibiriti?

Katiba mpya ni suala la mchakato, ni suala mtambuka na jumuishi kwa makundi mbali mbali ndani ya nchi hii.

Wao kama wanasiasa ni kundi moja tuh wenye maslahi yao na katiba hii, na maslahi yao kama chama cha siasa ni kushika Dola, lakini Kuna makundi mengine meengi ambayo nayo yana maslahi yao vile vile kama wao, sasa iweje wao walishikie bango kwa kiasi hiko hadi kutishia kuingia barabarani kufanya fujo?

Rais Samia kaahidi na kaomba apewe muda, hawataki na wanataka kulazimisha.

Magufuli hakuahidi, na alisema siyo kipaumbele chake, waliufyata na kukaa kimya, sasa tunawauliza wanataka KUMKWAMISHA huyu mama kwasababu gani?

Kwa kuwa ni Muislam au kwa kuwa ni mwanamke?

Wana ajenda gani kwani.
 
THE BIG SHOW ,

Natofautiana na wewe unapohusisha harakati za Chadema kudai Katiba mpa na suala la IMANI ya Rais Samia Suluhu pamoja na JINSIA yake.

Kilichotokea kati ya Rais Samia Suluhu na uongozi wa Chadema ni kupishana kwa mitizamo yao kuhusu muda gani ni sahihi kwa suala la Katiba mpya kushughulikiwa.

Sisi tunaowafuatilia viongozi hawa, tunapaswa kupima kauli na misimamo iliyotolewa na kila upande, na kuangali upande upi umejenga hoja iliyo sahihi.

Binafsi sijakubaliana na hoja ya Rais Samia Suluhu ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Zuio hilo linakwenda kinyume cha katiba na sheria zetu.

Pia sijashawishika na hoja ya Rais Samia Suluhu kwamba wabunge peke yao ndio wanaoruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Uamuzi huo ukitekelezwa utakipendelea chama cha Raisi, CCM, na kuvikandamiza vyama vingine vya siasa.

Vyama vya upinzani huku Tanganyika vina mbunge ktk jimbo moja tu, hivyo CCM watafanya mikutano ktk majimbo zaidi ya 200++ nchi nzima, huku Chadema wakifanya mikutano katika jimbo moja tu.

Kwa upande mwingine nadhani Mh.Mbowe anakosea anapolalamika, au kulazimisha, Rais akutane na Chadema. Kama Rais anaamini muda haujafika wa kuonana na Chadema basi wamuache aendelee na ratiba na majukumu yake aliyojipangia.

Kila upande hapa uendelee na shughuli, ratiba, na mipango yake. Raisi Samia Suluhu aendelee kurekebisha uchumi kama alivyoahidi. Chadema nao waendelee na operation yao ya kuelimisha kuhusu Katiba mpya, na wasibugudhiwe na mtu au chombo chochote.

Rais Samia Suluhu akirekebisha uchumi Watz wote tutafaidika. Chadema nao wakihamasisha kuhusu Katiba bora umma mzima utafaidika.
 
Katiba ni mchakato, kwann wanataka jambo hilo kwa kulazimisha? Bajeti ya kuliendea jambo hilo wanayo hao chadema?

Rais Samia Suluhu ajielekeze kurekebisha uchumi.

Chadema wao waendelee na program zao wanazoona ni muhimu kwa chama chao.

Suala la katiba mpya siyo vibaya Chadema wakaanza nalo, na Rais Samia Suluhu akawakuta mbele ya safari ikiwa atapenda kuwaunga mkono.
 
Danadana.com

E5MtGq9X0AQ9nRX.jpeg
 
Alituweza sisi pekeyetu au Taifa zima??

Nan alikuwa Ana nafuu??

Sasa ahuen imeanza kuonekana badala ya wao watulie nchi ipate Aman na utulivu wanaanza leta choko choko
Mambo ni mtambuka, wakati wewe ukiomba utulivu baada ya kusuffer wenzako wanaomba utulivu utakaochaguzwa na Katiba mpya ililiyotokea yasijitokeze tena. Shida iko wapi? Hutaki kuuza korosho kwa utulivu na uhakika?
 
Nakumbuka 2014 ccm iliweza tamka kwamba chadema ndio wanasababsha ajali zote zilizokua zinatokea road ...takwimu ilikua kubwa yavifo kuliko nch yeyote afrika mashariki nakati.
 
Sasa naamini kuwa kuna dini za kifirauni ambazo zinaondoa akili za kufikiri kwa kina kwa waumini wake. Kama mtu anakuja na wazo kama hili unagundua huyu anaweza baka hata mtoto mdogo.

Kwa sasa samia akikosolewa itaonekana ni sababu ni muislamu. Hii ni inferiority complex ya hali ya juu sana. Na wengi wanaamini hivi katika uislamu kuwa wao ni inferior ndo maana wanaonewa.

Hii lugha usingesikia kwa wasio na dini. Ila wenye dini inferior hawajiamini hata wakikosolewa wanakimbia kujifichia kwenye dini. Hopeless kabisa. ,😁😁😁😁

Mambo ni mtambuka, wakati wewe ukiomba utulivu baada ya kusuffer wenzako wanaomba utulivu utakaochaguzwa na Katiba mpya ililiyotokea yasijitokeze tena. Shida iko wapi? Hutaki kuuza korosho kwa utulivu na uhakika?
 
Friends and Enemies,

Mbowe na chadema wanataka kutupeleka wapi Tena??je ni kweli kwamba walishaziea ile hali ya kupelekwa kibabe na mwendazake na wameikumbuka kisha wameanza kutingisha kibiriti?...
Wanataka katiba mpya kwa bunge gani?

Watu wa maana wote wanetoka chadema.

Na hawana lolote la maandamano wakitishwa kidogo tu wataufyata.

Wanamjaribu.

Ukweli Watanzania sasa wanataka kujenga nchi yao na uchumi hawana habari na vyama vurugu.

Kila mtu anatafuta fursa.

Chadema wanajua Mama anazidi kubeba points dhidi ya chadema
 
Mkuu japo nakuunga mkono kuhusu jamaa wa CHADEMA...ila sikuungi mkono katika mambo yako ya "imani za kidini"....

Nope unakosea mkuu....

Japo simuungi mkono ndg.Mbowe...ila ndg.huyo si mjinga wa hayo mambo ya udini uliyosema hapo juu....

MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI

#KaziIendelee
 
Baada mla kitimoto kuondoka Ikulu umekuja na hoja zako za kishamba za udini na ukabila ! umetia aibu sana , huna hoja kabisa , na NATANGAZA KUKUDHARAU moja kwa moja katika kipindi chako chote hiki kifupi ukichosaliwa nacho hapa duniani .

Poor you !
Mkuu, hivi mfalme mbowe alipoenda kuhubiri ukabila kule kanda ya ziwa ulisema neno kweli?
Siungi mkono ukabila, ila sipendi undumilakuwili pia.
 
Friends and Enemies,

Mbowe na chadema wanataka kutupeleka wapi Tena??je ni kweli kwamba walishaziea ile hali ya kupelekwa kibabe na mwendazake na wameikumbuka kisha wameanza kutingisha kibiriti??

Katiba mpya ni suala la mchakato,ni suala mtambuka na jumuish kwa makundi mbali mbali ndan ya nchi hii,

Wao kama wanasiasa ni kundi moja tuh wenye maslahi yao na katiba hii,na maslahi yao kama chama Cha siasa ni kushika Dola,lakin Kuna makundi mengine meengi ambayo nayo yana maslahi yao vile vile kama wao,sasa iweje wao walishikie bango kwa kias hiko hadi kutishia kuingia barabaran kufanya fujo??

MMA samia kaahid na kaomba apewe muda,hawataki na wanataka kulazimisha,

Magufuli hakuahid,na alisema siyo kipaombele chake,waliufyata na kukaa kimya,sasa tunawauliza wanataka KUMKWAMISHA huyu mama kwa kuwa ni Muislam au kwa kuwa ni mwanamke??

Wana ajenda gan kwan hawa wachaga...
Ulifikiri kuwa Rais ni kwenda kucheza na kuimba taarab? Kwani lazima awe Rais? Anaweza kuacha kama hamtaki akosolewwe. Who the hell cares if you are a woman or a Muslim?
 
Back
Top Bottom