CHADEMA Picha na Maelezo: Hitimisho la Kampeni za Chaguzi ndogo Jimbo la Kalenga

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Ndugu zangu wana JF,

Leo ndiyo siku ya hitimisho ya kampeni zilizodumu kwa takribani mwezi mmoja kampeni za chaguzi ndogo jimbo la kalenga kufatia kifo cha aliyekuwa mbunge na waziri wa fedha marehemu Mgimwa, Leo chama cha Demokrasia na Maendeleo kinahitimisha kampeni zake kwenye uwanja wa Ifunda...nitawaletea kitakachokuwa kinaendelea....


=========
Mwenyekiti ameshawasili na msafara wa wabunge Nasari, Chiku, sugu,Wenje, Heche...Anasubiriwa mgombea atue na chopa.. CCM wamekimbilia mandali..

Chiku anapanda jukwaani anawaeleza wananchi umuhimu wa uchaguzi huu wa kalenga...

IMG-20140315-WA0031.jpg
Kalenga piga kura linda kura
View attachment 145026

 
Hizo picha ziko wapi au mmegundua uongo wenu utawatia aibu haraka mmetoa?
 
Sababu zipo nyingi sana za kuiadhibu CCM katika uchaguzi huu wa Kalenga lakini moja nako ni kubwa na muhimu kwenye siasa za nchi yetu ni kukataa kwa nguvu zote uagawaji au kupeana madaraka kwa misingi ya usultani/ufalme.

Tanzania kila mtu na fursa sawa ya kuongoza wenziwe mradi atimize vigezo na masharti lakini tunakataa kwa gharama zote kurithishana uongozi kama inavyotaka kutokea ktk jimbo la Kalenga

Wanakalenga, hima sana, hima wote mtuwakilishe vema, kataeni umwinyi na usultani

CHADEMA forever!
 
Hizo picha ziko wapi au mmegundua uongo wenu utawatia aibu haraka mmetoa?

Wewe dada yatakushinda, muulize Shonza na Faiza na HamyD, wako wapi? Wanatumiwa kama dekio alafu wanatupwa.Nakuonea huruma.
 
Anasema Chadema imefanya kampeni za kila aina. Anatoa ushuhuda namna ambavyo yeye ni mfano wa kukataa mfumo wa kurithishana ubunge.
Wananchi huko Kidamali wamemzomea mgombea wa CCM amempandisha jukwaani mke wake mzungu anaitwa Robbie. Wananchi wamezomea na kucheka sana. Nassar anapiga nondo za Arumeru, chopa hiyooooo inakatiza hapa umati unalipuka.
 
Mbunge mtarajiwa huyo katua hapa.
Sugu anasema wabunge wamekuja kukomaa hapa kwa sababu Grace ana uwezo. Anaeleza historia yake alivyokuwa mtu wa kawaida tu akaenda kuwa mbunge. Hakuwa mbunge kwa sababu baba yake alikuwa mbunge. Anawataka wananchi kesho watume ujumbe kwa watawala kwamba hilo halikubaliki. Alichokuwa nacho Mgimwa mkubwa hakiwezi kuhamishiwa kwa mtoto hats kidogo. Uchaguzi huu si wa Kalenga pekee...
 
Anaanza kwa kuwashukuru wananchi jinsi walivyoiunga mkono kwa amani kbs na ari ya juu kampeni ya Chadema. Anasema uchaguzi huu unaangaliwa na kila Tanzania kila mahali.
 
Anatuma salaam kwa polisi. Kwamba anawashukuru wao kuja mkutano wa Chadema lakini busara hiyo ya kuja kwa wingi Chadema wangeitumia pia kwenda kutisha mkutano wa CCM. Anamwambia RPC aache ukada wa CCM hatua hizi za mwisho mwisho.
 
Kila la kheri mfanye uchaguzi kwa amani na haki ikatendeke na ionekane kutendeka.
 
Mbunge mtarajiwa huyo katua hapa.
Sugu anasema wabunge wamekuja kukomaa hapa kwa sababu Grace ana uwezo. Anaeleza historia yake alivyokuwa mtu wa kawaida tu akaenda kuwa mbunge. Hakuwa mbunge kwa sababu baba yake alikuwa mbunge. Anawataka wananchi kesho watume ujumbe kwa watawala kwamba hilo halikubaliki. Alichokuwa nacho Mgimwa mkubwa hakiwezi kuhamishiwa kwa mtoto hats kidogo. Uchaguzi huu si wa Kalenga pekee...
Muulize Sugu mtoto wa Ndesamburo na mkwe wake walipataje ubunge pamoja na dada yake Lissu.
 
Back
Top Bottom