Chadema pelekeni makamanda jimbo la iramba magharibi kwa mwingulu mchemba

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Kutokana na mbunge wa Iramba Magharibi kutetea bajeti ya serikali kwa nguvu zote na matusi juu dhidi ya CHADEMA wakati wananchi wa jimbo lake wana hali mbaya kimaisha na maendeleo kwa ujumla ninashauri CHADEMA ipeleke makamanda kadhaa kule jimbo la Iramba Magharibi ili kumshitaki huyu mbunge kwa wapiga ambao walimchagua awawakilishe bungeni.

Huyu mbunge badala ya kuitaka serikali iandae bajeti ya kusaidia wananchi wake yeye eti anasema kwanza hasubiri bajeti na hivi karibuni alipeleka madawati 50 jimboni kwake. Sasa sijua ana maana kwamba bajeti haina maana kwa wapiga kura wa Iramba Magharibi??. Pia sijui kama hayo madawati 50 ndiyo yanatosha kunyanyua maisha wa wapiga kura. Halafu hizo hela za kununua madawati anapata wapi?

Ni jukumu la serikali ilioko madarakani kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwa kupanga bajeti inayoelekeza nguvu kwa wananchi wake. Na ni jukumu la mbunge kuhakikisha serikali inafanya hivyo sio jukumu la mbunge kuisaidia serikali kuwakandamiza wananchi kwa kupigania bajeti ya serikali ambao wananchi wenyewe wameshaona haina tija kwao.
 
Mkuu umenena Nguvu ya UMMA haijui ilivyo na C anaisikia itabidi CD kujipanga
 
Kama Dr. Kitila Mkumbo ni wa jimbo hilo, tunamsihi sana ajiandae kumun'oa huyu fedhuli.
 
Back
Top Bottom