CHADEMA pamoja na kushindwa uchaguzi bado mna deni kubwa wa watanzania

Mkuu hoja hapa ni Chadema kuomba msamaha ili kama ikajaliwa kirudi kwenye game. Mambo ya uteuzi yanahusika vipi? Ndio maana mnafeli sana.

Wanachama wengi wa chadema hawawazi maendeleo ya chadema, mahaba ni bora sana kwao kuliko brain

Ona walipofika sasa

Soon watapotea wote
 
Najua fika kuwa mlitegemea hili anguko ila mlifanya siasa kwa mazoea kwa kudhania kuwa Tanzania ya 1995- 2015 bado ni ile ile.

Hapana kabisa Tanzania ya leo sio kama hiyo mliodhania na kufikiria, sio Tanzania ambayo inahitaji wanaharakati au wanasiasa wajanja wajanja kama mlivyokuwa mmezoea.Ambao wao hutumia matukio au majanga kujinufaisha.

Tanzania ya leo imebadilika sana,haitaki harakati za kisiasa bali inahitaji maendeleo na panapotokea janga kubwa kama Covid 19 watanzania wanahitaji umoja wa kitaifa ili kukabiliana na janga kama hili.

Tanzania ya leo haihitaji mwanasiasa ambaye likitokea janga basi anataka apate manufaa ya kisiasa. Mfano lilipotokea janga la Covid -19, watanzania walimshuhudia Mbowe akisema mbele ya kituo cha luninga cha Aljazeera kuwa zaidi ya watu 30-40 walikuwa wanakufa kila siku Dar es laam peke yake. Hili ni jambo baya sana. Hata kama kuna watu walikuwa wanafariki lakini si kwa idadi kama hii,maana mitaani uswahilini ingekuwa kila mtaa ni msiba.

Kwa ujumla siasa za harakati,kupinga maendeleo ambayo yananufaisha watanzania wote na kutaka kutumia majanga makubwa kupata nguvu ya kisiasa imeigharimu Chadema ya Mbowe. Na hili limefanya wananchi waidhibu kwa kura.

Chadema imeanguka kifo cha mende na ili iweze kunyanyuka lazima ibinuliwe na wananchi maana haiwezi kunyanyuka. Hivyo mnatakiwa kuomba msamaha kwa wananchi hasa mlivyowakosea wakati wa janga la Covid-19. Pia kuomba msamaha kwa kuendesha siasa za kiharakati bila kusoma alama za nyakati.
Umenena vizuri mkuu ila kwa kuwa wanasaccos HAMNAZO! watakupinga tuuu!!
 
Back
Top Bottom