Chadema now has an upper hand and if they desire, they will shine!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,525
1,521
Kama kuna nafasi nzuri sana ya Chadema kuendeleza kuvuma na "mvuto" wao ni kwa sasa hivi wanapowasusia CCM na Kikwete kuleta msukumo wa nguvu sana kuleta mabadiliko ya Katiba na hata sheria za uchaguzi.

Ni ajabu kuwa Tanzania yetu hii, leo hii kunaaonekana wazi dhuluma kwenye upigaji kura na hasa kura ya Urais, lakini hakuna ruhusa kupinga hato matokeo au kulazimika kwa uchaguzi kurudiwa.

Ama kile alichokifanya Mkapa cha mwenye kura nyingi ndiye mshindi bila hata kupata nusu ya kura ni uuaji wa Demokrasia.

Chadema wana uwezo mkubwa sana kwa msimamo wao walioufanya wa kukataa kumtambua Kikwete kuanza kujenga hoja na hata kesi mahakamani ya kutaka Katiba yetu ibadilishwe na ikidhi mahitaji na matakwa ya Watanzania na si ya CCM pekee.

Hili lisisubiri 2014, lianze kesho!
 
Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
944
64
Rev, you have made it clear than ever, Watatnzania tushinikize katiba mpya na tume ya uchaguzi isiyo na wachakachuaji.
 
Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,707
637
..tena kwa kasi ya ajabu CHADEMA wanatakiwa kuwafundisha (kama si kuwaelewesha wananchi) nini maana ya kitendo walichokifanya leo. Kama ni kwa ma press conference, kama ni kwa mikutano ya hadhara majimboni kutoa shukrani kwa wananchi baada ya uchaguzi...litakuwa ni jambo la msingi sana. Hii ifanyike kama zilivyofanyika operesheni kadhaa kama ile ya Sangara n.k.

Watanzania wengi ambao wapo vijijini ni rahisi kurubuniwa na watu wa CCM kuwa CHADEMA labda kimefanya usaliti mkubwa, kususia hotuba ya Rais na hivyo kuonyesha usaliti mkubwa kwa wapiga kura hao.

Katika mchezo wa Drafti, hapa tunasema CCM wamepigwa king ya Nguvu.
 
Mwananzuoni

JF-Expert Member
Apr 22, 2009
290
69
Nakubaliana na wewe baba mchungaji kwa 110%

Mwanzo mzuri wa kuwashughulikia hawa si si emu. Bila kufanya hivyo hawatajua kama kuna upinzani. Na usitegemee kuwa CUF ni wapinzani. Wameshafunga Ndoa na si si emu.

Majemedari wa Chadema Kazi Imeanza. Tusonge Mbele kudai haki.
 
The Good One

Member
Oct 31, 2010
12
0
TUUNGANE SASA KUDAI KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHACHUZI BILA HIVYO TUTABAKI KUWA WA ZAMANI KAMA CHAMA CHA ZAMANI KINAVYOPENDA ILI WATUTAWALE NA WA TUTUNYONYE VIZURI!:nono:
 
Kagasheki

Member
Apr 12, 2010
34
0
Nakubaliana na watangulizi wa hapo juu kuwa kitendo walichokifanya wabunge wa CHADEMA jioni hii ni cha kuungwa mkono na wapenda demokrasia wote.Nina imani hawakukurupuka kuchukua uamuzi huu maana wana wanasheria mahiri na makini na hivyo kufikisha ujumbe husika kwa jumuiya ya kimataifa.Naamini matokeo ya tukio la leo ni mwanzo mzuri wa kuanzisha vuguvugu la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,la sivyo tutaendelea kudhulumiwa matokeo yetu halali yz uchaguzi.Hata C.C.M wanaotubeza ni wahanga wakubwa wa mfumo huu mbovu wa uchaguzi unaohalalisha uchakachuaji wa matokeo halali ya kura.Bravo CHADEMA
 
Mbega Mzuri

Member
Aug 1, 2008
44
2

Ni mwanzo mzuri wadau katika mabadiliko. if you want peace, declare war!!!
 
mzungukichaa

Member
Nov 8, 2010
57
27
Most of the time huwa napima mazungumzo ya kikwete na nimegundua kwamba huyu jamaa ana ufinyu wa fikira....Hebu Ona alichosema hapa
'Tumefanya vizuri sana upande wa michezo,tumeleta makocha wa kizungu kufundisha timu zetu..'...Hivi kweli michezo ni mpira tu ? hapa issue ni kuweka policy nzuri kuhakikisha micehzo yoote inainuka.....Hii ni akili mgando kabisa....
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
29
Hapo nakubali tunao watu pungufu ya 60 pale Bungeni (CHADEMA) wanaoweza kubadili mstakabali ya nchi yetu kwa faida ya maendeleo ya OUR MOTHERLAND wakati ndiyo huu.
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,549
8,670
Rev.Kishoka,
Duh! Hivi Chadema walitoka nje ya Bunge kwa sababu hawamtambui JK au kazungumza vitu ambavyo vinakidhalilisha chama chao!. Ebu nijuze wakuu zangu nimetoka kapa maanake hata huyo Ahamadinajad hutinga UN na hukaribishwa, only akiongea utumbo ndio watu hutoka nje.
Ni ujumbe gani Chadema wameutuma kwa wananchi?
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
935
Rev. Nadhani wazi kabisa chachu ya maendeleo imepamba moto nchini Tanzania.

Nimefuraishwa na swala zima la kususia ufunguzi wa bunge, sasa next move ni kwa Chadema kuandaa mfumo wa kujibu prime time speech za raisi kila anapomaliza kuzitoa, hasa zile speech za mwisho wa mwezi.Dawa ni kukaba full court na sio kwenye upande wenu.

Kilio cha tume mpya ya uchaguzi ambayo itachaguliwa kwa Bunge, na kwakutumia vigezo ambavyo vitawabana CCM wasiweke watu wao.
 
Mkandara ujumbe ni simple and clear kwamba njia uliyoingilia madarakani sio sahihi. Ni wazi kwamba ungeshinda, lakini ushindi wako kwa njia ya tsunami ni more lab technical. Hili linatumika kwenye mabunge mengi tuu, miezi iliyopita Republican walikaa wakati Obama anaingia kwenye ukumbi wa senate. Hii ni njia sahihi kabisa.

Walichokosea Chadema ni kutokujibu ile speech ya Jakaya na zile lawama za Pinda, ni wazi wananchi wanataka kusikia ni kwanini Chadema wametoka. Hapa panatakiwa mtu ambae ni good articulator (Mnyika) kujibu ile hoja. Kwa kutanabaisha ya kwamba ni dhahiri kabisa CCM wameingia madarakani kwa kuchakachua. Simple, dawa kuwabana full court....
 
Selemani

JF-Expert Member
Aug 26, 2006
890
208
Rev Kishoka, essentially wants people to do politics for the next 5 years. Somebody have to govern. Ukiwa na wabunge 46, huna mandate ya kugoma. You need the mercy of the majority to pass anything.

We will see, how this turn out. But Jakaya owned them on National TV today, and CCM will go out and govern. If Chadema wako kwenye mgomo, Sugu, Mdee, Mnyika and them will be on the ballot in 5 years. Tutaona wananchi watasemaje.
 
Selemani

JF-Expert Member
Aug 26, 2006
890
208
Most of the time huwa napima mazungumzo ya kikwete na nimegundua kwamba huyu jamaa ana ufinyu wa fikira....Hebu Ona alichosema hapa
'Tumefanya vizuri sana upande wa michezo,tumeleta makocha wa kizungu kufundisha timu zetu..'...Hivi kweli michezo ni mpira tu ? hapa issue ni kuweka policy nzuri kuhakikisha micehzo yoote inainuka.....Hii ni akili mgando kabisa....

Sio kwamba namtetea Jakaya, but wewe ni muongo. I watched the speech live. Aliongea kuhusu umuhimu wa kuwa na walimu wa michezo na kuwa na academy. Uongozi bora wa michezo, na akasema kaleta wataalamu kutoka nje kusaidia. Akaendelea kujifagilia kuhusu kuwa fundi wa kikapu.

You can disagree, lakini usipindishe ukweli kutimiza tu utashi wako wa kishabiki
 
Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,696
1,682
Rev.Kishoka,
Duh! Hivi Chadema walitoka nje ya Bunge kwa sababu hawamtambui JK au kazungumza vitu ambavyo vinakidhalilisha chama chao!. Ebu nijuze wakuu zangu nimetoka kapa maanake hata huyo Ahamadinajad hutinga UN na hukaribishwa, only akiongea utumbo ndio watu hutoka nje.
Ni ujumbe gani Chadema wameutuma kwa wananchi?

Mkandara, kama mke wako akikunyima unyumba lakini hakuombi talaka, ina tafsiri gani kwako?
 
Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
107
Rev. Nadhani wazi kabisa chachu ya maendeleo imepamba moto nchini Tanzania.

Nimefuraishwa na swala zima la kususia ufunguzi wa bunge, sasa next move ni kwa Chadema kuandaa mfumo wa kujibu prime time speech za raisi kila anapomaliza kuzitoa, hasa zile speech za mwisho wa mwezi.Dawa ni kukaba full court na sio kwenye upande wenu.

Kilio cha tume mpya ya uchaguzi ambayo itachaguliwa kwa Bunge, na kwakutumia vigezo ambavyo vitawabana CCM wasiweke watu wao.

nimeipenda hiyo sema tu sioni kitufe cha senks ninge kutwangia
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom