CHADEMA nomaaaaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA nomaaaaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makandokando, Feb 3, 2011.

 1. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna chama lingine lolote katika historia ambalo limeweza kutesa kama CHADEMA?

  Hakunaaaaa!

  Yaani kwenye mkutano wa CCM walikuwa wanaongelea CHADEMA.

  Waziri wa CCM anasema CHADEMA oyeee!

  Halafu tofauti na vyama vingine vya upinzani ambavyo vina jina mojamoja.....kwa mfano enzi zile za Mkapa tulikuwa tunamsikia Mrema tu. Kwenye CHADEMA majina makubwa mengiii...yaani ukisema Dokta kila mtu anajua unaomuongelea nani....ukisema ZITTO, MBOWE, TUNDU, MNYIKA, MDEE...yaani

  Kama watu hawajatunisiwa au kumisriwa miaka hii minne, basi 2015 ni mwaka ambao utakuwa interesting sana.
   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Huu ndiyo wakati hasa wa kubadilisha nchi yetu. Chadema wanapaswa kutumia wakati huu katika historia kujijenga zaidi. Pia wajitahidi iwezekanavyo kumaliza tofauti zao ndani ya chama.
  Ushauri wa viongozi, kuna mambo wanafanya ambayo yanawafanya wengine waanguke(stumble), Watanzania wengi si waelewa kiasi cha kumwelewa kwa nini kiongozi anashikana mkono na kiongozi wa upinzani kwa furaha. Ni jambo dogo lakini wakiendelea hivi ipo siku watapoteza mvuto. Bado watu hawaelewi upinzania ni nini. Kwa hiyo naomba mwendane na uelewa wao na si kuwapa maana za upinzani wakati bado hamjapiga hatua ya kutosha.
  Mungu awabariki na kuwaongoza.
   
 3. m

  mshaurimkuu Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonekana ndugu wewe ni shabiki damu damu wa chama chako - ni sawa ila nadhani kwenye mijadala humu JF tujitahidi kuweka ushabiki pembeni. Umeuliza:

  "Hivi kuna chama lingine lolote katika historia ambalo limeweza kutesa kama CHADEMA?"

  halafu unajijibu mwenyewe:

  "Hakunaaaaa!".

  Sijajua vizuri hiyo "historia" yako unayouliza ni ya wapi na kutesa kupi; Tanzania au duniani kote? I think it is too early to "praise" Chadema to that extent. Mkakati muhimu zaidi nadhani uelekezwe kwenye kuhakikisha yule "ADUI" (I hope you understand) na mbinu zake zote chafu (UDINI, UKABILA, MATUSI, kuhonga waandishi na viongozi wa dini uchwara - PROPAGANDA ZOTE CHAFU) anatokomezwa halafu hayo mengine yatakuja automatically.

  Kwa ufupi, kinachotakiwa ni ku-mobilize watu wajue haki na wajibu wao wa kiraia na kikatiba mengine baadaye. Hili ndilo tatizo kuu linalowasumbua wananchi kwa sasa.
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu watu wanajua mbivu na mbichi zisizoliwa!! technolojia ya habari japo ya kuchakachuliwa inawafikia walengwa na wanafahamu fika.Maisha magumu wanayopambana nayo ni somo tosha!!
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimekupa Thanks kwa kugusa mambo ya msingi, lakini ukweli unabaki kuwa watu wanaonyesha hisia zao kutokana na siku za karibuni/jana vyama vya upinza hasa CUF kukurupuka na kuanza kuwatusi viongozi wa CDM kwahiyo ni halali kwa huyu mtu kuonyesha unaazi wake kwa CDM na hakuna kitu kizuri kama kuwa mwazi je wewe uko upande gani maana hata CUF sasa watumia nguvu kubwa kuidhoofisha CDM bila kujua waTZ wanahitaji nini.
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu kinachotakiwa ni nguvu ya umma. Tukileta haya mambo ya vyama mchakato woote utavurugika, vyama vitapoteza muelekeo, ukombozi wa kweli ni pale watu watakapoamua kufanya kilicho sahihi...

  Utashi wa viongozi umekuwa corrupted vya kutosha... Nakuhahakikishia kwa hali ya misha invyokwenda, tutachoka tu na kuwafanyia hawa jamaa...
   
 7. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Mi najua kuwa hata wewe ukweli unaujua, unaweza kujaribu kuchakachua mjadala, ukweli unabaki palepale....by the way, leo mnakatiwa umeme saa ngapi huko kwenu?
   
 8. f

  furahi JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Umenifurahisha sana mshauri mkuu! Ndio ujue kuna some People are crazy about CDM. Which is good anyway..
   
 9. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mi nadhani wakati huu ni wa kukimarisha chama zaidi, tuhakikishe tunafungua matawi kila kona ya nchi, tumpe support kubwa mzee wetu, Dkt SLAA, hajakaa benchi kihasra hasara, kwanza ni faida kwetu coz tumepewa muda mrefu wa kuweza kufika vijijini hasa uko stimbi na Kishimundu ambako awjui chama kingine tofauti na hicho kibovu, tunatakiwa kuaweleza ukweli kuhusu NEEMA za nchi hii jinsi zinavyowanenepesha akina Azizi afu raia anakufa kwa mbu! Tunatakia kupanda mbegu ya kutaka haki zao akilini na kwenye ubongo wa Wananchi wa kpato cha chini sana, wao wenyewe wahukumu kama ni kumpiga mawe Kikwete au kuichoma nyumba yote ya CCM afu wajenge nyumba mpya! Tuache kujisifu kwanza, Sifa zitakuja tujifanikiwa kuiponya nchi hiii!!
   
 10. m

  mshaurimkuu Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu gidytitus nakupa big-up, kama vile ulikuwa kwenye ubongo wangu. Nilichoshauri; ushabiki uliopitiliza bila mipango na mikakati madhubuti ya kusonga mbele hausaidii. Sawa, ushabiki/unazi wako (wa chama chochote) haukatazwi, lakini toa mawazo na hoja za kujenga badala ya kupayukapayuka - haisaidii sana. Nilitegemea kusikia hoja zenye titles kama vile:-

  (i) Adui wa Nchi Yetu ni Nani?

  (ii) Jinsi ya Kumtambua na Kukabiliana na Adui

  (iii) Chama (chako) Kitumie Mbinu Zipi Kukabiliana na Adui

  (iv) ... nk.

  Mwingine anaweza akajenga hoja kwamba labda titles hizo ni nyepesi mno na hakuna asiyemjua ADUI lakini kwa taarifa yako ni wananchi (I mean the real wananchi - mvuja jasho) wachache mno wanojua ADUI wa nchi yetu ni nani; kwa nini nchi hii haisongi mbele - ni wachache wanaojua. Naamini pia viongozi mbali mbali wakiwepo wa vyama vya siasa wanasoma thread hizi, tungeweza kuwasaidia sana kwa mawazo yetu mazuri lakini hivi ukimwambia Dr. Slaa kwa mfano "Chama chako ni nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!", then what? Unakuwa umemsaidiaje?

  Lakini kwa mfano ikaja thread "Asili, Falsfa, na Athari za Udini Tanzania - Ukweli au Jinamizi na Hofu ya Watawala Malimbukeni Tu?", nadhani ingesaidia sana.

  Nawasilisha.
   
 11. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I CONCUR!! NYONGEZA ;;;;;; ILIBIDI pale aende mtu mwingine wa chini badala ya Mbowe ili kuonyesha seriousness you upinzani wao! sina maana kuwa seniors ni adui wa chama tawala bali ni kuijenga jamii ielewe hatua kwa hatua maana ya upinzani hasa kwa kuzingatia kuwa chama tawala hupendelea sana kutumia propaganda za chinichni kupotosha!!
   
 12. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,721
  Likes Received: 1,630
  Trophy Points: 280
  ni zaidi ya Nomaaaaaaaa, kila nikiifikria nashindwa kujua nguvu za CHADEMA, kilichopo ni kuondo virus vichache vya UWT ndipo kitulie, IPO haja na CDM kutuma Kirus kwenye CCM kuchunguza wanayozungumza, sisis virus wa CCM hatuviogopi kwa kuwa hatudanganyiki kwa Vijisent vya ROSTAM
   
Loading...