CHADEMA, Njia ya Ikulu ni nyeupe ila barabara sio tambarare... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Njia ya Ikulu ni nyeupe ila barabara sio tambarare...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Oct 15, 2012.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Chama cha demokrasia na Maendeleo kikiwa kiko mbioni kuingia ikulu 2015, kikiwa kwenye mikakati na utayari haitakuwa rahisi kwani wapinzani wao CCM wanatumia njia zote kudhoofisha mapambano haya kwa hila za kila hali. Chadema itaingia ikulu kwa uhodari na umahiri wa wanachama wake na viongozi wake kwa kufanya kazi usiku na mchana.

  Nchi zilizoendelea kidemokrasia na kiuchaguzi vyama vyao haviingi ikulu kirahisi hata kama vimewahi kushika madaraka miaka mingi, na vyenye mitandao mizuri na wapiga kura wengi wenye elimu ya uraia nzuri.

  Kwa miaka hii mitatu tutaona Chadema ikipitia vipindi mbali mbali.

  kipindi cha kwanza ni kuandamwa na vyombo vya dola kwa kila hila kama kuuwawa kwa wananchi kwenye shughuli za chama kama polisi tayari wamefanya arusha, Morogoro, iringa, igunga, Arumeru, baada ya kilio kikubwa cha wananchi vyama visivyo vya kiserikali, taasisi za kutetea haki za binadamu za ndani na nje ya nchi kupiga kelele mbinu hii inawafanya serikali ya CCM kutafakari upya.

  Mbinu nyingine watakayo tumia au wameanza kuitumia ni kurubuni au kuingiza mamluki ndani ya chama ili kudhoofisha moto huu wa mageuzi, dalili za watu kurubuniwa zinaonekana tayari, lakini wale mahiri na makini wamegundua mapema, mbinu hii inatumiwa sana na wanasisa wa kiafrika kwani ni rahisi ikizingatiwa umasikini na ahadi za kupewa madaraka upande mwingine ndio vinakuwa ndoana kubwa wanayoitumia.

  Msigishano wa mamluki utaongezeka ndani ya chama tukikaribia 2014 kwani ndio kipindi serikali ya CCM itamwaga fedha kama njugu ikijua inakata roho. Rushwa ndio kifo namba moja cha demokrasia ya Afrika.

  Mbinu nyingine kuwagombanisha viongozi wa CDM na wananchi ambapo mbinu hii imeshindwa mara nyingi sana.

  Vijana na wazee wa Chadema tutambue wazi hii vita sio vita ya mtu mmoja mmoja ni vita ya wananchi kujikomboa na kuunda serikali ya watu inayotokana na watu kwa manufaa ya watu na kizazi chetu.

  Huu sio muda wa kulumbana na wale wote wenye nia ya kudhoofisha haya mapambano, katika mampambano kama haya historia inaonyesha wale waliotegemewa walisaliti wengi na wale wasiotegemewa walivusha boti ng'ambo ya pili.

  Chadema ni chama cha wananchi ni wajibu wetu wote wanachama kuhakikisha hakuna wa kutuzuia kuingia ikulu 2015. Eyes on the prize not on somebody.

  Tunahitaji ushiriki wa kikamilifu na sio wakinafiki. Na ujumbe kwa viongozi wasituchanganye "clean your closets because no mercy with traitors" Tunawamini viongozi wetu wote na tunataka huu ndio uwe muda wa kufanya kazi "Team work" hatuna muda wa kusikiliza craps za tamaa nia ni kuingia ikulu , kuleta katiba mpya ya wanachi, kuhodhi mali za asili, na uchumi wa nchi kwa faida ya Mtanzania, kuinua elimu iliyooza ya mtanzania, miundo mbinu imara na kutoa lolongo kwenye mambo muhimu.

  Hatuwezi kuingia ikulu na majeraha tunaingia ikulu wote wakiwa kwenye boti, kama kuna anayeona hawezi kushika bomba ashuke sisi tunasonga mbele muda wa kubembelezana wakati tunalala gizani, hospitali hakuna dawa na wachache wanaishi peponi wakijifanya ni masikini wenzetu hatuwezi kuwavumilia.

  Mtanzania masikini hana uhakika wa kula mlo mmoja kwa siku halafu leo waliojuu ya magari na mishahra zaidi ya milioni sita wanataka kujifananisha na sisi hakuna mwenye maisha kama yetu aliyeko bungeni msituletee lugha za kuuza maneno. kubalini tunawaunga mkono kwa sababu tunawaamini tu.

  Sasa tunahitaji utulivu wakati huu tunapoihitaji nchi yetu kuliko wakati mwingine wowote.

  Makamanda twendeni kazi.
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahhh mimi naona kama operation zitaendela na kuimarisha muundo wa CDM hadi angalau ngazi ya tawi, Ikulu ni mteremko tu. Mpaka sasa miundo mingi imeishia kata. Viongozi wengi walioingia mwanzo katika baadhi ya matawi wameingia mitini na hakuna wanachokifanya, huwa wanaibuka vingozi wakubwa wanapotembelea hizo sehemu. Tukazane kutengeneza uongozi kwa mujibu wa katiba, tumuunge mkono katibu mkuu kwa nguvu zetu zotee kufanikisha hili. Ikulu geti liko wazi mbona.
   
 3. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  safari hii ya miaka mitatu iliyobaki si lelemama kama kamanda ulivyosema,we need to use all our resources frm our minds to tackle ccm,twafaham mbinu zao zote na mikakati yao,na hakika Mwenyezi Mungu husimamia haki,twafaham hakuna la kuletewa lazima tutafute kwa jasho,uzuri watz walio wengi wanatambua,wamekuwa wakipaza sauti pamoja nasi.na hakika tukisimamia kwa nia moja matakwa ya walio wengi hakuna wa kuzuia cdm kuingia ikulu,lakini kwanza watz wazitambue haki zao na nani amezihodhi haki hizo kwa maslahi ya nani.ndipo watasimama pasi kuyumbishwa kumuondoa mkoloni mweusi kwa sanduku la kura.tuko pamoja kamanda!
   
 4. piper

  piper JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Well stated ni muda mwafaka wa kushughulika ipasavyo kwa CDM na kuondoa tofauti zilizopo na zinazoweza kujitokeza
   
 5. real thinker

  real thinker Senior Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  The end of the domination of magamba in tanzania is going to be end up, cdm be pantual on the journey of to take the power!
   
 6. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi bado nzito kamanda, viongozi inabidi wasikae ofisini!
   
Loading...