Uchaguzi 2020 CHADEMA nidhamu inawapungua katika kampeni zenu, mnaweza kukosa baadhi ya kura kwa kutafsiriwa kama msio na maadili

El Roi

Member
May 29, 2020
61
150
Ukiona kampeni za CHADEMA siyo siri zinasisimua. Naweza nisiwe hasa na sababu zinazoeleweka, lakini ukweli unabaki kwamba ni kampeni nzuri.

Kuna tatizo la utovu wa nidhamu ninaloliona ambalo bila shaka litawafanya watu waliostaarabika kuinyima kura Chadema au kuwa katika mtanziko.

Nijuavyo mie Tundu Lissu bado ni mgombea na hajawa mheshimiwa Rais kama anavyoitwa kwenye majukwaa ya kampeni. Inakera na haipendezi kusikia mgombea akiitwa Rais.

Sijui sababu kwa nini haitwi mgombea. Hivi mnajua kwa hakika kwamba kuna watu hawataenda kumpigia kura kwa sababu ya kuamini kesha kuwa Rais? Lakini mbaya zaidi watu wanaoelewa mambo na wasitaarabu wanatafsiri hiyo kuwa fujo na kutojua kuyaweka Mambo mahali pale.

Na ni ukweli usiopingika pia kwamba, mnainyima hadhi nafasi mnayotafuta lakini pia kutotenda haki kwa Rais na mamlaka iliyoko madarakani sasa.

kama Kuna mtu aliwadanganya kufanya hivyo kuwa ni suala la kuongeza matumaini (optimization) ukweli ni kwamba inaudhi na iko out of touch kwa watu wastaarabu na wanaojielewa. Embu muiteni mgombea urais na siyo Rais.

Mkidharau kuna kura mtazikosa manake mtatafsiriwa kama watu unethical, riotic and uncivilised.

Wasalaam
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
8,513
2,000
Ukiona kampeni za CHADEMAsiyo siri Zina zinasisimua. Naweza nisiwe hasa na sababu zinazoeleweka, lakini ukweli unabaki kwamba ni kampeni nzuri.

Kuna tatizo la utovu wa nidhamu ninaloliona ambalo bila shaka litawafanya watu waliositaarabika kuinyima kura Chadema au kuwa katika mtanziko...
Asante kwa ushauri wako mzee mama.

Naomba uwape na ccm ushauri huo huo , waache kumuita Hussein Mwinyi Rais Mteule.
 

mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,127
2,000
Binafsi nimehudhuria mkutano wa CCM kuanzia Bukoba Mjini na Biharamulo. Kagera na haswa Biharamulo wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea wa CCM John Magufuli, yanayosemwa ni uzushi tu..ukweli usemwe, Kama hukua eneo la tukio usipoteze muda kubishana
Yah ni kweli watu hawamtaki kabisa
Magufuli atapoteza huu uchaguzi

Akijaribu kuiba ndo ataharibu kabisa
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
447
500
Iyo ni kawaida kwa mashabiki wa vyama kipindi Cha kampeni ata Lowasa ali itwa Rais. Ukweli uliopo uchaguzi wa mwaka huu Upinzani ni kama haupo kinacho fanyika ni futuhi.
Utabaini uhalisia muda ukifika,kwani kwasasa mbinu zote chafu zinatumika,ikiwa ni pamoja na kuwanyima coverage.
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,263
2,000
Ukiona kampeni za CHADEMA siyo siri Zina zinasisimua. Naweza nisiwe hasa na sababu zinazoeleweka, lakini ukweli unabaki kwamba ni kampeni nzuri.

Kuna tatizo la utovu wa nidhamu ninaloliona ambalo bila shaka litawafanya watu waliostaarabika kuinyima kura Chadema au kuwa katika mtanziko...
Unaumia bure kwa kitu ambacho huna control nacho. Eti watu hawataenda kupiga kura kwasababu wanajua ameshakuwa rais? Yaani mtu mzima unafikiria kitu cha namna hiyo? Inawezekana kwasababu ccm imedumaza akili za watu. Wewe mgombea anawafokea kwenye mkutano na kujiapiza kuwa hataleta maendeleo kwasababu mmechagua, unadhani zawadi yake ni nini kama siyo kumkataa?

Endapo kuna fujo itatokea, itasababishwa na wahuni wa ccm na si vinginevyo.
 

anophelesi

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,031
2,000
Ukiona kampeni za CHADEMA siyo siri Zina zinasisimua. Naweza nisiwe hasa na sababu zinazoeleweka, lakini ukweli unabaki kwamba ni kampeni nzuri...
Pole sana mkuu, naona umeumia sana. Kunywa maji ulale. Raisi wa ukweli na haki ni yeye 2020.
 

Mibas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
3,747
2,000
Ukiona huridhiki na style ya kampeni za Lissu na wafuasi wako, peleka kura kwa wagombea unaoridhika nao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom