CHADEMA, Ni wakati wa kujadili Rasimu! Agenda ya Zitto wekeni kando, hamtaeleweka

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,759
2,000
Nakipenda sana chama changu za cdm, kwa kuwa hakina mbadala katika kutetea Taifa hili, kimevumilia mengi, kimepita mabonde na milima, wanachama wetu wamemwaga damu katika juhudi hizi za ukombozi wa pili.

hata hivyo ninajua kuwa kamati kuu inakutana wiki end hii na kuwa agenda ni kuwavua uanachama wasaliti, sina kinyongo katika hili, ila NAOMBA KUTOA TAHADHARI, KILA JAMBO NA WAKATI WAKE, HUU NI WAKATI WA KUJADILI KATIBA MPYA NA MUSTAKABALI WA NCHI YETU, WENZENU CCM WANASUBIRI KWA HAMU MLIANZISHE NA ZITO WALICHOCHEE KAMA KAWAIDA NA BAADA YA HAPO WAIKARABATI RASIMU WANAVYOPENDA WENYEWE, MKIMALIZA UGOMVI TAYARI MTAKUWA MMECHELEWA.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,151
2,000
kaka mbona habari ya ZITTO imemalizika kitambo sana ! Au wewe ndiyo unataka kuiendeleza ?
 
Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,723
2,000
Wanaoendeleza story ya Kabwe ni MaCcm, Chedema mbona kitambo tu tulishamaliza kamuzizi!
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,087
2,000
Mbiwe na siloi hawakualikwa katika makabidhiano ya ripoti ya tume?
 
Wa Kwilondo

JF-Expert Member
Sep 15, 2007
1,083
1,250
Mkuu Mwikimbi issue ya zito imeisha kitambo wk hii wanakamilisha tu! Tunatupa kule msaliti watakao baki wanajadili ni ccm siyo cdm ! Mbaya zaidi dogo ameshazunguka ss sijui safari hii atarudi tena kigoma na mabango? Ha ha ha cdm wajanja sana walimtega MM akaingia mzima kwa ss wanamtimua kilaini bila kelele
 
Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,451
1,170
Watanzania wenzangu kwanza natoa salaam zangu za heri ya mwaka mpya.
Napenda kutumia jukwaa hili kutoa maoni yangu juu ya sakata hili lililopo mbele yetu kati ya Zitto na CHADEMA kwa ujumla wake.

Kwa ufupi ni kuwa sakata hili limetikisa chama na wanachama wake wote! na ukweli umejaribu kuwekwa hadharani na mwenye macho kaona mwenyewe na kusikia mwenyewe. Sasa kuendelea kutunishiana msuli huku kila mtu akitaka kuonesha ni nani zaidi, sioni kama ni jambo muafaka kwa sasa. Kuna haja ya kukaa chini kama binadamu na kuonyana na wale wote ambao wamekwenda kinyume na Katiba wakili na waombe msamaha.

Zitto wewe bado ni kijana mdogo sana na kete yako ya kufika mbali bado ipo wazi kabisa, hivi kama ni uongozi ni kitu gani kinachokusukuma kwa nguvu namna hiyo kana kwamba dunia inapinduka kesho na usipoongoza leo utakufa????!!
Je, ni wangapi ndani ya CCM waliambiwa kuwa hawana hadhi hata ya kuwa wajumbe wa nyumba kumi lakini leo ndio wanaotuongoza?

Je, umewahi kujitafakalisha ni jinsi gani walivyoamini kuwa bila Nyerere na Tanzania itakwisha lakini bado tunadunda ki mtindo?!

Je, kwa nini usivute subira na ukatumia muda mwingi kujenga matakwa yako kwa wananchi ambao sasa muda wao wa kushika hatamu unawadia (kwa mujibu wa Katiba mpya) ambapo tutakuwa na mandeti ya kuongozwa na tunaemtaka?

Mambo yapo mengi sana ya kuainisha katika kufikia mustakabali wa jambo hili, ila kwa ufupi tu naomba tuingie mwaka mpya kwa mambo mapya ya ujenzi wa chama kwa nguvu mpya.

Naomba Kamati kuu mtakapoingia kwenye kikao chenu hapo kesho kutwa isiwe ni kwa kumkamia Zitto, bali iwe ni jinsi gani ya kumtengeneza upya ahesabike kuwa mtoto ndani ya familia ya CDM.

Nawe Zitto, ukweli ni kuwa umekuwa na mambo mengi sana ambayo kwa macho hata ya upofu yanionesha kwenda kinyume na mipango mikakati ya chama, kama kweli unataka kubaki ndani ya CDM jifanye mdogo nasi tunaokuangalia tutakuinua hata kwa maombi yetu.

Je, nani angejua kuwa ipo siku moja sauti ya wanyonge itasimamam na kusema tunataka hili katika katiba yetu na likasikilizwa?! Je, mbona leo ipo hivo?

HIZI NDIO SALAAM ZANGU ZA MWAKA MPYA.

TAFAKARINI.
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Chadema imeshapoteza dira na kama iliweka nanga basi ndio kamba imeshakatika ,akirudi zito akifukuzwa it will test the same ,Chadema mbali ya kuwa chama chenye harufu ya kidini kimeongezea na ukabila ,wale wasio na uhusiano na kabila la wakuu huwa kama watumwa ndani ya Chadema.

Watumwa hawa huwa hawana kauli wala hawawezi kutetea au kusemea lolote lile ,ni kama ng'ombe aliefungwa shemere ile kamba puani ,hawezi kupinga wala kutoa wazo ,na ikiwa mtumwa huyu atataka kuwa huru basi ajaribu kupinga ya wakuu japo kwa hoja atakiona kilichomfanya twiga kuwa na miguu mirefu.
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,664

Umeshakuwa wimbo unaorudiwa mara kwa mara, na sasa unaonekana hauna washabiki tena, nashangaa wewe nawe unajaribu kuurudia. Vipi CUF, bado mmeungana na CCM kusimamisha mgombea mmoja Zanzibar mwaka 2015?
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,664
2,000
Habari ya sasa mujini ni meno ya tembo na meli ya kivita ya China
 
simbilisi

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
792
0
Watanzania wenzangu kwanza natoa salaam zangu za heri ya mwaka mpya.
Napenda kutumia jukwaa hili kutoa maoni yangu juu ya sakata hili lililopo mbele yetu kati ya Zitto na CHADEMA kwa ujumla wake.

Kwa ufupi ni kuwa sakata hili limetikisa chama na wanachama wake wote! na ukweli umejaribu kuwekwa hadharani na mwenye macho kaona mwenyewe na kusikia mwenyewe. Sasa kuendelea kutunishiana msuli huku kila mtu akitaka kuonesha ni nani zaidi, sioni kama ni jambo muafaka kwa sasa. Kuna haja ya kukaa chini kama binadamu na kuonyana na wale wote ambao wamekwenda kinyume na Katiba wakili na waombe msamaha.

Zitto wewe bado ni kijana mdogo sana na kete yako ya kufika mbali bado ipo wazi kabisa, hivi kama ni uongozi ni kitu gani kinachokusukuma kwa nguvu namna hiyo kana kwamba dunia inapinduka kesho na usipoongoza leo utakufa????!!
Je, ni wangapi ndani ya CCM waliambiwa kuwa hawana hadhi hata ya kuwa wajumbe wa nyumba kumi lakini leo ndio wanaotuongoza?

Je, umewahi kujitafakalisha ni jinsi gani walivyoamini kuwa bila Nyerere na Tanzania itakwisha lakini bado tunadunda ki mtindo?!

Je, kwa nini usivute subira na ukatumia muda mwingi kujenga matakwa yako kwa wananchi ambao sasa muda wao wa kushika hatamu unawadia (kwa mujibu wa Katiba mpya) ambapo tutakuwa na mandeti ya kuongozwa na tunaemtaka?

Mambo yapo mengi sana ya kuainisha katika kufikia mustakabali wa jambo hili, ila kwa ufupi tu naomba tuingie mwaka mpya kwa mambo mapya ya ujenzi wa chama kwa nguvu mpya.

Naomba Kamati kuu mtakapoingia kwenye kikao chenu hapo kesho kutwa isiwe ni kwa kumkamia Zitto, bali iwe ni jinsi gani ya kumtengeneza upya ahesabike kuwa mtoto ndani ya familia ya CDM.

Nawe Zitto, ukweli ni kuwa umekuwa na mambo mengi sana ambayo kwa macho hata ya upofu yanionesha kwenda kinyume na mipango mikakati ya chama, kama kweli unataka kubaki ndani ya CDM jifanye mdogo nasi tunaokuangalia tutakuinua hata kwa maombi yetu.

Je, nani angejua kuwa ipo siku moja sauti ya wanyonge itasimamam na kusema tunataka hili katika katiba yetu na likasikilizwa?! Je, mbona leo ipo hivo?

HIZI NDIO SALAAM ZANGU ZA MWAKA MPYA.

TAFAKARINI.

mbona haujatoa ushauri kwa mbowe kuhusu kufuja mali za chama, ruzuku na vimada?? au unataka CDM mwisho wake uwe m'baya

umejiona ulivyo?? mnafiki
 
Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,943
1,500
...mbona ishu ya zzk ishamalizika kitambo,kilichobaki ni maamuzi yake aende wapi,ccm(wazee wa fitina),cuf(wadini),nccr, au aanzishe chama chake...
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,532
2,000
Wanaomjadili Zitto na kuleta threads zinazomhusu ni wanaCCM. Tumjadili Zitto kwa lipi? Thithimwewe ndo wanaanzisha story zake ili kuchochea fujo na tushawastukia!
 
watundawangu

JF-Expert Member
Mar 26, 2011
250
170
Wanaomjadili Zitto na kuleta threads zinazomhusu ni wanaCCM. Tumjadili Zitto kwa lipi? Thithimwewe ndo wanaanzisha story zake ili kuchochea fujo na tushawastukia!

Kama ni hilo unalosema ni sahihi, basi wanachadema tunafarijika sana! Na kama hilo la Zitto halijafungwa, wanachadena wanaomba kamati kuu isitoe mwanya kuliendekeza hilo la ndugu Zitto. Zitto atoke au asitoke ndani ya Chadema, jambo hili lisipewe uzito (wache wafu wawazike wafu wao). Kuna agenda nyingi zenye umuhimu, kama hili la rasimu ya 2 ya katiba, chaguzi mbalimbali, zinazokuja, jinsi ya kuendeleza ujenzi wa chama vijiji na kujadili matatizo ya watanzania kwa ujumla.
 
umla

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
1,166
1,250
Wanaomjadili Zitto na kuleta threads zinazomhusu ni wanaCCM. Tumjadili Zitto kwa lipi? Thithimwewe ndo wanaanzisha story zake ili kuchochea fujo na tushawastukia!

Hili ndo gojwa lenu kubwa kuamini kila anaemsupport zitto ni ccm kwan zitto hana suport ndani ya chadema tumieni akili mtakuja shituka mmekwisha.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,413
2,000
Ya wasaliti yalishapitwa sahivi kwa CDM ni Chadema ni msingi
 
theROOM

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
946
250
Hili ndo gojwa lenu kubwa kuamini kila anaemsupport zitto ni ccm kwan zitto hana suport ndani ya chadema tumieni akili mtakuja shituka mmekwisha.

ZZK hana support yoyote CDM, yaani mtu mpaka magamba (Stella Mwampumba et al) ndio wanamuandalia press conference then unasema ana support CDM? Huoni ameitisha mikutano na Waha tu? ZZK hana issue tena, kwishney...

Tamaa, Kiburi, majivuno na dharau ni vitu vibaya sana maishani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom