Chadema:ni sahihi serikali kuingilia uhuru wa mahakama?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema:ni sahihi serikali kuingilia uhuru wa mahakama??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kulwa12, Nov 7, 2011.

 1. k

  kulwa12 Senior Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu leo jioni nimeona taarifa ya habari(i.t.v),viongozi wa wakuu wa chama chetu cha chadema wameitisha maandamano ya siku saba (usiku na mchana) ili kushinikiza serikali kumuachia huru mbuge wa arusha mh.lema.nimepata maswali yafatayo kutokana na tamko hili kwanza,je ni sahihi serikali kuingilia uhuru wa mahakama na kuamulu lema aachiwe huru??je tukipewa kuongoza serikali tutakua tunaingilia uhuru wa mahakama kwa kutoa executive order kama hivi kwa mahakama? Je hatuna imani na mahakama ya tanzania katika kutoa haki?,je tunakumbuka mda sio mrefu viongozi wetu walitoa pongezi kwa mahakama hihi kutoka na kutoa maamzi sahihi katika kesi ya madiwani wa arusha?.nahisi kunamambo yatafanya watu wenye busara na uwezo wa kutafakari kwa kina wawe na mashaka na uwezo wetu na ufahamu mzima wa utendaji wa MIHIMILI MITATU YA serikali.nasema tuwe makini sana sana.kama mwanasheria hili limenipa mashaka sana sana.
   
 2. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hii ndiyo Tanganyika ya leo utata mtupu wasomi wenyewe wanahaha kujua haki zao sisi wakulima sindiyo tutaozea jela.Naipenda chadema kwasababu inaniandalia maisha mazuri ya wajukuu zangu.
   
 3. j

  jigoku JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  mkuu kuwasifia Mahakama kwa jambo ambalo limeshafanyika na maamuzi yakafuata misingi ya haki sidhani kama kuna tatizo,na haimanishi leo ukifanya jambo zuri tukakusifia basi kesho ukifanya jambo la kijinga na lenye kudhulumu haki na msingi ya kiutendaji basi hatupaswi kusema ulichokikosea eti kwa vile jana ulifanya jambo jema,hiyo ni hali yakujinafikisha,mtu mkweli anakubali kile kilichobora na anakataa kilicho kibovu bila kificho.
  Na hapo utujuze wewe unadhani hata kama jambo limeamuriwa ki siasa ulitaka viongozi wetu wachekelee,kwani maamuzi gani unayoyaona mahakama imefanya sahihi kumunyima Mh Lema damana?ukumbukue mahakamani siku ya kwanza ya kesi hii ilitamkwa wazi kuwa dhamana iko wazi,leo kimeharibika nini tena kuzuia dhamana?au leo sio siku ya kazi?au Mh Lema amebadilishiwa kosa analotuhumiwa kiasi kwamba kesi hii inaonekana hatakiwi kupewa dhamana?au maamuzi ya mahakama yanatilewa kwa jinsi hakimu atakavyojisikia au kwa jinsi itakavyompendeza?
  Na sheria sio msahafu,wala Biblia,kuna sheria zingine zina mapungufu na zinzkandamiza na kuhusu suala la Arusha linataka tafakari ya kina,niliwahi kusema hapa,source ya uvunjifu wa amani na ukandamizwaji ni CCM kupoteza jimbo na hawako tayari kukubali wameshindwa na kwa vile wao wana dola.na rejea maneno ya mropkaji Nape ameshauhakikishia umma kwamba lazima watashinda kesi na watapiga kambi kwa ajili ya uchaguzi jimboni Arusha,hii ndo inadhihirika kwa kuhakikisha mbunge Lema anapewa usumbufu wa kila aina ikiwemo kubambikiwa kesi na kufanya maamuzi ya kibinafsi zaidi nje ya matakwa ya sheria.na hapa si kweli kwamba Mh Tundu Lisu hajui sheria ndogo tu ya mtuhumiwa kupewa dhamana au kutokupata dhamana,Je mwenzetu jambo hili unliangaliaje?
   
 4. k

  kulwa12 Senior Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu nashukuru sana kwa maelezo yako yakinifu,lakini bado hujajibu hoja yangu ya msingi,amabayo je ni sahihi kuishinikiza serikali iamulu mahakama ifanye nini juu ya suala hilo??je nasisi tikishika dola itakua sahihi kwetu kuiingilia mahakama ifanye maamzi kutokana na shinikizo la kisiasa? Mi nakubariana na yote uliosema kwa upande wa matatizo yaliopo na uonevu pia,ila sio sahihi kuiagiza serikali iingilie mahakama,mi nazani ingekuwa sahihi sisi kuidai mahakama haki yetu kama tumenyimwa na hata kutumia vyombo vya juu zaidi vya kimahakama kupata haki lakini sio kuiambia serikali iingilie.tunatoa picha gani?? Kuenel;eza utamaduni wa kuiingilia uhuru wa mahakama kuna madhara makubwa sana,na hata tukichukua zamana ya uongozi hili litakua kaa la moto kwetu tukifuga utamaduni huu.tuwe na fikira zaidi na tufikili kwa upana zaidi ya wapunzani wtu tutajijengea heshima zaidi.
   
 5. k

  kulwa12 Senior Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wenzangu hoja zikiwa wa moto tunakaa kimya,njia rahisi ya kushinda ni kukubali kujirekebisha katika mapungufu yetu.nawasilisha.
   
Loading...