johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,616
- 141,447
Kupanga ni kuchagua na mara zote umakini unahitajika sana.
Chadema inakwenda kwenye uchaguzi mkuu utakaompata Mwenyekiti na makamu wake pamoja na kamati nzima ya utendaji.
Miongoni mwa wagombea wa nafasi hizo ni mh Mbowe na wakili msomi Tundu Lisu bila kumsahau mh Mwambe.
Angalizo muhimu linawahusu wagombea wote watatu, tukianza na Mbowe yeye anakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani.
Kwa upande wa Tundu Lisu yuko nje ya nchi kwa matibabu ambako alienda na dereva wake kabisa.
Na huyu Cecil Mwambe yeye alishafunguliwa mlango wa ubunge kwa 2020 na mwenyekiti wa CCM taifa akiwa ziarani Masasi.
Tahadhari iliyopo Chadema inaweza kufika pahala ikawa haina mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa sababu za kimahakama na kimatibabu na ukitilia maanani uongozi wote wa juu wa Chadema wako mahakamani, hapo tutabakiwa na waandamizi wawili tu Sugu na Lema kuongoza jahazi ya Chadema.
Ni hayo machache
Maendeleo hayana vyama!