Chadema ni kama vile wanabet Mbowe yuko mahakamani na Tundu Lisu yupo uhamishoni wamebaki Sugu na Lema

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
32,582
2,000
Kupanga ni kuchagua na mara zote umakini unahitajika sana.

Chadema inakwenda kwenye uchaguzi mkuu utakaompata Mwenyekiti na makamu wake pamoja na kamati nzima ya utendaji.
Miongoni mwa wagombea wa nafasi hizo ni mh Mbowe na wakili msomi Tundu Lisu bila kumsahau mh Mwambe.

Angalizo muhimu linawahusu wagombea wote watatu, tukianza na Mbowe yeye anakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani.

Kwa upande wa Tundu Lisu yuko nje ya nchi kwa matibabu ambako alienda na dereva wake kabisa.

Na huyu Cecil Mwambe yeye alishafunguliwa mlango wa ubunge kwa 2020 na mwenyekiti wa CCM taifa akiwa ziarani Masasi.

Tahadhari iliyopo Chadema inaweza kufika pahala ikawa haina mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa sababu za kimahakama na kimatibabu na ukitilia maanani uongozi wote wa juu wa Chadema wako mahakamani, hapo tutabakiwa na waandamizi wawili tu Sugu na Lema kuongoza jahazi ya Chadema.

Ni hayo machache

Maendeleo hayana vyama!
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,033
2,000
Sipingani na wewe comrade but hapa chini ni muktadha kwa ajili ya thread yako hii....

wakati wa vita dhidi ya makaburu kule sauzi, viongozi wakuu wa ANC walikuwa wakiishi uhamishoni (particularly Tanzania na Zambia).
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,665
2,000
Kupanga ni kuchagua na mara zote umakini unahitajika sana.

Chadema inakwenda kwenye uchaguzi mkuu utakaompata Mwenyekiti na makamu wake pamoja na kamati nzima ya utendaji.
Miongoni mwa wagombea wa nafasi hizo ni mh Mbowe na wakili msomi Tundu Lisu bila kumsahau mh Mwambe.

Angalizo muhimu linawahusu wagombea wote watatu, tukianza na Mbowe yeye anakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani.

Kwa upande wa Tundu Lisu yuko nje ya nchi kwa matibabu ambako alienda na dereva wake kabisa.

Na huyu Cecil Mwambe yeye alishafunguliwa mlango wa ubunge kwa 2020 na mwenyekiti wa CCM taifa akiwa ziarani Masasi.

Tahadhari iliyopo Chadema inaweza kufika pahala ikawa haina mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa sababu za kimahakama na kimatibabu na ukitilia maanani uongozi wote wa juu wa Chadema wako mahakamani, hapo tutabakiwa na waandamizi wawili tu Sugu na Lema kuongoza jahazi ya Chadema.

Ni hayo machache

Maendeleo hayana vyama!
Ngoja nikuulize wewe Johnthebabtist, swali dogo tu, hivi unadhani ni nani wamesababisha huyo Mbowe kila siku anaenda mahakamani??

Ni nyinyi wanaccm kwa "kuliagiza" Jeshi letu la Polisi limbambikie kesi huyo Mbowe

Kwani nani asiyejua kuwa "waliompyupyu" Tundu Lissu hadi wakati huu alazimike kuishi uhamishoni ni nyinyi vigogo wa Chama tawala??
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,656
2,000
Usijali, chama kineza kuendeshwa kupitia mtandao wa WhatsApp, siku hizi WhatsApp inapokea nyaraka za aina zote, PDF, Powerpoint , voice note, hata group video calling inawezekana.
 
Oct 26, 2019
37
95
Mtoa post unacho kilenga ktk dhima yako ni sawa,

Chama kama chama ni lazima mjipange kukabiliana na wapinzani kuweka mipango thabiti kukifanya chama kisi yumbe

Kutokana na hali ilivyo kwa sasa mwambe angepaswa kupewa chansi ya kuwa m/k taifa
Kutokana na makesi yaliyo wajaa makamani akiwemo mbowe
Kwani kwa sasa chama kinaenda ktk uchaguzi mkuu kwa upande ule waweza fanya kama kamtego wanasubilia uchaguzi unakaribia Ndio wanatoa hukumu
Mfano kwa sasa kesi inayo mkabili mbowe inamashaidi zaidi ya kumi yeye ndie akiwa wakwanza kusikilizwa je wengine ni leo si hadi uchaguzi utafika

Kwa masilai mapana ya chama mwambe apewe um/k chama kitazame mbele ikumbukwe mizengwe yote ya upinzani wanayo fanyiwa ni man made
Na kama ni man made kuna time line na kama ni time line kila sekunde ina event yake
Bila shaka mm na wewe tutakuwamashuhuda endapo chama kisipo soma nyakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndammu

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
1,770
2,000
Wananchi wa ccm hameni huko mjiunge na chadema kwasababu raha ya kuijadili Ccm huko hampati uhuru lakini leo alhamdulillah mnaijadili chadema hamtekwi wala kunyanyaswa. Jaribu kwa Ccm utaozea jela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom