Zee la kitaa
JF-Expert Member
- Oct 25, 2017
- 403
- 211
Kwa hali ilivyosasa; inadhihirisha zaili kuwa Tanzania haina vyama imara vya upinzani vyenye ajenda ya kudumu katika kuleta mageuzi yenye neema kwa taifa hili. Jamii ya Watanzania wengi walijenga imani kubwa kwa chadema katika uchaguzi wa 2015; lakini wengi kwa sasa wanajutia kuipa imani kubwa chama kisicho na misingi iliyoimara. Kwa bahati mbaya chadema wameshindwa kujitambua kuwa wao ni chama kikuu cha upinzani Tanzania wanatakiwa kuweka mazingira ya kuchukua dola kwa kuongeza imani kwa watanzania waliowengi; ila kwa sasa wamebaki na porojo katika mitandao ya kijamii. Vijana wengi wa chadema wakiambiwa ukweli wanakimbilia kutukana bila kutafakari wapi chama kimejikwaa na nini wafanye.
Watanzania walio wengi wanatamani kuona vyama vinakuja na hoja za kuwaletea mabadiliko ya maendeleo na sio mabadiliko ya kuzungusha mikono. Kila wakati kupinga hata ambayo hayastahiri kupingwa; hivyo kuathiri imani ambayo watanzania wengi waliiweka kwa chama hiki. Viongozi mbalimbali kujiudhuru na kuachia nyazifa zao kunaonesha ni namna gani chama kimekosa dira ya kuimarisha mikakati ya kukieneza chama na kupata wanachama wengi zaidi.
Chama cha siasa ni wafuasi; kukimbia kwa wafuasi ni moja ya kiashiria kwamba kuna tatizo; lakini vijana wa chadema waburuzwa na hisia eti wanachama wao wananunuliwa. Chadema kimekuwa chama cha kiwanaharakati kuliko uhalisia nini wananchi wanataka. Watanzania wachache sana hususani walioko katika mitandao ya kijamii tena na wao sio wote wanaopenda siasa za kiuwanaharakati. Ni wakati chadema mkajitambua; mkaacha matusi, mkaelezena ukweli na kukijenga chama chenu; la sivyo mtabaki na ajenda za maandamano na mkaandamana bila mafanikio. All the best.