Chadema ni chama cha SIASA............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema ni chama cha SIASA.............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Nov 25, 2010.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu zanguni wanaJF especialo ma - great thinkers.

  Kuna swala moja linanisumbua sana naomba ufafanuzi nadhani pengine kuna kitu kina miss ndani ya chadema. Nimekuwa kwa mfano nimekuwa nikititatizwa na mfumo wa demokrasia kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali hususan za "viti maalum" ambapo hakukuwa na demokrasia ila kupewa mtu jukumu la kuwateua wawakilishi kupitia kapu la "viti maalum" nadhani tafsiri ya viti maalum pengine kina mhe Mkumbo wanatumia nafasi hizi maalumu kuwapa watu maalum ndani ya chama. Wote tunawafahamu wanamama maalum ndani ya Chadema ambao ni aghalabu kukosa nafasi hizo "maalum" maana wao ni "maalum" ndani ya chama. Na ni Chadema pekee ndio kina record ya kuingiza Bungeni Baba, mtoto na mkwe kwenye bunge japo baba anapambana kuingia bungeni lakini mtoto na mkwe wamehakikishiwa nafasi hiyo au pengine "bila kupingwa".

  Nayasema hayo yote ili tuache unafiki! unafiki unakiua chama angalie unafiki unaofanywa na chama tawala oneni hasira za wananchi kwenye uchaguzi uliomalizika. Hayo mafanikio yaliokipata Chadema yametokana na unafiki ndani ya CCM na taratibu za kupendeleana. Sote mashahidi tumeona yaliyomkuta Mwakalabela na Bashe wapo wengi lakini huo ni mfano tu ambao kwa kiasi kikubwa umeweza kunufaisha Chadema. Sipendi Chadema ifate mule ambapo CCM imepita. Napenda kuona Chadema kinakuwa chama imara na kimbilio la wanyonge maana juu ya ukweli kwamba CCM imebakiwa na watu wachache wenye uchungu ( na hii ni kutokana na kuwa hakuna chama mbadala ) Chadema kinatakiwa kionyeshe kuwa kinaweza kuwa chama mbadala kiache baadhi ya mambo yake ambayo yamejengeka kama mazowea.

  Hakuna budi ukafika wakati kujenga viongozi wawe wanasiasa wenye ueledi wa siasa maana tatizo jingine kubwa ndani ya Chadema hakuna wanasiasa na kama wapo basi wa kuhesabika. Wengi wao ni wanaharakati. Tofauti yao ni kuwa wanaharakati wao wanapohitajia kitu hutumia njia za kugoma na kulazimisha ( mfano wakitaka mvua inyeshe basi hata kama hakuna wingu ni lazima inyeshe ) hawawezi kusubiri wingu ili mvua inyeshe lakini wanasiasa wao mara nyingi wanaendesha mambo kidiplomasia zaidi wanafuata process mpaka azma yao inafanikiwa. Ndani ya Chadema tumewashuhudia wanasiasa wanapotoa mawazo yao au wakifanya jambo linavyochukuliwa kwa hisia tofauti na baadhi ya viongozi ambao ni wanaharakati na wamewalisha wanachama kasumba sawia na yao. Utaaona kuwa mwasiasa Zitto Kabwe anavyosakamwa kwa baadhi ya mambo anayoyafanya au mwasiasa John Shibuda anavyotolewa maneno mabaya kwa kusalimiana na Rais! Nina uhakika ndani ya CCM kuna wanaotofautiana mambo na chama chao na hili hupelekea siri nyingi za vikao kuvuja jambo ambalo hapo zamani ilikuwa ni aghalabu kutokea. Hii ina maana kila mtu ana mawazo yake na lazima yaheshimiwe.

  Kwa kumalizia napenda kusema Chadema kiwaachie harakati makundi ya kijamii wao wajikite kwenye kukuza chama na kuikalia serikali kooni bungeni ili iweze kuleta tija kwenye majimbo na Tanzania kwa ujumla. Haya ni maoni yangu na kwa kutambua uhuru nategemea kila mmoja wetu atoe maoni yake kwa ajili ya kujenga chama wakati umefika tusisubiri kutokee matatizo ndio tutoe maoni yetu.   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  crap of the day
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo Mkuu watu hawachangii post zako kwa sababu zimejaa Propaganda na Provocative Language, Ku duplicate Topic zako wala hakutadraw attention za Watu Makini humu Jamvini
   
 4. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Wewe na Malaria Sugu ni mapacha tena identical
   
 5. A

  Awo JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 793
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  As far as I am concerned you are supposed to be "dead" as you are already kneeling down!! Umeng'ang'ania sana viti maalum vya CHADEMA. Umeelezwa utaratibu uliotumika ulikubaliwa kwenye vikao halali, lakini mwenzetu hutaki kuelewa, umeng'ang'ania tu kupiga magoti na kufa hutaki!
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Imefikia kipindi post ikirushwa tu anaangaliwa aliyeanzisha.
  "kumbe sokomoko! aah! kumbe Malaria sugu!!"
  inapotezewa.
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimependezwa na Calmness ya Viongozi wa CHADEMA, inawaumiza sana CCM hawajui CHADEMA watakuja Kivipi so wanakuja hapa na Kutoa Provocative Language ili wajue ni nini hasa Msimamo na next Move ya CHADEMA

  Ufupi ni kwamba wana KIHORO
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Duh, kwa vile unapenda kuuliza the swali lile lile basi majibu utapata mengi na tofauti, ( The same question which was asked last year if repeated this year may have completely different answers - By Albert Einstein)

  Kwanza, kama ulifuatilia toka mwanzo jinsi uchaguzi ulivyoanza kulikuwa na mamluki ndani ya vikao vyao waliokuwa wamepandikizwa, Pili kulikuwa na mvutano kidogo katika namna ya kupata hivyo viti maalumu kwa hiyo kamati kuu ya chama ikakaa na kupendekeza namna nyingine ya kuwapata. Kwa hiyo mwisho wa siku ndo ikawa imependekezwa hiyo njia ambayo wajumbe walikubaliana.

  Hata hivyo mkuu, ukifuatilia saaana unaweza kupata mchele na pumba sasa ni juu yako kuchukua unachotaka.
   
 9. b

  bojuka Senior Member

  #9
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaaandika vitu gani ?
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu......
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haijalishi nitasema sitanyamaza kwakuwa mimi ni mtu huru na nina uhuru wa kutoa maoni yangu, kama wewe unavyotoa maoni yako kwa kunifananisha mimi na malaria sugu. Ila ukweli utabaki palepale.......
   
 12. g

  gomezirichard Member

  #12
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hujakatazwa kusema ila angalia mambo ya kusema wakati mwingine sokomoko

  mzee gomezi
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Duuh umejitahidi lakini hakuna tija kwenye waraka wako huo tunataka ushauri wa kujenga sio kila wakati unazusha udhaifu tuu
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  uhuru lazima uwe na mipaka
   
 15. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa maana hiyo mwataka kutuambia kuwa hii JF ni ya viongozi wa CHADEMA ?, kama iko hivyo basi tumepoteza mwelekeo wetu aisee. Sie kama GREAT THINKERS hatutakiwi ku-base upande wowote ule, tuwe tuna analyse na kutoa maoni yenu for the betterment ya watanzania wote bila kujali chama, dini, rangi, kabila au mkoa.
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  je wale viti maalum wa kwenu ccm ambao mmewabana mpaka asasi za kiraia kwa kumpitisha rit malaki na anna abdallah ilihali hat siku moja hatujawahi kuwasiki wakifanya lolote katika assi za kiraiana wafanyakazi mmepitisha mtoto wa kawawa ambaye hajawahi kuwa kiongozi wa tucta, mbona huulizi hayo?
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tuliisha tambua CHADEMA tangu zamani. CHADEMA kuna UDINI, UKABILA, UPENDELEO WA WAZI WAZI KM VITI MAALUM WALIVYOFANYA NA HAKUNA UHURU WA MAWAZO KM WANAVYOTAKA KUFANYA WAKINA ZITTO NA SHIBUDA
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Hivi kumbe Chadema ndiyo kile chama kimeahidi kuanzisha Mahakama ya Kadhi na kuisilimisha nchi kwa kuingiza OIC? Aisee nilikuwa sijui kama ni hivyo kweli Chadema kuna udini.
   
 19. Mpelijr

  Mpelijr Member

  #19
  Nov 25, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Hahahhahaahah jamani hizi ni siasa za kuibomoa chadema au?
   
 20. D

  DENYO JF-Expert Member

  #20
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sokomoko huna nafasi hapa jamvini unatia kichefuchefu kajadilianeni na makamba hapa ni forum ya wanamapinduzi watanzania waliobahatika kusoma wanapashana habari na kujua namna gani wasonge mbele nenda kwa mkwere akakwere au kwa makamba aliyekutuma chukua time
   
Loading...