Elections 2010 Chadema ni chama cha kitaifa

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
147
Kwa idadi ya viti vilivyochukuliwa na CHADEMA mpaka sasa kwenye uchaguzi mkuu 2010 na kwa kura za uraisi atakazopata Dk.Slaa nina matumaini CHADEMA wataongeza wabunge wengi wa viti maalum na hivyo CHADEMA kuwa na wabunge wengi katika bunge lijalo la 2010 - 2015.

Mimi nawashukuru sana CHADEMA chini ya MBOWE,ARFI,SLAA,ZITTO ,MNYIKA,wabunge wa bunge lililopita na wanachama wote wa CHADEMA kwa kufanikiwa kukiuza chama kwa wananchi na wananchi kuweza kukikubali CHADEMA na kuwa chama KIKUU cha USHINDANI Tanzania.

Kwa viti vya Ubunge na Udiwani ilivyopata hadi sasa katika uchaguzi mkuu 2010 wa Tanzania,CHADEMA imeweza kufuta ule UVUMI uliokuwa ukienezwa na CCM kuwa ni chama cha kikabila.

Mimi nasema hivi CHADEMA SIO chama cha kikabila BALI ni chama cha Umma wa KITANZANIA kinachoamini katika Nguvu ya umma.

Kwa mujibu wa matokeo mpaka naandika thread hii CHADEMA imeweza kupata viti vya Ubunge katika mikoa ifuatayo

ARUSHA,MWANZA,DAR ES SALAAM,RUKWA,RUVUMA ,SHINYANGA,KILIMANJARO,KAGERA,KIGOMA,MBEYA ,MOROGORO na IRINGA.Hii ni mikoa ya Kanda zote za Tanzania isipokuwa kanda ya kati na Visiwani Zanzibar.

CHADEMA NI CHAMA CHA KITAIFA NA WALA SIO CHAMA CHA UPANDE MMOJA TU WA KASKAZINI.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI CHADEMA,MUNGU WABARIKI WATANZANIA WAENDELEE KUISUPPORT CHADEMA.AMEN
 
Waliokuwa wanasema vingine walikuwa na lao jambo na walifanya hivyo kuhofia nguvu za hoja zake wakati wao hawana hoja bali ile ya kuwaibia na kuwafukarisha Watanzania. Mapambano sasa yanaendelea kukiimarisha katika kila wilaya na mkoa.
 
Huu ni mwanzo tuu, tunawasihi sana ndugu zetu mliopewa dhamana ya kutuwakilisha msimu huu mkaongeze chachu ya kweli, tunaamini kabisa kuwa CHADEMA itakuwa na wawakilishi katika kila mkoa wa Tanzania Bara na visiwani msimu ujao. Sisi tuko nyuma yenu. Jipangeni na msiende tusaliti tafadhali.
 
ukitaka kuona ukabila angalia majina ya wale watakaoteuliwa viti vya wanawake. kura zivunwe mbeya kigoma mwanza iringa lakini ubunge kilimanjaro na arusha
 
Mimi nasema hivi CHADEMA SIO chama cha kikabila BALI ni chama cha Umma wa KITANZANIA kinachoamini katika Nguvu ya umma.

Hizi ni propoganda chafu za CCM ambayo imefilisika kisiasa na kiitikadi kabisa
 
wamesema vyema
msijidanganye hamna chama chenye ukabila bali undugu
hata wewe ukipata ulaji una kula kwanza na ndugu au washikaji
 
Back
Top Bottom