CHADEMA ni chama bora kuliko ACT-wazalendo na CCM (mkubwa na mwanae)

Mhere Mwita

Verified Member
Jan 24, 2012
234
1,000
Leo nimeamua kuwajibu Wana ACT-Wazalendo ambao wanasema chama chao ni chama bora na kina viongozi makini kuliko vyama vyote vya upinzani ndio maana Magufuri ameamua kuwa anachukua kwao.

Hoja hii ni ya kitoto kabisa kwa hawa wanaojiita makini na waadilifu, katika uchunguzi Wangu Wa kisayansi umenionesha kuwa Chadema ndio chama kina watu makini kuliko ACT- Wazalendo na CCM.

Tunayo mifano hai mingi tu ambayo inaweza kuthibitisha kuwa Chadema ni chama bora kuliko (Mkubwa na Mwanae) yaani ccm na ACT- Wazalendo hapa nitaiweka mifano michache tu ili nisiwachoshe wasomaji.

1)- Mfano Wa kwanza Mama Anna Mughwira alishindwa kwenye kura za Maoni za Ubunge Mwaka 2012 Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mdogo na mwaka 2014 alishindwa uwenyekiti Wa Bawacha mkoa Wa Singida.

Kwa ACT Wazalendo akawa Mwenyekiti Wa chama taifa na mgombea Urais kwa kupitia chama hicho, kwa ccm amekuwa Mkuu Wa mkoa Wa Kilimanjaro.

2)- Samson Mwigamba, Chadema alikuwa Mwenyekiti Wa chadema mkoa Wa Arusha, ACT Wazalendo amekuwa Katibu mkuu Wa chama taifa sasa ni kaimu kiongozi mkuu wa chama.

3)-Prof Kitila Nkumbo, Chadema amekuwa mjumbe Wa kamati kuu, ndani ya ACT Wazalendo amekuwa Mshauri mkuu Wa chama na ndani ya serikali ya ccm amekuwa Katibu mkuu Wa wizara.

Kwa mifano hiyo michache japo ipo mingi inaonyesha Chadema ni chama Bora, ili waweze kuelewa vizuri mchezaji ambae yuko Bench Real Madrid ukimleta simba au yanga lazima awe first Eleven.

Lakini mchezaji Bora Wa simba au Yanga akienda Madrid anaenda kukaa Bench kwa sababu Madrid ni team Bora inawachezaji bora wengi.

Kwa maana hiyo Chadema ni kama Real Madrid waliobench kwenu ndio wachezaji bora. Na ukiangalia kwa umakini viongozi hao wamelelewa na chadema, kwa maana hiyo chadema ni Mwalimu kwao je unaweza ukawa bora kuliko Mwalimu?

Ni Mimi Mhere Mwita
 
Marlex Jr El

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
1,759
2,000
Viongozi wengi wa chadema sina mashaka nao isipokuwa mbowe sijawahi muamini sijui ni kwann?
 
nanjinji

Senior Member
Mar 23, 2017
151
250
Mkuu hao viongozi au wanachama wa ACT ambao unawajibu walikuuliza humu..?
mada zingine hizi wajibu huko huko facebook
 
babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,367
2,000
Leo nimeamua kuwajibu Wana ACT-Wazalendo ambao wanasema chama chao ni chama bora na kina viongozi makini kuliko vyama vyote vya upinzani ndio maana Magufuri ameamua kuwa anachukua kwao.

Hoja hii ni ya kitoto kabisa kwa hawa wanaojiita makini na waadilifu, katika uchunguzi Wangu Wa kisayansi umenionesha kuwa Chadema ndio chama kina watu makini kuliko ACT- Wazalendo na CCM.

Tunayo mifano hai mingi tu ambayo inaweza kuthibitisha kuwa Chadema ni chama bora kuliko (Mkubwa na Mwanae) yaani ccm na ACT- Wazalendo hapa nitaiweka mifano michache tu ili nisiwachoshe wasomaji.

1)- Mfano Wa kwanza Mama Anna Mughwira alishindwa kwenye kura za Maoni za Ubunge Mwaka 2012 Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mdogo na mwaka 2014 alishindwa uwenyekiti Wa Bawacha mkoa Wa Singida.

Kwa ACT Wazalendo akawa Mwenyekiti Wa chama taifa na mgombea Urais kwa kupitia chama hicho, kwa ccm amekuwa Mkuu Wa mkoa Wa Kilimanjaro.

2)- Samson Mwigamba, Chadema alikuwa Mwenyekiti Wa chadema mkoa Wa Arusha, ACT Wazalendo amekuwa Katibu mkuu Wa chama taifa sasa ni kaimu kiongozi mkuu wa chama.

3)-Prof Kitila Nkumbo, Chadema amekuwa mjumbe Wa kamati kuu, ndani ya ACT Wazalendo amekuwa Mshauri mkuu Wa chama na ndani ya serikali ya ccm amekuwa Katibu mkuu Wa wizara.

Kwa mifano hiyo michache japo ipo mingi inaonyesha Chadema ni chama Bora, ili waweze kuelewa vizuri mchezaji ambae yuko Bench Real Madrid ukimleta simba au yanga lazima awe first Eleven.

Lakini mchezaji Bora Wa simba au Yanga akienda Madrid anaenda kukaa Bench kwa sababu Madrid ni team Bora inawachezaji bora wengi.

Kwa maana hiyo Chadema ni kama Real Madrid waliobench kwenu ndio wachezaji bora. Na ukiangalia kwa umakini viongozi hao wamelelewa na chadema, kwa maana hiyo chadema ni Mwalimu kwao je unaweza ukawa bora kuliko Mwalimu?

Ni Mimi Mhere Mwita
Hapo umedhihirisha kuwa cdm ni chama cha wasiojitambua na kutambua vipaji na uwezo wa wengine.
Wale mliowadharau leo wamethibitisha kuwa cdm ni makanjanja.

Baada ya kuona mliowapuuza wanafanikiwa mmeshindwa kuvumilia kutwa kucha kwenye mitandao kupooza maumivu yenu.
JINYONGENI KWA MAKAMASI
 
Alfan issa

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,153
2,000
Hivyo tujifanye hatujui sheria?
Mnajua sasa! Mngejuwa mngefungiwa umeona ee, waongezee na big g ili wajinyonge vizur
Hapo umedhihirisha kuwa cdm ni chama cha wasiojitambua na kutambua vipaji na uwezo wa wengine.
Wale mliowadharau leo wamethibitisha kuwa cdm ni makanjanja.

Baada ya kuona mliowapuuza wanafanikiwa mmeshindwa kuvumilia kutwa kucha kwenye mitandao kupooza maumivu yenu.
JINYONGENI KWA MAKAMASI
 
Makusudically

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
2,203
2,000
Mhere Mwita umechemka kabisa ktk kujibu hoja hii, ni bora hata ungenyamaza tu, ACT imeanzishwa miaka mingapi? ACT imeshika nafasi ya Tatu ktk uchaguzi Mkuu baada ya kushiriki mara ngapi ktk chaguzi? ACT imepata kuungwa mkono na Viongozi wa Kitaifa hususan viongozi walioko madarakani mara nyingi kuliko hiyo Chadema ambayo omejizolea umaarufu kwa kufanya "fujo, kutukana viongozi, kutoa lugha za kubeza vyam vingine kama pale Chadema ilipokituhumu CUF kuwa ni CCM B, CUF ni mashoga , maneno ambayo hayastahili kutamkwa na viongozi ambao wanatoka chama kikuu cha upinzani. Chadema kinaongoza kwa kuburuza wabunge wake kwa nguvu na wakati mwingine kuwalazimisha kutoka bu geni ili kuwakosesha fursa ya kuwawakilisha Wananchi waliowachagua kama tulivyoona hivi karibuni, ambapo Mbunge wa Chadema alifanya kitendo cha AIBU kubwa na hakijawahi kufanyika kokote ktk mabunge ya Afrika, Cha mbunge kuwalazimisha kwa nguvu wabunge wa chama chake kutoka nje ya Bunge. ACT ni chama bora kabisa cha Upinzani kuwa kutokea Tanzania na Afrika Mashariki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom