CHADEMA ndicho chama makini kilichobaki Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ndicho chama makini kilichobaki Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkondakaiye, Jan 6, 2012.

 1. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika vyama vya siasa vilivyopo hapa Tanzania CDM ndicho chama pekee kilichobaki kuwa chama makini na kinachoshughulika na matatizo ya watanzania kwa sababu zifuatazo:
  1. CDM Toka uchaguzi umalizike wamekuwa msitari wa mbele kupigania haki za wananchi na kuibana serikali kwa kusababisha uchumi wa Tanzania kushuka na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu. Na hata ilipofukuza wanachama hakuna malalamiko yaliyotolewa.
  2. CCM wao toka uchaguzi umalizike wamekalia kulalama kuvuana magamba ambayo yameshindikana kuto na huku wananchi wakiumia na hali ngumu ya uchumi na wala hawajali.
  3. NCCR-MAGEUZI na CUF Toka uchaguzi uishe wamebaki kuwatukana CDM kwa kufadhiliwa na CCM na wananchi kuwaita CCM B na laana iliyowapata wameanza kufukuzana.
  4. TLP na UDP Toka uchaguzi umalizike wamejikita kutafuta maslahi yao binafsi huku wakiunga mkono CCM na kuacha kutetea wananchi
  5. Vyama vingine ni vya musimu wakati wa uchaguzi kuitibulia CDM

  CDM kazeni buti, Msikae mjini nendeni vijijini mkawaamushe watu waliolala ili magamba wasiwaibie kura tena.

  Tujadili
   
 2. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Maelezo yako, yako wazi ni ukweli mtupu na iyo haina mjadala ivyo basi tushikamane dumu na chadema yetu, mpaka 2015 na kuendelea ili tuwasurprise magamba, mafisadi wa ccm na washirika wao inshallah
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Haikuwahi tokea chama kingine tofauti na CDM kikawa makini.
  Labda unikumbushe lini CCM au CCB-B vilikuwa makini?
   
 4. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Akijawai na hakita wai ni chama cha machumia tumbo
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Ebu ngoja tuangalie sifa za chama makini Chadema.

  1. Chadema inawalazimisha wabunge wake kususia mijadala ndani ya Katiba.

  2. Chadema haikujali kwamba wabunge hao hawakufikishwa bungeni kwa kadi za Chadema bali kwa kura za wapigakura.

  3. Chadema waliwafukuza kwa nguvu Madiwani wake ambao ni wawakilishi halali wa wananchi.

  5. Chadema wanataka kutuendesha wananchi kama maroboti, ndio maana wanatarajia kuungwa mkono kirahisi watakopoanza kuuza siasa nyepesi za kuwataka Watanzania wasusie mjadala wa katiba.

  6.Narudia kusema tena Chadema, Wananchi sio misukule kiasi cha kuburuzwa kirahisi kwani wanajua kupembua kati ya dhamira njema na dhamira mbaya.

  Hizo ni baadhi ya sifa za chama makini Chadema
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nitarejea baadae kaa mkao wa kula Mkondakaiye.
   
 7. K

  KIROJO Senior Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo Ndo naona sasa wewe Ritz ni fake kwelikweli ,hayo yote unayajua mwenyewe pia ,wewe ni Gamba kweli hujuwi kucompare na contrast ,hayo ni negativity zako juu ya CDM huijuwi CDM na usomi Katika yake.Unaendesha ushabiki tu ambao hauna jipya zaidi ya kutunga vitu vya upande mmoja au ndo wewe uliyepoteza kiti cha uchanguzi 2011 kwa CDM nini?
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Nakwenda kukusanya data za chama makini Chadema tarudi kuziweka humu jamvini tuwe na subira.
   
 9. K

  KIROJO Senior Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  leta data na usichakachuwe hizo data tutakuona wewe ndo unayeleta mambo bila ushahidi
   
 10. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  1. CCM inawalazimisha wabunge wake kuunga mkono hoja za kimasabuli.
  2. Bila kuwa mwanachama wa chama chochote huwezi kupitishwa kuwa mgombea kupitia chama hicho
  3. Walifukuzwa lakini hakuna wananchi waliolalamika. ona kafulila na HR watu wanavyolalamika.
  4. Watanaznia ni watu wenye akili, siasa za zidumu fikira za mwenyekiti unazotaka kuziendeleza zimepitwa na wakati.
  5. Watanzania sio misukule unatakiwa uwaombe radhi.

  Kwajinsi usivyo makini hata kuhesabu hujui. ona ulivyopanga umasabuli hapo juu
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mkondakaiye,

  Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa hili iweze kukabiliana na chanagamoto za karne ya 21 bahati mbaya mpaka sasa hakuna chama chochote cha siasa ambacho kimejipanga kimkakati kuwakomboa waTanzania dhidi ya madui wanne wakubwa UJINGA,UMASIKINI,MARADHI na UFISADI.Narudia tena vyama vyote vimejikita zaidi kupata madaraka lakini havina ajenda ya maana ya kuondokana na hao maadui watatu wakubwa.
   
 12. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nithibitishie, isije kuwa unatumia kauli ya samaki mmoja akioza wote wameoza.
   
 13. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Adui namba nne ni CCM ufisadi ni chembe tu ktk adui CCM. Bado kuna undugunization,udinization,ukoonization,urithinization nk
   
 14. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  A plan is not a litany of complaints...
  Ikiwa Chadema kazi yake kubwa ni kubwabwaja tu..then it is a useless party..

  Ndio maana wenzenu waligundua hili kule Zanzibar, wakaona hawawezi kuwaambia wananchi same stories everyday..
  malalamiko.. malalamiko..malalamiko..
  Huwezi kujenga nchi kwa kulalamika tuu..

  Wananchi wanahitaji maendeleo sio MAANDAMANO!

  Sijuwi umakini wa Chadema una upimaje?
  1. Chama ni NGO ya watu wachache wa Kaskazini
  2. Inaendeshwa kama family property
  3. Iko religiously polarized..
  4. Haina national agenda..bali ni Zonal agenda..
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  CHADEMA pekee ndiyo yenye uthubutu wa kupambana na hao maadui watatu nchi hii. Hebu wapeni nafasi ya kuongoza nchi.
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hofu yangu ni kwamba pindi CHADEMA watakapochukua utawala wa nchi hii, hakutakuwa na chama makini cha upinzani, kwani wakati huo CCM na wakala wake watakuwa wamezikwa.
   
 17. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wameiga sasa wametepeta....tulienda ikulu wakapiga copy..tukawatimua wanachama ambao sio waaminifu sasa wameiga wamepotea vibaya..big up chadema sasa tusonge mbele kwa kasi ....watakuwa wamejifunza hawataiga tena...tunawategemea mtakuja na mbinu kabambe itakayotusaidie tutoke hapa tulipo..viva chadema
   
 18. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Sina la zaidi la kusema,kwani matendo ya CHADEMA yanasema yenyewe na wananchi wanaona!CCM wapo Ikulu,lakini Dr Slaa na CHADEMA wapo mioyoni mwa watanzania wengi!
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Maneno yako nimeyakubali kabisa mkuu .Idumu Chadema
   
 20. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Yaah,umeongea jambo la msingi mno!Unapendekeza nini mkuu?
   
Loading...