CHADEMA, NCCR kwa hali hii hamjengi Viongozi kuwa na madaraka zaidi ya moja mnakuwa mnafanana na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, NCCR kwa hali hii hamjengi Viongozi kuwa na madaraka zaidi ya moja mnakuwa mnafanana na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Jan 13, 2012.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Hi wakuu.

  Suala la kiongozi mmoja kulundikiwa vyeo, kiasi kwamba anapotakiwa kuhudhuria mialiko sehemu tofauti tofauti inakuwa ngumu kwake kuhudhuria na hivyo kutuma mwakilishi, limekuwa sugu hapa nchini. Kwa mda mrefu, tumekuwa tukijadili kwa mda mrefu kuwa tunahitaji watu wawajibikaji, sio wasaini posho pekee tu.

  Kwa mda mrefu na nyakati tofauti, viongozi na wapenzi wa vyama vya upinzani na mimi nikiwemo, tumekuwa tukipinga suala la mtu kuhodhi madaraka tofauti, na hivyo kuwa na nafasi nyingi, kitu kinachopunguza utendaji na uwajibikaji wao.

  Tumepinga kitendo cha mtu kuwa mbunge, halafu anapewa ukuu wa wilaya/mkoa, tumepinga tabia hiyo na vyama vyetu vimekuwa vikilisemea hilo.

  Ezekiel Wenje na Moses Machali, ni wabunge, wanaotakiwa kuwatumikia wananchi kwa nafasi waliyonayo. Kitendo cha vyama vyao kuwateua na kuwapa nafasi nyingine ndani ya chama, ni udhaifu wa wateuaji na kuendeleza anacho kifanya mkuu wa kaya kuwateua rafiki zake kushika nyazifa mbalimbali ili hali tayari wana majuku mengine.

  Kwa kuwa kuna watu waligombea nafasi mbalimbali hasa ubunge na wananchi wengi wakaonesha kuwa na imani nao, ni mda sasa wa kuwazoesha na kuwapa CV kuwaandaa kuingia 2015, wapewe nafasi hizo ambazo wabunge hawa kina zitto, mnyika, wenje, machali na wengine wamejilimbikizia.

  Kukubali kuzitumikia nafasi hiyo, ni ishara ya UCHU WA MADARAKA, AMBAYO WANAIONESHA WAKATI HAWAJAPEWA NCHI, WAKIPEWA NCHI, HALI ITAKUWA MBAYA ZAIDI KULIKO HATA CCM WANAVYAFANYA LEO.

  Kwa pamoja tuwakemee waache hulka hiyo ya kujilimbikizia kazi kama vitenzi vya kiswahili

   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Aaah! huo ni mtazamo wako potezea
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ni sahihi kabisa, ni mtazamo wangu wewe mtazamo wako ni upi?
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Thanks in advance mode, mmeiweka vizuri
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  hivi hamnaga kazi ya kufanya! kila dakika chadema,chadema.
   
 6. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hoja za kuokoteza hizo. Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa chama ni vyema akawa mbunge. Ufanisi wa kazi yake unategemewa kukifaidisha chama bungeni pia. Sasa sidhani kama kumchagua mtu toka mtaani ambaye haingii bungeni kama kutakuwa na manufaa kama ambayo yanapatikana kwa mkurugenzi akiwa mbunge pia.

  Naikupe mfano wa migongano ya kauli ndani ya chama chenu cha CCM kati ya NAPE na wabunge wa CCM. Hii ni sbb ya kutokuwa na mjumuisho wa majukumu. Sikatai kuwa ni kweli kuna umuhimu wa kugawana majukumu, lkn tunapaswa pia kuangalia ni majukumu yepi tunayozungumzia. Huyu Wenje tayari ana Diplomatic Passport na uelewa wa shughuli za bunge, kwa hiyo naamini ni msemaji mzuri wa chama nje ya mipaka yetu zaidi ya asiyeshiriki shughuli za bunge.
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Ok haiko mbaya chagua wewe unataka cheo kipi?
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  hata wewe umedhihirisha ulichokiandika, eti chadema, chadema
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Kwani katiba inaruhusu kumteua yeyote ndani ya chama na kumpa cheo cha kiserikali?
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  haya naunga mkono hoja kwa huyu wenje, je mnyika, zitto, nafasi wanazomiliki, zinawafaa wao pekee tu? Wengine hasa wale walioshiriki kuwania ubunge wakashindwa kwa hila za ccm hawawezi kupewa nafasi hizo ili wazitumie kujenga chama katika maeneo yao?
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Kwa CCM inaruhusu, na mifano ipo mingi, lakini kwa wanamapinduzi inakuwa aibu kuzomea CCM wakati na wewe unafanya hivyohivyo. watanue wigo
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  mtanzania/mtanganyika vyeo.
   
 13. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja, ni hoja yenye mashiko. Hivi ni kwa nini watu warundikiwe vyeo wakati kuna wengine wanaweza kufanya kazi hizo tena kwa ufanisi. Suala hili halipo tu kwenye vyama vya siasa lakini pia serikalini. Kila siku, hakuna ajira wakati mtumishi mmoja ana vyeo vinne au vitano kwa wakati mmoja.

  Tubadilike kuanzia leo kwa kujiraumu kwanini hatukubadilika jana. Suala hili ni muhimu na wala lisiusishwe na siasa maana ni ufa kati ya nyufa tulizonazo.
   
 14. d

  davidie JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cheo sio zawadi bali ni uwezo wa kiutendaji na wala cheo sio nguo kwamba ngoja niijaribu kama hainitoshi nitaivua
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  MKUU humu ndani, ukisoma btn the line WASHABIKI=WABOMOAJI utawajua, na WAPENZI=WAJENGAJI UTAWAJUA. AKSANTE KWA KULIONA HILI
   
 16. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Umetafakari kabla hujaandika au umeandika tu? Unaweza kutoa mifano ya watu wenye utitiri wa vyeo na kuchambua utendaji wao? acha ushabiki, jibu kwa kujenga mkuu
   
Loading...