Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,162
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
KURUGENZI YA BUNGE NA HALIMASHAURI.
TAMKO KUHUSU ZOEZI LA UCHUKUAJI WA FOMU ZA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
KURUGENZI YA BUNGE NA HALIMASHAURI.
TAMKO KUHUSU ZOEZI LA UCHUKUAJI WA FOMU ZA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Itakumbukwa kuwa kuna mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unaendelea ndani ya vyama vya Siasa .
CHADEMA tunapenda kuutangazia Umma wa wanachama wa CHADEMA kuwa mchakato huo umeanza rasmi leo ndani ya chama na kila mwanachama wa CHADEMA ambaye anasifa zinazostahili anatakiwa kuchukua fomu kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa chama .
Masharti kwa wagombea ni kama ifuatavyo;
1. Awe ni Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba na sheria za Bunge la Jamhuri ya Muungano.
3. Awe mwanachama wa CHADEMA .
4. Awe mtu mwenye mwenendo na maadili mema ndani ya jamii .
Gharama ya fomu hizo ni shilingi elfu hamsini tuu.
Zoezi la uchukuaji fomu linaendelea na mwisho wa kurejesha fomu hizo ni siku ya Jumatano tarehe 10/11/2010 saa kumi kamili jioni ofisi ya Katibu Mkuu.
Nawatakia kila la kheri katika zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo.
Imetolewa na ,
John Mrema .
Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri