CHADEMA nao wamshupalia Makamba kuhusu uchochezi

  • Thread starter Chadema Diaspora
  • Start date

Chadema Diaspora

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Messages
479
Likes
220
Points
60
Age
30
Chadema Diaspora

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2010
479 220 60
Sakata la kikundi cha ushirika wa wakulima wa chai wa Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga limeingia sura mpya baada ya watu mbalimbali kuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba afikishwe mahakamani kwa kuchochea uasi.

Wametaka serikali kumvua unaibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknorojia kwa kuwa kitendo hicho ni cha udhalirishaji wa serikali, jamii ya Watanzania na nchi kwa ujumla.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuitaka serikali itoe tamko haraka iwezekanavyo ili kurejesha hali ya amani badala ya hatari iliyotangazwa na baadhi ya watu wakiongozwa na mbunge wa jimbo hilo.

Ofisa wa chama hicho mkoa, Jonathan Bahweje, alisema kuwa kutokana na matokeo ya vurugu hizo zilizodaiwa kuchochewa na kiongozi huyo, Chadema inaunga mkono bodi ya UTEGA kutaka kumfikisha mahakamani mbunge huyo pamoja na kuitaka serikali ichukue hatua kali ikiwa ni pamoja na kumuondoa kwenye orodha yake ya manaibu waziri ili kulinda heshima ya nchi.

Bahweje ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu ametoa siku saba kwa serikali kuhakikisha uasi huo unazimwa na shughuli kiwandani hapo kuendelea ili kumpunguzia hasara zisizo na ulazima mwekezaji huyo na siku 14 nyingine za kumchukulia hatua Makamba.


Alisema yeye kwa niaba ya chama Mkoa wa Tanga wanalaani vitendo vya kufungiwa nje kwa kufuli walinzi wa kiwanda hicho waliopo wawapo ndani ya kiwanda watu wanaojiita wawakilishi wa wakulima na kwamba hatua hiyo ni ukatiri na ni hatari na ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Alieleza kuwa kwa kuwa matukio yote ya kihalifu yanayofanywa na wakulima hao yanaelezwa kuwa ni utekelezaji wa maazimio ya mkutano baina yao na mbunge huyo ni wazi kuwa serikali imehusika na vurugu hizo na ili kujisafisha ni kumuwajibisha Makamba aliyeuitisha.

"Huyu bwana kwanza ni mvunjaji mkubwa wa demokrasia…ameshawahi kumhujumu aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya Kwekitui kwa tiketi ya Chadema ambaye alitoroka siku mbili tu baada ya Mbunge huyo kufanya ziara kijijini hapo…hii ni hujuma, hafai mtu huyu," alisema Bahweje.


Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wa chai walisema kuwa hakuna ubishi juu ya uvurugu zinzoendelea baina ya muwekezaji wa kiwanda cha chai Mponde na wakulima zimebuniwa na Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba. Baadhi ya wananchi ambao ni wakulima wa zao la chai Jimbo la Bumbuli, walidai kuwa chimbuko la mgogoro huo ni kutokana na masuala ya kisiasa na kwamba hauna tija yoyote.

Wakulima hao ambao ni wapigakura wa Makamba ambao walionekana kumgeuka, walieleza kuwa vurugu hizo zinawaathiri kwa kiwango kikubwa na kwamba wanalazimika kula mlo mmoja kwa siku baada ya kiwanda kuzuiwa kufanyakazi. Walidai kuwa sababu ya vurugu hizo ni kutokana na mbunge huyo kutaka kuhakikisha kuwa sehemu zote muhimu anaweka wapambe wake ili kujiweka vizuri kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
H

hans79

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2011
Messages
3,802
Likes
26
Points
145
H

hans79

JF-Expert Member
Joined May 4, 2011
3,802 26 145
Haya bana gamba hanashindwa hoja wanakimbilia mbinu dhaifu za kuiba kura.Gamba kila jambo wapo dhaifu
 
zomba

zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,081
Likes
84
Points
0
zomba

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,081 84 0
Haina mshiko hii habari yako. Peleka kwenye vijiwe vya mbege.
 
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Messages
12,498
Likes
2,644
Points
280
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2012
12,498 2,644 280
Haina mshiko hii habari yako. Peleka kwenye vijiwe vya mbege.
Mkuu hebu tupe ya kwako yenye Mshiko!!!
Nafikiri zenye mshiko kwako ni kama
1. Lekwatare anyongwa kwa Ugaidi
2. Dr slaa agombana na Rose Kamili
Kama unahitaji kama hizo nenda kwenye magazeti ya shigongo
 
Maboso

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Messages
4,555
Likes
3,077
Points
280
Maboso

Maboso

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2013
4,555 3,077 280
Nipashe nao wamekosa habari za kuandika maana hata haieleweki
 
S

salisalum

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2010
Messages
379
Likes
19
Points
35
S

salisalum

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2010
379 19 35
Itaeleweka tu!
 

Forum statistics

Threads 1,272,642
Members 490,095
Posts 30,455,814