Chadema nao wakishindwa wakubali bila kulalamika

NgomaNgumu

Senior Member
Nov 20, 2010
194
24
Chadema imeshinda ubunge Arumeru Mashariki ambapo takriban wapinzani wote walizipokea habari hizo kama tukio la kawaida. Ingawaje ktk chaguzi ningine nyingi chadema wanakua wazito sana kukubali matokeo ya uchaguzi na ni lazima watatia dosari kwa njia moja au nyingine. Ni vyema wakishindwa wakakubali matokea kwani kufana hivyo ndio kuwiva kidemcrasia.
 
Mazingira ya chaguzi zetu yapo wazi. Upinzani kushinda uchaguzi mpaka wakomae sasa la sivyo inakula kwao! Mpaka wapiga kura walinde kura zao na waoneshe kweli wakidhulumiwa watawasha moto ndio haki itatendeka! Katika hali kama hii NgomaNgumu ni vigumu anayeonewa kila mara kukubali matokeo. Tumeanza vibaya na tutamaliza vibaya pia na kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa haraka huko mbele ni kiza kinene. Wanaosimamia uchaguzi hawaaminiki kwenye macho ya wanaochagua unatazamia nini kwenye hili?
 
mbona matokeo ya ubunge\uwakilishi yalofanyika Zanzibar majuzi kati Chadema waliyapokea bila zengwe na wakasaini?
 
mbona matokeo ya ubunge\uwakilishi yalofanyika Zanzibar majuzi kati Chadema waliyapokea bila zengwe na wakasaini?

nafikiri mtoa mada hakujua kama uzini kulikuwa na uchaguzi, chadema yanayakubali matokeo kama tu haukukua na mizengwe katika uchaguzi huo, unafikiri uchaguzi kama uliofanyika shy town 2010 chadema ikubali tu kuwa imeshindwa, hata kama wizi na mabavu ya wazi kabisa uliofanyika?. hakuna kitu kama hicho. mbona ccm wanakesi zao za uchaguzi uchwara za 2010 mahakamani hv sasa ingawa kesi zenyewe hazina hata mashiko
 
mbona matokeo ya ubunge\uwakilishi yalofanyika Zanzibar majuzi kati Chadema waliyapokea bila zengwe na wakasaini?

Nimesema hivyo kwa kuangalia matokea ya kiti alichokiacha Rostam Aziz chadema waliyapokea shingo upande pamoja na kua gharama walizotumia CCM Arumeru mashariki zinaonekana kua kubwa zaid lakin wamekubali kushindwa bila kulalamika. Kama kweli tunataka democrasia ya kweli ni lazima tuwe na imani na matokeo yoyote yatakayo tangazwa baada ya utaratibu wa uchaguzi kukamilika.
 
Chadema imeshinda ubunge Arumeru Mashariki ambapo takriban wapinzani wote walizipokea habari hizo kama tukio la kawaida. Ingawaje ktk chaguzi ningine nyingi chadema wanakua wazito sana kukubali matokeo ya uchaguzi na ni lazima watatia dosari kwa njia moja au nyingine. Ni vyema wakishindwa wakakubali matokea kwani kufana hivyo ndio kuwiva kidemcrasia.

Yaani umeshasahau mida hii. Kwenye uchaguzi wa 2010 tuu, CCM wamefungua kesi ngapi mahakamani dhidi ya wabunge wa chadema walioshinda? Mnyika kafunguliwa kesi. Tundu Lissu kafunguliwa kesi. Lema kafunguliwa kesi. Haya nayo sio malalamiko? Sio kwamba naifagilia Chadema bali mikono ya CCM sio misafi pia. Kwa nini CCM wasikubali tuu walishindwa kwenye hizo chaguzi na kuacha kufungua kesi ambazo ukifuatilia hearing zake ni aibu tupu?
 
Mtoa mada nadhani anahasira ya kubwagwa Arumeru na kitendo cha jamaa yao Nape kukubali matokeo haraka. Nadhani alitamani wakatae matokeo ili waende mahakamani, maana hata mgomea wao hakusaini fomu ya matokeo.
 
Nimesema hivyo kwa kuangalia matokea ya kiti alichokiacha Rostam Aziz chadema waliyapokea shingo upande pamoja na kua gharama walizotumia CCM Arumeru mashariki zinaonekana kua kubwa zaid lakin wamekubali kushindwa bila kulalamika. Kama kweli tunataka democrasia ya kweli ni lazima tuwe na imani na matokeo yoyote yatakayo tangazwa baada ya utaratibu wa uchaguzi kukamilika.

ugunga hawakulinda kura zao kama arumeru kwa hiyo inaonesha kabisa ccm waliiba maeneo ya vijijini kwani sasa hivi maeneo ya vijijini hawaipendi ccm kwa sababu ya maisha magumu kwao
 
wao wanataka wae wanashinda wao tu ndio wnakuwa wameshinda kihalali na hii ni kwa wapinzani wote
 
wao wanataka wae wanashinda wao tu ndio wnakuwa wameshinda kihalali na hii ni kwa wapinzani wote

Mmh!! Mmeanza kuibuka mmojammoja, mlikuwa wapi mkuu!!? Bora ya Ritz alijitoa kimasomaso na pongezi japo za kinafiki lakini alitoa!! Wewe na wenzio mnaolipwa na Nape hata za kinafiki hamjatoa!!!
 
Nimesema hivyo kwa kuangalia matokea ya kiti alichokiacha Rostam Aziz chadema waliyapokea shingo upande pamoja na kua gharama walizotumia CCM Arumeru mashariki zinaonekana kua kubwa zaid lakin wamekubali kushindwa bila kulalamika. Kama kweli tunataka democrasia ya kweli ni lazima tuwe na imani na matokeo yoyote yatakayo tangazwa baada ya utaratibu wa uchaguzi kukamilika.

Ukisikia Chadema wanalalamika ujue wamechakachuliwa, ndo maana hawalalamiki kila jimbo....Igunga, Shinyanga, Segerea,.... was obvious kwamba jamaa wameiba. Kumbuka kwamba ccm ndo chama kilicho na serikali ambapo watendaji wote huteuliwa na viongozi ambao pia ni wana ccm. Hata viongozi wa vyombo vya dola na tume ya uchaguzi. Ni rahisi sana kwa chama tawala kuchakachua matokeo lakini haiwezekani kwa chama cha upinzani kufanya hivyo kwa kuwa havina nyenzo zozote za kuchakachulia.
 
Chadema wakishindwa siku zote uwa wanasema wameibiwa kura, wakishinda wanasema wamelinda kura zao!
 
Mmh!! Mmeanza kuibuka mmojammoja, mlikuwa wapi mkuu!!? Bora ya Ritz alijitoa kimasomaso na pongezi japo za kinafiki lakini alitoa!! Wewe na wenzio mnaolipwa na Nape hata za kinafiki hamjatoa!!!

Mkuu, siasa sio uadui muwekeane visasi mwanasiasa unaemkubali leo kesho hanaweza kuwa adui yako mkubwa!
 
Yaani umeshasahau mida hii. Kwenye uchaguzi wa 2010 tuu, CCM wamefungua kesi ngapi mahakamani dhidi ya wabunge wa chadema walioshinda? Mnyika kafunguliwa kesi. Tundu Lissu kafunguliwa kesi. Lema kafunguliwa kesi. Haya nayo sio malalamiko? Sio kwamba naifagilia Chadema bali mikono ya CCM sio misafi pia. Kwa nini CCM wasikubali tuu walishindwa kwenye hizo chaguzi na kuacha kufungua kesi ambazo ukifuatilia hearing zake ni aibu tupu?
Mkuu kulikuwa na agizo la kisiasa la.Mzee Makamba! Baadaya ya kuagiza kusitishwa kwa kipindi cha mchakato majimboni kushindikana na mwisho CCM ikafanya vibaya chini yake akaamua kufuta aibu kwa kuagiza kufunguliwa kwa kesi karibu kila mahala.
 
Mkuu, siasa sio uadui muwekeane visasi mwanasiasa unaemkubali leo kesho hanaweza kuwa adui yako mkubwa!
Katika siasa hakuna urafiki wala adui wa kudumu! Leo Ritz na Rejao wanaweza kuwa marafiki kesho Ritz akahamia CDM na Rejao akabaki CCM!
 
Nikweli CDM ni walalamishi pengine ndio maana hufanikiwa ktk baadhi ya chaguzi.
Lakini CCM nao kwa upande mwingine wamezidi kutumia mabavu na kupora ushindi pasi halali ktk chaguzi.
Hivyo basi kadiri ya hoja zitakavyohudhurishwa hapa kila mmoja atavutia upande wake kulingana na itiqad ya chama chake!
Mwisho naomba tukubaliane kutokubaliana kwani nayo si ni makubaliano pia?
 
Nimesema hivyo kwa kuangalia matokea ya kiti alichokiacha Rostam Aziz chadema waliyapokea shingo upande pamoja na kua gharama walizotumia CCM Arumeru mashariki zinaonekana kua kubwa zaid lakin wamekubali kushindwa bila kulalamika. Kama kweli
tunataka democrasia ya kweli ni lazima tuwe na imani na matokeo
yoyote yatakayo tangazwa baada
ya utaratibu wa uchaguzi
kukamilika.
Sitaki kuumiza kuchwa changu kwa kuchangia thread iliyoandikwa kwa mtazamo wa kufikili kwa kutumia Masaburi, uzi huu unaudhi sana kuandikwa ili usomwe na watu wenye akili timamu
 
Hiyo haiwezi kuwa hoja ya msingi, ikiwa mazingira ya ushindani yako fair, hakuna chama kinachoweza kupinga ushindi wa yeyote ashindaye. Tatizo la ccm, ni kulazimisha ushindi wakati ni dhahiri shahiri wameshindwa, ubabe na kutumia vyombo vya dola kama vile Mwanza haukubaliki kabisa
 
Back
Top Bottom