Chadema nacho kuvua gamba?

twijuke

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
547
252
Mugu Ndugu wana janvi poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa letu, na kwa wale wabomoaji wa taifa letu tusema sasa basi inatosha.

Wapendwa ndugu zanzgu, wakati CCM wameazimia kuvua kile walichokiita GAMBA,Kuna swali nilijiuliza. Ikiwa CCM wamefika mahali na kuona ndani ya chama kuna watu wachafu na hivyo iliwapasa kuwaondoa maana yake lilikuwa ni tatizo. Swali hapa lilikuwa je! ikiwa ni tatizo je nguvu ya kushugulikia tatizo inalingana na ukubwa wa tatizo? na jingine ilikuwa ni je hesabu zimezingatiwa? Ninapo sema hesabu kuzingatiwa ni saw na una bunduki imejaa risasi badala ya kulenga kichwani unalenga mkia.

Tukumbuke watu walio daiwa kuwa ni wachafu ndani ya CCM, ni wale wanao tajwa kwa dhati kabisa kuiingiza serikali iliyopo madarakani, lakini si tu kuiweka serikali iliyopo madarakani bali mchakato mzima katika uungwaji mkono kwa maana ya mahusino ya mtu na mtu, jambo lililo pelekea hawa watu kuwa na wafuasi wengi ndani ya chama, kwani ina sadikika katika chaguzi mbalimbali pesa za kampeini zilizotumika kwa baadhi ya wagombea wengi zilitoka kwa watu walio batizwa kwa jina la FISADI jambo ambalo lilifanya zoezi zima la uvuaji gamaba kuwa gumu, ikizingatiwa kuwa wenye nguvu kiuchumi ndani ya chama ndio walitakiwa kufukuzwa.

Ndugu zangu suala la kumvua Zitto madaraka na mwenzie Dr. Mkumbo binafsi nalifananisa na kitendo cha CCM kuvua gamba ambalo hadi leo wote tu mashahidia ugumu wa uvuaji gamba. Kwa sasa tunapo taja vyama pinzani hapa Tanzania CHADEMA ni Mbuyu, na kama ni Mbuyu wanasema Mbuyu nao ulianza kama mchicha.


Leo Chadema kinaonekana ni chama chenye afya njema, linapo kuja suala la nani wamekifikisha Chadema kilipo, Naapa tutakuwa hatumtendei haki Zitto kama hatumtaji, naamini kabisa wote tu mashahidi kuwa Zitto ni mhusika katika kukinenepesha chama. Kwani umahili wake katika kujenga hoja ndani ya Bunge ni kati ya mambo yaliyo vutia wengi katika siasa za Chadema.

Zitto naye ni binadam, wakati tunamuoona kwa jicho la mabaya tukumbuke kuwa upo utitiri wa meme yake, na kama ndinvyo huenda mema yakawa ni Mlima kuliko makosa ambayo ukubwa wake ni sawa na Kichuuguu.

Lakini lipo swali lingine kuhusiana na suala la Zitto, najiuliza, Je! ikiwa MEMA yake huenda ni kama mlima, alistahiki aachwe? huenda jibu ni hapana, Je! kama ndinvyo adhabu aliyopewa inawiana na kosa? ikumbukwe kuwa si kila majira ya faa kwa kila jambo, kwani jambo laweza kuwa sahihi lakini wakati usiwe sahihi, Je! wakati ulikuwa ni sahihi?


Sifa ya mnene imetokana mwembamba, je tungemtambuaje Mrefu kama si uwepo wa mfupi? Ndugu zangu wana janvi katika nia njema ya kuteanda mema makosa yaweza kufanyika, lakini lipo jingine kubwa, nalo ni kwamba katika kutatua tatizo waweza kusababisha tatizo kubwa kuliko tatizo awali. Naomba niweke wazi simtetei Zitto ila chondechonde hekima na busara kama havikutumika kwenye hili itakuwa sawa na kusababisha tatizo jingine katika utatuzi wa tatizo.


Mungu tubariki sote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom