chadema na zidumu fikra za m/kiti......zidumu!

Status
Not open for further replies.

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,849
2,000
mm nikiwa mfuatiliaji wa siasa zetu kiukweli wala bila unafiki ndani ya chadema chama tulichokiamini, chama kilichoanza kuleta matumaini sasa demokrasia ndani ya chama shakani kama si kumalizwa
1. uchaguzi wa bavicha ulionyesha ni namna gani demokrasia kwa vitendo ni ngumu, kuna hujuma kubwa iliofanywa hata haisemeki wakti viongozi wa bavicha wakichaguliwa hii kila mpenda demokkrasia alikwazika mno
2. mwaka 2009 DEMOKRASIA ilizuiwa kufanya kazi yake kwani baadhi ya waasisi wa chama pamoja na wazee kuzuia misingi ya demokrasia ambayo in asema kila mtu yupo huru kuchagua au kuchaguliwa provided havunji katiba lakini hakuna aliejali takwa hili la kidemokrasia
3. uhuru wa mawazo sasa ni kipimo cha utiii ndani ya chama, ukiwa uko tofauti na baadhi yaviongozi unapewa label ya usaliti kisha unaandailiwa sanduku la kuzikiwa ili usisike tena. demokrasia ya kweli si kukimbia changamoto kwa kuwafukuza watu wenye maoni tofauti bali ndio afya ya chama kwani mnajua mkikosea ndani kwa ndani mnakosoana kisha mnajirekebisha, naogopa sasa chama kinakuwa cha kidikteta kama alivyosema malimu nyerere kama angetaka kuwa dikiteta agekuwa kutokana na jinsi alivyokuwa hapendi kukosolewa na alipenda aambiwe zidumu fikra za mwenyekiti....zidumu hapo ndipo hata mwasisi EDIN MTEI alipoamua kutoka CCM sasa mbona leo tumesahau kwa muda mfupi huu na kutaka kukata matawi wakati ndio yanashikilia mti ili ukue
4. uwazi wa matumizi na uteuzi ndani ya chama, demokrasia maana yake ni uwazi kwa kila hatua inayofanyika ndani ya chama, utakuwa mwendawazimu kusema ndan ya chama hakuna malalamiko juu ya matumizi ya fedha na rasilimali za chama pamoja na uteuzi wa maafisa,wakuregenzi, mpaka namna viti maalum vyawanawake kote kuna malalamiko. kutumia ubabe kuua hoja au malalamiko huko ni kuua demokrasia bali demokrasia ni kuijib hoja kwa data, uwazi na malalamiko yataisha
5.waasisi kuchagua nani atakuwa kiongozi au nani hatakuwa kiongozi huo ni ubakaji wa wazi wa demokrasia mfano mzuri ni mzee wetu ARFI alilalamika wazi juu ya mwasisi kuingiliakazi za chama na kutaka kuwachagulia viongozi demokrasia ya kweli haiko hivo, viongoz wote wawe na iko access yanafasi yoyote ndani ya chama n sanduku la kura ndilo liamue nan awe kiongozi wetu na nan asiwe kiongzi wetu. 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom