Hossam
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 3,538
- 2,155
Kila siku kukicha utasikia CCM kaiba kura zetu, kanunua shahada, kachakachua matokeo, tunaenda court! Ni sawa hayo yoote ni sawa wala hapana shaka. Wazo langu ni kwamba, CDM ijitahidi kuwa na wanachama wapigakura wengiiii ili hata CCM wakiiba vipi kura wabaki wameshindwa tu, hii ndio hoja. Hapo utaona hiyo nguvu ya umma 'ikihoji' matokeo bila hata kuhamasishwa. Kwa sababu ni sawa na baba kuwa na mkewe na watoto nane wote wana shahada za kupiga kura. Halafu baba kama mgombea akapata kura moja tu katika kituo cha kupigia kura wakati anajua kwenye kampeni mama na watoto walikuwepo, wakala wake amamwambia ni kweli alishuhudia kura moja tu, atafanyaje? Unadhani atanyamaza wakati mkewe na watoto wako kimya pia? Ni kivumbi hom tu hapo, talaka itaandikwa kwenye kituo cha daladala, na kwa watoto wakatafute baba yao, hiyo ndio demokrasia ya kweli. Tuwajenge wananchi wazalendo wahoji uhalali wa mambo bila kuhitaji msukumo. Alamsiki wandugu...