CHADEMA na washirika wenu jiandaeni kukabidhiwa nchi 2020

Sasa ni wakati mwafaka kwa vyama vya upinzani kupokea kijiti Kutoka kwa CCM ifikapo 2020, ingawa CCM haiko tayari kuona nchi inatwaliwa na upinzani kutokana na mazowea na ulevi wa madaraka ambayo wamekuwa nayo kwa miaka mingi, kumekuwa na vuguvugu la vyama vya upinzani duniani kupata ushindi wa kushitusha, wote tumeshuhudia Donald Trump Republican alivyombwaga Hilal Clinton wa Democratic ambacho ndicho chama tawala kwa miaka nane, Rodriigo Dutete wa Philipins, Nana Akufo Ado kamshinda John Mahama raisi anayemaliza muda wake huko Ghana.

Kadhalika Gambia muungano wa upinzani ukiongozwa na Adama Barrow wamemshinda rais wa nch hiyo Yahya Jammeh, kwa hapa bongo kinachotakiwa ni kuungana vyama vyote vya upinzani ili kuwa na nguvu za pamoja ingawa zipo changamoto za kuunganisha vyama hasa unapokuwa na wapinzani aina ya Dovutwa na Lipumba, Kiuhalisia CCM imeshachokwa ila upinzani nao wamekuwa wanashindwa kuweka mikakati sahihi ila naamini safari hii kwa kuwa CHADEMA wamempata mtaalam wa mikakati mr Lowassa 2020 ndio mwisho wa CCM huo ndip ukweli mchungu kwa chama cha mapinduzi.

Wapinzani walikuwa na heshima zamani wakati Viongozi kama Dr Slaa alikuwa kiongozi, kiongozi mwenye principal. Sasa imeshikwa na wapiga dili kila kona. Lowassa alihamia Chadema siyo kwa principal zake, bali kwa tamaa ya kuwa Rais, kusema ukweli Lowassa hawezi kuleta mabadiliko zaidi ya kuligawa taifa, kati ya matajiri wachache na masikini wengi wa kutupa. Na kama Watanzania wanafikili Lowassa ataleta mabadiliko, kumbukeni sakata la Richmond lilomfanya ajihudhuru, mpaka Leo hatujui kesi yake iliishia wapi, tumeshitukia tu anaomba atuongoze, Je kesi imeishia wapi? Mbona hawa viongozi wametufanya sisi hatuna akili, kila mtu anataka kuwa kiongozi hata walio tukopa pesa zetu na kushindwa kutulipa, Je wakishika uwongozi sinwatachota tu bila ya kutuuliza mpaka hata taifa likose maji ya kunywa. Chadema wakati kiongozi wao bila ya haya kakaa kwenye jengo la NHC, jengo la umma bila kulipa kodi zaidi ya billion 1.5? (Excuse my language ) Si itakuwa kuluka tope na kukanyaga mavi?

Mpaka Sasa pamoja na makosa madogo madogo kwenye serikali ya Rais Magufuli, sioni alternative zaidi ya serikali ya Rais Magufuli . Mimi najuwa kuna upinzani mkubwa kwa anayoyafanya kwa faida ya Watanzania wote, kwa mwendo wake wa kuligomboa taifa kutoka kwa wapiga dili, watu wenye ubinafsi, waliozowea kujipatia utajili kwa shida za wengi hawa ndiyo wanaotuyumbisha. Kufanikiwa zaidi kwa Rais Magufuli, itambidi hatuwa anazochukuwa kwa mufano ya kuchunguza vyeti n.k zisichaguwe, kama kuchunguza basi vichunguzwe vya wafanyakazi wote asichaguwe, akichaguwa imani ya wananchi itashuka. Ni kazi kubwa kuligomboa taifa hili, baada ya uongozi mbovu wa miaka mingi, Watanzania wengi tumekuwa wavivu wa kutupa, eliminated dunia ambayo haiendi na wakati, tumezowea kuchuma bila ya kufanya kazi.
 
Kipimo cha wapinzani kutawala nchi kutatokana na uwezo wao wa kuyaletea maendeleo katika maeneo tulowachagua kwanza.mi nadhani huo ndio mtaji mkubwa wakiutumia wataingia magogoni
Lakini miaka mitano hii wakiendelea kuitumia kukimbizana na polisi kushinda kwenye viunga vya mahakama kushupalia tz kuna balaa la njaa baada ya kuwahamasisha wananchi wao kulima mazao yanakabiliana na ukame.wapinzani timizeni ahadi zenu kwanza itawasaidia sana kuingia ikulu
 
Back
Top Bottom