CHADEMA na washirika wenu jiandaeni kukabidhiwa nchi 2020

Nikiiangalia ukawa kwa jicho LA mbali naona hata wakishinda hawawez kuunda serikali maana kule hakuna hazina ya viongozi wanaoelewa jinsi ya kutawala watanzania,,,
 
Kwa USA, ni kawaida kubadilishana. Kabla ya Democrats (Kipindi cha Obama) walikuwepo Republicans.

Kama kutakuwepo na tume huru ya uchaguzi, upinzani nchini TZ wanaweza kushinda lkn kwa tume hii sijui. Pia wajipange kuwapa watu wa vijijini elimu ya uraia ili kuwaondoa hofu ya kuchagua upinzani maana wengine huamini kuwa kuuchagua upinzani ni kuleta vita
Hata kama itakuwepo tume mpya, bado hawawezi kushinda, huwezi kushinda kama hujawa na maandalizi ya viongozi wa juu, na hilo ndo tatizo, ukiona watu wanakaa kwa kuvizia kama simba mzee, kwa wenye akili na kutafakari wanaelewa kuwa hamna kitu, kama mpaka dakika za mwisho huna kiongozi wa nafasi ya uraisi alafu unavizia wanaotemwa na chama A, alafu unajipa matumaini kuwa utashinda je walomtema wao watasemaje, anzeni mapema kuandaa viongozi na kama tena ni uviziaji - bado mtaendelea kuchemsha.
 
Red: Naamini unawalenga wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani. Count me out.
Je, Miaka yote wamekuwa wakivizia hadi dk za mwisho kumpata mgombea aliyetemwa chama A?

Wapinzani kushindwa ktk uchaguzi hasa kiti cha urais unachangiwa na sababu nyingi, tume ya uchaguzi ikiwemo.
 
Kweli bora tuchukue sisi wapiga dili aiseeee hatukubali kabisa.

Yani mambo yetu hayaendi kabisa.
Huyu jamaaa amefukuza miladi yetu ya wafanyakazi hewa hapana hatutaki 2020 bora tumpe Lowassa tu.
 
Ni wakumbushe tu kuwa hakuna mwaka mlikuwa na matumaini kama mwaka 2015, mliamini kama mnachukua Nchi kwa 80% au90% sasa endeleeni tu kujifariji,mlijaribu kuweka "wadukuzi" ili muibe kura kwa kuuinglia mfumo wa kieletroniki wa kutoa matokeo mkaishia kudakwa na dola,hizo ni ndoto tu jifarijini
 
Ukawa walishinda kwa kura nyingi sana lakini wale vijana wa Mtandao wa ukawa walikuwa sahihi wawazo na ukweli lakini ukatumika Udikteta kuwakamata na kuacha kikundi chao cha uchakachuaji ndipo wakawahadaa watanzania kuwa wamepata ushindi mkubwa, na kama ni mfumo wa kieletroniki kuingiliwa uliingiliwa na CCM ambao timu yao iliweka kambi kule masaki chini ya usimamizi wa February.
 
Vijana Bado Mnajidanganya , si Chadema Wala NCCR chenye Uwezo Wa Kutawala Nchi hii, Maana Sioni Sifa Za wazi Ndani Yao so Kutawala Nchi Hii , Hawana Sera Wala Mbinu za Kuweza Kuteka Hadhira ya Watanzania , Chama Pekee Ambacho Na kiona Na kilikuwa Kweli Kina sifa Za kuweza Kutrake Over Ni CUF, Ila wamefail Kwa Sasa Wameshindwa kusimamamia Katika sera Zao Na Agenda, so Itakuwa VIgumu Kurejesha , Iman .....Kama Tutakuwa Hai Mwaka 2040 Panapo Majaliwa Ndo Mwaka Ambao Kwa Mara Ya Kwanza CCM watatoka Madarakani, na Chama Kitakachoingia Madarakani si CDM Wala NCCR ama CUF bali kitakuwa Kipya Na Chenye Sera Endelevu Chenye kuweza Kusimama Na sera Zake..
 
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
 
Nikiiangalia ukawa kwa jicho LA mbali naona hata wakishinda hawawez kuunda serikali maana kule hakuna hazina ya viongozi wanaoelewa jinsi ya kutawala watanzania,,,
Hazina ni JPM kwa kipindi cha mwaka ametengua zaidi ya ishirini ikifika 2020 ataingia kwenye vitabu vya Guinness kiongozi ambaye kila mwezi lazima atengue uteuzi wa wateule wake angalau kwa uchache wawili
 
Wapinzani wakitaka kushinda ni lazima kwanza wawaunganishe watanzania ambao ama kwa hakika wamegawanywa sana na CCM.
Ni lazima Wapinzani waje na sera ya kuunda serikali ya pamoja.
Waje na sera ya kufanya marekebisho ya katiba na kuweka serikali ya pamoja.

Serikali itakayowaweka madarakani watu wenye uwezo na maono mapana bila kujali kabila,dini,chama na rangi.
Hata muzungu au muhindi akiwa ni mtanzania mwenye maono chanya kwa taifa letu basi ateuliwe awe mkuu wa mkoa au wilaya au hata uwaziri.

Upinzani wameshaona madhara ya ubaguzi wa kiitikadi waliofanyiwa kwa muda mrefu. Sisi wote ni watanzania ni lazima tufikie mahali tuweke maslahi ya pamoja ya Taifa na sio vyama.
Kwa sasa tunaona jinsi CCM inavyojenga chuki dhidi ya wale wasiounga mkono chama chao. Leo ukiwa mpinzani unakua ni adui mkubwa asiye na thamani yoyote katika nchi hii.
Hata maisha yanakuwa ni kama bahati na sibu mana hata ukiuawa na majambazi hata uchunguzi unaofanya na vyombo husika unakua ni wa kusuasua.
Mpinzani hata akiwa na madai yake ya kisheria anakua na wakati mgumu sana kwenye nchi zetu za kiafrika na hata tanzania imeshaanza kuwa na mfumo huo usiowatendea haki wale wanaopingana na chama tawala.

Wapinzani ni lazima waje na mfumo tofauti wasije kuwa kama CCM kwa kuendeleza hali hii ya kuwabagua na kuwaumiza na kuwatesa waafrika na watanzania wenzao kwa sababu tu ya vyama vilivyoundwa na watu waliokua na malengo yao binafsi.
Ni lazima binadamu na ubinadamu uwe ndio kitu cha kwanza hapa duniani.
Binadam akiondoka kwa kwa maana ya kunyanyaswa au kuteswa na hatimaye kupoteza maisha haiwezekani tena kumrejesha lakini vitu vinaweza kutengenezwa upya tena kwa ubora zaidi. Tusiutweze na kuudhalilisha utu wa mtu kwa namna yoyote kwa sababu ya kutaka vitu vya kidunia.
Ni lazima binadamu aheshimiwe na kupewa kipao mbele.
Vyama vya upinzani huu ndio wakati wa kuanza kujenga sera imara kwa taifa letu. Hasa sera za kuwaunganisha watu.
Kwa sasa nchi hii watu wanachuki hata pale panapohitaji kuvumiliana. Viongozi wanaolipwa mamilioni kwa ajili ya uongozi na majukumu waliyopewa ikiwemo kulaumiwa na kusemwa vibaya leo hii wamegeuka kuwa watu wenye hasira jazba na kukosa uvumilivu. Wao ndio wamekua na hamaki na kila aina ya kulipa visasi kwa wale wanaowakosoa. Utafikiri wanajitolea bure kulitumikia taifa hili kwa gharama za familia zao,kumbe wengine wameingia madarakani kwa kila aina ya mbinu wakijua kuwa ni sehemu ya kuwa na maisha bora na yenye unafuu na heshima kubwa.
Viongozi wetu wanapaswa wawe wavumilivu sana kwa wakosoaji wao kama alivyofanya Lowasa na Mwinyi. Huo ndio uongozi. Kwa nchi changa kukosolewa kwa malalamiko ni jambo la kawaida.

Hakuna namna ya wapinzani kushinda kwa urahisi kama wataendelea na mipango na misimamo inayofanana na ile ya CCM. Ni lazima kila mtanzania apewa ahadi na aone kuwa ana nafasi sawa ya kuheshimiwa na kulijenga taifa lake bila kubaguliwa au kupuuzwa kama ilivyo sasa ambapo hata vyombo vya dola vinafanya kazi sio kwa weledi bali kwa ukada , sio kwa maono ya kusimamia haki sawa na kufuata sheria bali huyo ni mwenzetu na yupo kwa ajili ya kuwazuia wale wasiingie kwenye utawala.
Ningetamani nione wapinzani wakiwa na maono ya kuwatumia watanzania wote wenye uwezo bila kujali vyama. Uchaguzi ukiisha watu wote wunganishwe ili kujenga taifa . Sio kama wanavyosema CCM leo kuwa uchaguzi umeisha tujenge nchi huku ikiwajaza makada wa CCM kila idara bila kuangalia uwezo wao.
Nilitegemea watu kama Kafulila ,Zito, Mdee , Rwekatare , Mtatiro, Mbatia na wengine wengi wangekuwa wanapewa nafasi katika kujenga taifa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi ili kuonyesha kwa vitendo kuwa uchaguzi umekwisha na sasa tunajenga nchi. Matokeo yake hata wakuu wa mikoa na wilaya wamekua wakiwatenga na kuwanyanyasa wapinzani wa CCM. Kadi ya CCM imekua ni ya kuwatengeneza binadamu wa daraja la kwanza na hao wengine ni wa daraja la pili. Hii sio Tanzania iliyokuwa imepiganiwa na babu zetu ili kupata uhuru. Uhuru walioupigania wazee wetu haukua na malengo ya kuwatengeneza wakoloni kupitia vyama vya siasa.

Wapo watu wenye uwezo ndani ya CCM na pia wapo wenye uwezo kwenye vyama vya upinzani. Hawa wote ni lazima washirikiane ili tusonge mbele na sio kuchukiana na kubaguana kwa misingi ya vyama. Mambo ambayo kwa sasa yanafanywa na wanasiasa yanawagawa watanzania badala ya kuwaunganisha.
Watanzania wote kwanza vyama baadae.
 
Mpaka sasa, hakuna dalili ya chama cha siasa cha upinzani chenye uwezo wa kuiondoa CCM madarakani.

Vyama vilivyopo vina uwezo wa kuikumbusha tuu CCM na serikali yake kutimiza wajibu wake, na sio kushika dola.

Huo ndo ukweli, japo ni mchungu.
 
The best post ever seen for the truly mutual national benefits. I wish ACT Wazalendo, chadema CUF, NSSR and my favorite party CHAUMA will buy this brilliant idea. Without setting national agenda with a well diversified opposition leaders and, CCM will rudely rule this country for even over the next 100 years. I don't see any logic to exclude other people wrt their ethnic background or political affiliations in building their nation. By the way, the current leadership system results into more uncoordinated approach than the one you propose. It kills even our patriotism. The time is now to get away from this outlandish system. We divide our country unnecessary, being opposition is like temporary being suspended your citizenship. Seriously, we can't move in this way!

It doesn't matter whether a person is from opposition; an indian, arab, chinese, American etc, as long s/he is Tanzanian and has courage and very much concerned about the county poverty, should actively be involved, participate and given a chance to contribute to the national development agenda, including taking high level technical and political positions.

This has worked and still working very well in many countries now like US, UK, Canada, etc. The current Governor of UK used to be a governor of Central Bank of Canada before (dual citizenship +natural relationship between UK and Ca).

We real need a new approach to run our country if we care about development and long-term national sustainability. Big up great thinker.
 
Back
Top Bottom