CHADEMA na wapinzani wengine, mkiendelea kucheza ngoma ya CCM na Polisi msahau kutawala

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Kinachoshangaza ni ninyi mnaoitwa vyama vya upinzani nchini kikiwamo chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, mmeshidwa kabisa kuwa na non-stop mission ambayo ingeweza kusaidia kuwapa nguvu kuwaambia watanzania yanayoendelea juu ya Katiba Mpya nchini ni uonevu na ni kuzuia haki ya msingi ya kila raia.

Mnachezeshwa ngoma ya CCM na Polisi wakiwapiga mikwara nanyi mnalegea na vimikwara vyenu visivyoisha, wewe John Mnyika si ulisema mtakua na maandamano yaliyoishia na makongamano yahusuyo katiba mpya? Mmekaa kimya napiga kelele mnachezeshwa segere na CCM pamoja Polisi eti mnaogopa kufutiwa chama chenu, kwani chama kikifutwa ndio mwisho wenu wa siasa? Si miwaache wafute? Si mna akili ninyi chama kikifutwa mtakosa la kufanya?

Nimewahi kuona maandamano yasiyo ya kikoloni nchini Kenya ya kudai tume huru ya uchaguzi na polisi walikamata mpaka wakachoka na hatimaye wakafikia walipo hivi sasa wanaheshimiana. Unafki wenu na uogoa ndio unaoipa Polisi na CCM kufanya wafanyavyo. Mwenyekiti wenu yupo ndani mmekua wa bariidi eti suala liko mahakamani, kule Afrika kusini kuhusu hukumu ya Zima kesi haikua mahakamani? Wafuasi wake walifanyike? Acheni kuogopa kukaa Selo wakati mnajua kua kuna mambo hayapo sawa kisheria na kikatiba.

Hawa hawa CCM ndio waliowaondoa kwenye uchaguzi nchi nzima na polisi walikuwepo wanaangalia tena wengine wakiwaambia wapinzani hadhari kua hawawezi kushinda.Hamjawa Aggressive kuiondoa ccm madarakani hata wapinzani wa nchi jirani wanawashangaa sana. Ni kama mpo kwenye siasa kuigiza mkiwazia madaraka na familia zenu balaa ya taifa.Wananchi wamechoka hawana mbadala wa kuwasemea ndio maana hata kwenye kupiga kura wengi hawajitokezi.

USHAURI WANGU KIPI CHA KUFANYA
Ikiwa mnajua mko ndani ya haki msiogope kujazwa mahabusu za polisi na magereza acheni zijae tu. Mnatakiwa kusimama kwa nguvu na jambo ambalo mkiwaaminisha wananchi watawaunga mkono msikalie kuogopa ogopa. Ninyi vyama vya siasa ndio wahanga nambari moja wa katiba mbovu iliyopo na CCM ndio wanufaika nambari moja pia.

Hata kama suala la Mbowe liko mahakamani na aina ya kesi anayotuhumiwa na utofautiano wa maelezo ya hati ya Mashtaka na yale ya Polisi msingeweza kuendelea kukaa kimya.Pazeni sauti kwa nguvu Mbowe afutiwe makosa au apewe dhamana msikae kimya.
 
Sijawahi kuona chama chenye watu wabishi kama CHADEMA, kila kitu wao wanajua
 
Tatizo la Chadema na upinzani wote ni Uongozi, tulio ishi ndani kwa zaidi ya miaka 21, 1994 to 2015 tunafahamu vizuri.

Hata Mbowe binafsi anajua hilo. Huwezi kuwa na vyama vinavyo aminiwa na wasomi lakini vinaongozwa na watu wenye elimu ya Mungu nisaidie.

Na ikitokea msomi yeyote atoe mawazo mbadala atapigwa vita sana, kosa ni kutaka ubora wa uongozi. Utapona tuu kama utaimba nyimbo za viongozi waliopo na nyimbo zile tuu wanazozitaka.

Na lazima uimbe sana nyimbo hizo hata kama wana upungufu unao onekana wazi kwa wenye macho .
 
Ushauri chama kiongozwe na wakurya na wajarua ndo wawe viongozi wakuu hawaogopi kuwa frontline,bila kusahau wasukuma,wanyakyusa,wagogo,wanyaturu warangi hawa no watu ambao wanakuwa na hasira za asili hawahitaji kunywa mbege,ugoro na mirungi kama wachaga
 
Ushauri chama kiongozwe na wakurya na wajarua ndo wawe viongozi wakuu hawaogopi kuwa frontline,bila kusahau wasukuma,wanyakyusa,wagogo,wanyaturu warangi hawa no watu ambao wanakuwa na hasira za asili hawahitaji kunywa mbege,ugoro na mirungi kama wachaga
Duh,akili zako ni hatari!
 
Ushauri chama kiongozwe na wakurya na wajarua ndo wawe viongozi wakuu hawaogopi kuwa frontline,bila kusahau wasukuma,wanyakyusa,wagogo,wanyaturu warangi hawa no watu ambao wanakuwa na hasira za asili hawahitaji kunywa mbege,ugoro na mirungi kama wachaga
Wasukuma hapana,hakuna watu weaoga kama wasukuma.
 
Kila kitu ni hatua.sidhani kama siasa vya vyama vingi vya hili taifa vimefikia uko kwenye mifano unayoitoa. Jipe muda kutafakari mabadiliko ya jamii halafu jiulize kati ya CCM na vyama vya upinzani ni yupi yuko kwenye wakati mgumu.

Ukiona chama tawala kimejiegemeza kwenye vyombo vya dola inatskiwa ujue hiyo ndiyo pumzi yao ya mwisho.Na kwa hatua ilikofikia jamii sasa hivi ni kiasi cha muda kidogo tu yote wanayoyahitaji wapenda mabadiliko yatakua dhahiri, hatua hiyo ikipita bado CCM wakaendelea kupumulia mashine ndo hayo mawazo yako yatakapojileta.
 
Back
Top Bottom