Chadema na usimamizi wa fedha zake; mgongano wa maslahi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na usimamizi wa fedha zake; mgongano wa maslahi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Balantanda, Dec 5, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  • YAONYESHA MBOWE, NDESAMBURO WANAKIDAI CHAMA SH53 MILIONI

  Fidelis Butahe

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) kimesema kwamba kama kuna mtu mwenye ushahidi kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chama hicho ni mafisadi atoe ushahidi.

  Vilevile, kimetoa taarifa kwamba mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo wanakidai chama hicho jumla ya Sh53milioni walizokikopesha.

  Hata hivyo, Chadema imechukua hatua hiyo inayokifanya kuwa chama cha kwanza kuweka wazi mapato yake ya fedha na matumizi yake, baada ya wanachama kuutuhumu uongozi kuwa unafuja fedha za chama.

  Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alilieleza gazeti hili jana kuwa kati ya fedha hizo, Mbowe anadai Sh 42milioni na Ndesamburo Sh 11milioni.

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Dk Slaa alisema: "Deni la Ndesamburo ni Sh11m, wakati Mbowe anadai Sh 42milioni ambazo zinaweza kuongezeka muda wowote kwa sababu chama kinajiendesha kwa michango.

  "Nasema hivi, tutaendelea kukopa na kulipa bila kukoma kwa sababu hata Marekani wanatumia utaratibu kama huu.

  "Mbowe ataendelea kuwa mtia saini wa chama, hilo halina mjadala. Wasioelewa hapa inatakiwa waelewe kuwa fedha zote za chama lazima zipite kwanza kwa mdhamini, sasa kunapoibuka maneno kuwa fedha za Chadema zinatafunwa na mwenyekiti, hakuna ukweli wowote."

  Dk Slaa alikuwa akielezea maamuzi ya kikao cha kamati kuu ya Chadema kilichofanyika Desemba 2 hadi 3 kwenye hoteli ya Keys iliyo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

  Alisema pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili taarifa zilizohoji uteuzi wa Mbowe kuwa mtiaji saini wa chama kwa mujibu wa taratibu za fedha.

  "Baada ya kujadili kiliamua kwamba, Mbowe kwa wadhifa wake aendelee kuwa mtiasaini kama sehemu ya usimamizi wa kifedha uliopo kwenye taratibu za fedha za chama zilizopitishwa na vikao vya juu vya chama," alisema.

  Dk Slaa alisema Chadema hakuna ufisadi na kwamba haiogopi kukaguliwa, iko tayari kukaguliwa kwani ukaguzi ni kazi ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

  "Fedha za Chadema, CUF na UDP ukizijumlisha huwezi kufikia hata nusu ya fedha zinazotafunwa CCM.

  Chadema hatuwezi kuogopa kukaguliwa na CAG na hatuwezi kumwita atukague... kwani hajui kazi yake? Sisi hatuna wasiwasi na hilo tunajiamini, labda anaogopa kuwa akifanya hivyo anaweza kuiumbua CCM," alisema Dk Slaa.

  "Wanaosema Chadema ni mafisadi warejee sheria namba 375 hapo ndipo watakapojua kuwa kelele zao ni 'makelele ya debe tupu', lakini pia wanaosema hayo waje hapa wakiwa na vielelezo vinavyoonyesha jinsi hizo fedha zinavyotafunwa sio kusemea pembeni"

  Maamuzi hayo ya CC ya Chadema yamekuja huku aliyekuwa ofisa habari wa chama hicho, David Kafulila na ofisa wa masuala ya Bunge Danda Juju ambao walienguliwa nyadhifa hizo na baadaye wenyewe kujitoa Chadema, wakikitupia tuhuma nzito chama hicho.

  Kwa nyakati tofauti Kafulila na Juju walishutumu kitendo cha Mbowe kuwa mtiaji saini wa fedha za chama huku wakimwomba CAG kukagua mapato na matumizi ya chama hicho kujionea ubadhirifu.

  Kafulila alieleza hayo juzi katika hafla iliyoandaliwa na NCCR-Mageuzi kuwapokea wanachama wapya. Alisema Chadema kuna ufisadi na kusisitiza kuwa kama viongozi wa chama hicho wakiendelea kujificha, atawaumbua.

  Hata hivyo, jana Dk Slaa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Kafulila na Juju wanazungumza maneno ya uongo kwa lengo la kujipatia umaarufu wakati hata siku moja hawakuwahi kuzungumza au kulalamika kwa barua kuhusu suala la matumizi mabaya ya fedha ndani ya chama hicho.

  "Hapa naomba mnielewe waandishi kikao hiki cha kamati kuu kilikuwa hakijadili mgogoro ndani ya chama. Baadhi ya ajenda zilizojadiliwa ni tathmini ya uchaguzi wa serikali za mitaa, mikakati ya kutekeleza mipango na mikakati ya chama, kuthibitisha makatibu wa wilaya na mikoa, taarifa za rufaa mbalimbali za uchaguzi wa ndani, taarifa za mfumo wa kiuanachama kwa njia ya elektroniki, taarifa za fedha, uteuzi wa bodi ya wadhamini pamoja na kupanga tarehe ya mkutano wa baraza kuu na mkutano mkuu na mengineyo," alisema Dk Slaa.

  "Pamoja na hayo suala la Kafulila na Juju lilizungumzwa pia kwenye mkutano huu lakini halikuwa ajenda kuu. Hapa mnielewe lilijadiliwa lakini halikuwa ajenda kuu."

  Alisema kuwa Chadema haiwezi kupangiwa na mtu jinsi ya kujiendesha na kusisitiza kuwa anayejua machafu ya Chadema ajitokeze wazi na kusema bayana kama mbunge huyo wa Karatu anavyofanya bungeni.

  "Mimi kumwita Kafulila na Juju 'sisimizi' kuna tatizo gani? Hiyo ni kama 'analogy' tu ni misemo ya kisiasa mbona rais wa awamu ya pili aliwahi kusema kuwa yeye ni kichuguu akijifananisha na Nyerere, hilo sio tatizo," alisema.

  "Akina Kafulila walitakiwa kutambua kuwa kila chama kina msemaji wake, sasa wao kikao cha chama wanasema kana kwamba chama kimekaa 'geto', hapo kwa nini wasichukuliwe hatua?

  "Maamuzi niliyoyafanya kwa Kafulila na Juju yamepongezwa na CC, wanachotakiwa kujua ni kwamba hata mimi leo nikiondoka Chadema itaendelea kuwepo, kuondoka ndani ya chama ina maana kuwa umeshindwa kuendana au kuhimili ajenda za chama"

  Akizungumzia ajenda ya hali ya siasa nchini ambayo ilijadiliwa katika kikao hicho, Dk Slaa alisema taifa limegubikwa na migogoro na malumbano yanayosababishwa na uongozi mbovu na udhaifu wa kisera wa serikali na taasisi zake.

  "CCM nayo imegubikwa na malumbano ya hali ya juu yanayoashiria kufilisika kwa hali ya juu kimaadili kama tulivyoeleza kwenye orodha ya mafisadi Septemba 15. 2007," alisema Dk Slaa.

  Alisema Kamati Kuu imebaini pia kuwa uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa ulikuwa wa kihuni na kulitia aibu taifa kwa kuwa uliendeshwa kinyume na kanuni na misingi ya demokrasia na haki za binadamu.

  "Kuhusu rufaa mbalimbali katika chaguzi za ndani, kamati kuu ilijadili taarifa na kuielekeza sekretarieti ifuate maelezo na vielelezo vya ziada ili maamuzi yaweze kufanywa katika kikao kijacho," alisema Dk Slaa.

  Kuhusu mikakati ya chama kuelekea uchaguzi mkuu 2010, Dk Slaa alilaani kitendo cha serikali kwa kushirikiana na utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kukataa kuongeza mkataba wa aliyekuwa mhadhiri wake, Prof Mwesiga Baregu ambaye ni mjumbe wa CC wa chama hicho.

  Alilalamika kuwa hiyo imekuwa tabia ya serikali kwa sababu iliwahi kumfanyia hivyo Dk Masumbuko Lamwai wakati akiwa NCCR-Mageuzi. Kwa sasa Dk Lamwai ni mhadhiri wa sheria Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam na kada wa CCM.


  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mtu ambaye anakidai chama na wakati huo huo ndie mtiaji sahihi wa hundi; ni mojawapo ya mfumo mbaya zaidi wa usimamizi wa fedha! Yaani mdai wako ndiye anasimamia fedha zako!? .. grrrrrrrrrrr! Kwa kadiri ya kwamba Mbowe anaidai Chadema HAPASWI KUWA msimamizi wa fedha za chama. Labda ashuke malaika toka mbinguni kutuelewesha hili. Ni kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa haya maneno. Katibu Mkuu ndiye achukue nafasi hiyo au wachague CEO wa chama!
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ukiwa mtia sahihi kwenye cheki huruhusiwi kukopesha chama? Inawezekana alikopesha kama MBOWE LTD. Pia inategemea level ya sahihi yake kwenye cheque
   
 4. i

  ishuguy Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hongera Chadema kwa kutoa ufafanuzi, pia mmeonyesha confidence.

  kwa kufanya hivyo wananchi wataendelea kuwa na imani na chadema kama chama mbadala wa ccm.
  Hawa akina kafulila na juju inawezekana walikuwa wanatafuta gia ya kuondoka chadema bila kupoteza umaarufu.. Songeni mbele chadema.

  KILA LA HERI CHADEMA.
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji

  Mfumo wa CHADEMA umeweka check and balance ili kudhibiti hali hii; na hata yameelekezwa katika taratibu za fedha(finnancial regulations) ambazo zimepitishwa na vikao vyama chama.

  Kuna ngazi tatu za udhibiti;

  Mosi; ngazi ya upangaji wa mipango na bajeti- hii nayo ina ngazi zake mbalimbali; mipango ya miaka mitano- hii kupangwa na mkutano mkuu; mipango na bajeti ya mwaka-hii hupangwa na Baraza Kuu; Mipango na bajeti ya miezi mitatu(quarterly)- hii hupangwa na Kamati Kuu; Mipango na Bajeti ya Kila mwezi- hii hupangwa na sekretariati. Chini ya mgawanyo huu wa mamlaka ya kupanga mapato na matumizi na kupokea taarifa husika. Sasa swali la kujiuliza; Je, vikao hivyo kwa CHADEMA vinakaa? Jibu ni: NDIO. Je, vinapitia mipango, bajeti na kupokea taarifa za fedha? Jibu ni: NDIO. Kwa mantiki hiyo basi, vikao hivyo viliidhinisha chama kikope kwa yoyote; in this case Mbowe; na ni vikao hivyo hivyo vinapanga utaratibu wa kumlipa- in this case Mbowe. Na si Mbowe tu, tofauti kwake ni kiwango tu; lakini tupo wengi tumekikopesha chama, na tunakidai; hata kama ni deni(soma sadaka) ya mwanamke mjane.

  Sasa baada ya fedha kufika; fedha za ruzuku hupitia kwenye akaunti ya Wadhamini(Trustees account); hata za mfumo wa kuchangia chama kwa SMS nazo zinapita huko. Kwenye akaunti hiyo, watia saini sio Mbowe, Wala Slaa wala Komu; ni trustees wenyewe.

  Kwa maelekezo yao, na kwa sahihi zao kwa kuzingatia maombi toka kwenye uongozi wa chama yanayotokana na mipango na bajeti; fedha zinasambazwa kwenye akaunti mbalimbali: izingatiwe kwamba chama kina akaunti nyingi kwa kuzingatia ngazi na kazi. Zipo akaunti ambazo mimi ni mmoja wa signatories.

  Ngazi ya Pili ya Udhibiti ni Akaunti za chama. Sasa akaunti inayotajwa sana ni akaunti ya ujumla ya matumizi ya kawaida.(Operational Account); hii lazima watia saini wawe operatives kwa nafasi zao. Nayo kwa ajili ya check and balance imewekewa watia saini wa makundi mawili kwa nafasi zao:Category A; Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu. Category B: Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Hii ni kwa mujibu wa maazimio ya vikao ambavyo yameingizwa katika kanuni ambazo zimeeleza bayana kwamba ili fedha zitoke lazima kuwe na mtia saini mmoja kutoka katika kila kundi. Yaani Mbowe na Dr Slaa, hawawezi kabisa kutoa fedha peke yao. Sasa hawa wanaolaumiwa kwanini wanasaini cheque, ilipaswa lawama iwe kwanini wamechaguliwa kwenye nafasi zao. Siku Mkurugenzi wa Fedha akiwa Mwanakijiji, ama Mwanakijiji akawa Mwenyekiti, ni wazi Mwanakijiji atasaini cheque.

  Ngazi ya tatu ya udhibiti ni mfumo wa matumizi na uidhinishaji wa kawaida. Hapa ni pamoja na hatua zinazopitiwa mpaka cheque inandikwa. Mathalani kuandikwa kwa vouchers mbalimbali, nani anaandaa vocha, nani anaidhinisha nk. Kuandaliwa kwa payrolls nk, nani anaandaa nani anaidhisha. Tenda za kupata huduma, nani zinatolewaje, zinajadiliwaje, zinapatishwaje. Nani anafanya malipo. Ipi mipaka ya Mkurugenzi wa Fedha, ipi mipaka ya cashier.

  Kwa hiyo ukijadili mfumo wote huu kwa ujumla wake; utaona kwamba ni mfumo ambao unatia matumaini; ni wazi kwamba zipo taratibu kadhaa zinahitaji kuboreshwa; lakini hilo la Mwenyekiti kuweka sahihi si kipaumbele na wala halimuondolei wajibu wa kukikopesha chama wala haki ya kulipwa mkopo aliokopesha ili mradi tu taratibu zifuatwe.

  Tunamkaribisha yoyote yule mwenye fedha safi kuikopesha CHADEMA kwa kiwango chochote; leo tukipata mkopo mkubwa; tukawekeza kwenye vijana cream kama 200; wasomi wenye ubunifu, uwezo wa kujenga hoja na kuongoza, ambao wanakosa tu mtaji wa fedha za kushindana na mafisadi majimboni; kati yao tunaweza kabisa kupata wabunge takribani 100-150. Sasa ukipata kiasi hicho cha wabunge na idadi kubwa ya kura kwa wastani kwa mwezi come baada ya uchaguzi 2010 ruzuku ya chama inaweza kabisa kupanda toka milioni around 60 ya sasa mpaka takribani Bilioni Moja. Hapa chama kitakuwa na uwezo zaidi wa kulipa madeni huku kikitoa uongozi mbadala kwa taifa.

  Sasa majimbo 100 ukitumia kila jimbo milioni 100(hili ni kadirio la juu sana la matumizi kwenye kampeni, CCM washatangaza kwamba wanapanga kutumia Bilioni 40 ambazo ukigawa kwa majimbo ni takribani milioni 200 kwa kila jimbo!); hii ni sawa na 10,000,000,000. Hii ni sawa na Bilioni 10. Kwa hiyo kwa makadirio ya chini; ukiwa na Bilioni 3 tu unaweza kushinda majimbo mengi sana mwakani. Tatizo ni kuwa, hakuna mabilionea(wenye fedha safi) waliohuru kutoa kiwango hicho cha fedha kwa upinzani; kama kuna mtu anawafahamu awataje ama atuandikie tu kupitia info@chadema.or.tz tukawaone ama kama kuna taasisi zinaweza kutoa kiwango hicho(za ndani ya nchi). Mabenki yetu hayakopeshi vyama vya siasa(labda makampuni ya kibiashara yaliyoanzishwa na vyama vya siasa). Hoja ya vyama kuanzisha makampuni ya uwekezaji, ni ya muhimu(in terms of long term thinking) lakini haiwezi kutufaa sana kwa muda mchache uliobaki wa takribani mwaka mmoja kuelekea uchaguzi wa 2010. Lazima tufikirie njia mbadala ya vyanzo vya rasilimali kwa ajili ya uchaguzi. Kichekesho zaidi ni kuwa serikali inajiandaa kupeleka marekebisho ya sheria bungeni; ndani ya mapendekezo yao mpaka sasa, wanataka kukutaza fedha zisichangwe kutoka nje ya nchi(hii naikubali kama ni kutoka serikali za nchi nyingine, taasisi na makampuni yao, au watu wao) lakini inakataza hata watanzania walionchi za nje. Sasa mchango wa diasphora, kwa maana ya kuleta fedha na kuja kuwekeza, serikali inautaka; lakini mchango wao wa kisiasa kwa maana ya kupiga kura ama walau kuchangia rasilimali za kuchochea mabadiliko serikali inaukacha. Tukubali?

  JJ
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  sasa Mafisadi mkiongozwa na waandishi wa New Habari co. leta ushahidi adharani ili tumkate kichwa nyoka .
  Kwaujumla kile wanachojitahidi kueneza dhidi ya CHADEMA , Daima raia wameng'amua mchezo wao, wameanza kupuuza, ama kweli WAtz wanabadilika sana .

  Niwape ujumbe RA, Karamagi,Makamba, kingunge kama mtakua hai ama wafu miaka kumi ijayo TZ inakua kwenye mabadiliko makubwa kisiasa na kiuongozi ngazi ya Taifa, kweli RA NA LOWASA kama hawatanyea debe keko mimi nasubiri kuona.
  kama hamuamini tutaona....ninamashaka na Kingunge kama miaka kumi atakua hai, ila RA ATAKUA HAI, HAPA TUTAMJUMUISHA NA FISADI MKUU DARAJA LA KWANZA Manji Yusuph.
  [​IMG]
   
 7. b

  bambumbile Senior Member

  #7
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji,

  Hapa utagonga mwamba tu na wenye chama hawawezi kukuelewa. Sanasana wataishia kusema umetumwa na CCM.

  Mnyika anasema kuna checks and balances za kutosha, kama ni kweli, hayo malalamiko yote yanatoka wapi? Penye uwazi majungu hujitenga.

  Tuweni wakweli, huo mfumo wa usimamizi wa pesa utaendelea kuwaletea matatizo makubwa. Mwache mwenyekiti aongoze chama na usimamizi wa fedha uwe kwa watu wengine.

  Hakuna kitu kigumu kwenye uongozi wowote kama usimamizi wa fedha. Ukitaka watu wakorofishane kirahisi, basi vuruga kidogo tu kwenye pesa. Kwa nchi kama TZ ambayo ufisadi umekomaa, inabidi kuwa muwazi hata zaidi ya kawaida.

  Mna mlolongo mrefu sana wa uthibiti wa pesa na kwenye barabara ndefu hakukosekani kona. Someni corporate governance, mbona kuna mifano mingi sana ya kusimamia pesa za shirika au chama na kuondoa kabisa conflict of interest?
   
 8. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hili hapana! Mwenyekiti kukikopesha Chama, kuwa mtiaji sahihi wa hundi, ni hatari kwa Demokrasia ya Chama! Tafadhali DK. Slaa, sisi ndio wanachama wa Chadema, kwa hili la madeni tunaomba utuwekee wazi zaidi, hayo madeni na assets na mapato na matumizi, za Chama kwenye Tovuti yetu! Maana at the end michango ya wanachama ndio italipa madeni hayo. Tuainishie hizo Milion 42 za Mbowe na 11 za Ndesamburo, isijeikawa wamejilipa marupu rupu halafu siye tuwalipe! Mfumo wa wanachama na haswa viongozi kukikopesha chama una walakini! Unapaswa kuepukwa mara mmoja!
   
 9. K

  Kabogo Member

  #9
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenena!!!!!. Mwanyka anajitetea tu M/Kit kua signatory huo ni uozo mkubwa hakuna chek&balance hapo uizi mtupu.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna shida yoyote ile kwa chama kukupa fedha kwa watu kama wakina mbowe na jamii wakajua, Je yale ya ufisadi nayo vipi??. Hongera Mnyika kwa akazi nzuri sana
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi nilitegemea pamoja na hoja nzuri sana na mkinzano wa mawazo na mtizamo juu ya swala hili sasa tungaliwabana wale wote wenye madai ya matumizi mabaya ya pesa ndani ya Chadema wamwage ushahidi maana watakuwa na documents zote . Nafasu hii kaitoa Slaa mwenyewe na anangojea au hilo sasa halipo bado tuna endeleza longo lomngo ? Ni wazi kwamba kuna shida mahali fulani ndani ya Chadema na labda watu kuto eleweshwa makosa yaliyo tendeka basi wanaamka na maneno .

  Maneno ya ndani kabisa leo yakianza kusema na watu walio kimbia wenyewe Chama kesho watasema mengine wakisha ondoka huko waliko kimbilia . Sifa moja ya uongozi ni kutunza siri na kuwa muwazi nakukemea uozo ukiwa umekalia kiti na si zaiid ya hapo .Kemea ukiwa ndani kwa nguvu usipo sikika kimbia semea nje tutakuelewa .
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu kwenye hili tupo ukurasa mmoja sana, ninamfagilia sana Mwenyekiti wa sasa wa Chadema kwa kuweza kuongoza chama chake cha siasa kama inavyotakiwa, lakini kwenye siasa hasa za vyama sauti ya wengi, sometimes ni ya political Gods,

  - It is a high time sasa Chadema wakaunda mfumo mpya wa usimamizi wa fedha zao, kuliko walio nao sasa ni kitu kidogo sana ambacho hakitakiwi kuwa na malumbano huko ndani kuki-implement, makelele yametokea binafsi siamini kwamba Freeman anaweza kuiba hela za Chadema, ninasema no way the man is too rich to do that, sana sana ninaikubali hoja kwamba amekuwa akiisaidia Chadema kwa hela zake binafsi, ambazo zingine wala hawawezi kumlipa back,

  - However: The time is up sasa Chadema kwa Chadema, kuanzisha mfumo mpya wa usimamizi wa fedha zao na Freeman should step aside on this na awaachie Chadema as chama waamue what and how they want to do on that!

  Respect.


  FMEs!
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mh. Dr.Slaa,
  Kusema kweli kuna kayli moja inapingana na taratibu za mahesabu. Mtu ambaye anayekidai chama hawezi kuwa muidhinishaji wa malipo ktk chama cha kisiasa..Mwenyekiti anaweza kutumiwa kama uongozi wa Waziri ktk wizara ambaye sii lazima awe mweka sahihi ya mtumizi ya wizara yake.

  Ni muhimu sana kuelewa hizi lawama zinatokana na kitu gani kwani mara nyingi mfadhili wa chama akiwa ndani ya maswala ya fedha ndipo matatizo huzuka. tazama CCM na kina Rostam..makosa ni yale yale na CCM wamekmwondoa Rostam ktk sekretariet yao kwa sababu kama hizo..Mbowe ni mshikaji wetu na tunampa hongera nyingi sana ktk kujitolea kwake ili Chadema nao wahongere, lakini ktk swala la fedha ni bora na muhimu yeye akae pembeni ktk matumizi ya fedha hizo. Kama amekiamini Chama na kukipa mkopo mkubwa kiasi hicho basi anatakiwa kukubali pia kuwaamini viongozi chinin yake ktk matumizi ya fedha alochangia. Hii ni ktk kuondoa fitna na chuki ambazo hazina maana wala sababu ktk jambo dogo sana lakini lenye mvuto mkubwa ktk migogoro..Na ndio maana taratibu za mahesabu haziruhusu mfumo kama huu, hata kama....Labda kama ingekuwa NGO..
  Ni maoni ya ushauri wangu kwenu...
   
 14. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hapana, hii logic yako haiwezi ku-apply kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani Tanzania. Duniani kote vyama vya siasa hujiendesha kwa michango ya wanachama. Hapa kwetu ni tofauti sana. Kwetu vyama vya siasa vya upinzani vinaendeshwa kwa kiasi kikubwa na michango ya viongozi wake wa juu. Hapa kwetu kama viongozi wa chama cha siasa wapo hoi kiuchumi na hawana ruzuku ya kutosha kutoka serikalini hicho chama lazima kidode na kiloe. Na mifano ipo tele hapa kwetu ambapo vyama vya siasa kati ya karibu 20 vilivyopo ni vyama visivyozidi 5 ambavyo angalau vipo kwenye lime light. CHADEMA tunabahati kwamba tangu kianze kimekuwa kikipata viongozi ambao wana uwezo na wana moyo wa kutumia uwezo wao kifedha kuendesha chama.

  Unavyoongea wewe ni kama vile chadema walipanga kikatiba kumkopa Mbowe kama ambavyo wameweka katika kanuni zao kwamba mwenyekiti wa chama atakuwa signatory wa cheque. Na unaongea kana kwamba kukopa ni harusi. Ndugu yangu unakopa kwa sababu una shida. Sasa mwenyekiti hawezi kukosa sifa ya kuwa signatory kwa sababu tu eti amekisaidia chama chake. This is simply bad logic, lakini ni vigumu kuelewa kwa sababu umesema hadi ashuke malaika kutoka mbinguni ndio akuelewesha.

  Kwa mujibu wa kanuni za fedha za chadema, Mwenyekiti wa chama ni moja wa signatories wa account za chama katika kundi moja, wakati Katibu Mkuu ni moja wa signatories katika kundi lingine. Ndivyo ilivyokuwa wakati wa Mzee Mtei chama kilipoanza, ndivyo ilivyokuwa wakati wa Bob na ndivyo ilivyo kwa Mbowe na ndivyo itakavyokuwa kwa Mwenyekiti yeyote ajaye huko mbele unless Kamati Kuu na Vikao vingine katika chama viamue vinginevyo.

  Kuchangia harakati za mabadiliko, tuma neno CHADEMA kwenda 15710 (kwa mitandao ya Vodacom na Zain pekee)
   
 15. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #15
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  This is great. Lakini so far Mbowe kuwa signatory wa account ni kwa mujibu wa kanuni za chama. Kwamba kuna haja ya kuziangalia hizi kanuni, this is absolutely fine; ni jambo ambalo tutaliangalia katika vikao vyetu vya ndani. Being one of the wawakilishi wa sauti za wapenzi wa mageuzi ndani ya chadema naahidi kabisa kuwa tutaliangalia hili katika vikao vyetu ili kuona uwezekano huo.

  Ambacho binafsi nimekuwa napinga ni kitendo cha baadhi ya watu kumlaumu Mbowe kuwa signatory as as if amejiamulia kinyume na taratibu. Tufike mahala tutofautishe kati ya kosa la kikanuni na kosa la kiongozi kama kiongozi. Ambacho kimekuwa kikiendelea katika siku za karibuni ni kumshambulia Mbowe kana kwamba amevunja kanuni na katiba ya chadema. Sasa ukweli ni kwamba Mbowe hajavunja kanuni au sheria yeyote ndani ya chadema na ya nchi kwa kuwa signatory wa account. Sasa kama tatizo ni kanuni tusema hivyo, na kama ni kosa ni la kamati kuu na hivyo kazi yeu kama viona mbali kupitia forum hii ni kuishauri na hata kuiagiza (ushauri wa wengi ni amri) kamati kuu ya chama hiki kuziangalia upya kanuni hizi. Kwa kuwa CHADEMA ni chama cha watu chenye masikio makubwa ya kusikia, watasikia na watalifanyia kazi hili.

  Mimi binafsi nawashukuru sana wana JF kwa kutoa ushauri murua kwa chama chetu; hii ni ishara kwamba mnataka kuona hiki chama kinaongoza nchi katika kuleta mabadiliko ambayo wananchi wanayalilia kwa miongo na miongo.

  Mbali ya mawazo haya mazuri, mnaweza pia kuichangia kwa kutuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 (mitandao ya Zain na Vodacom pekee).
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapana shaka kuwa CHADEMA chama makini sana
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji leo umechemsha kabisa kabisa.Huwezi ukabdilisha kanuni za chama eti kwasababu kati ya wasimamizi au watia saini wanakidai chama.Nadhani umesoma vizuri hii habari Dr Slaa amesema kwakuwa CHADEMA ni chama chenye mahitaji mengi hivyo suala la kukopa haliepeukiki hivyo wataendelea kukopa pale itakapobidi kufanya hivyo.Leo utamtoa Mbowe na kumuweka DR Slaa kama unavyodai au mwingine yeyote,next year ni Uchaguzi Mkuu Slaa huyu huyu ambaye unasema ndiye awe signatory au msimamizi wa fedha anaweza akakikopesha chama,je naye inabidi kanuni ibadilishwe tena?jamani let think outside the box tusiwaze kitototo.Hoja hapa ni kuwa chama kina wadhamini ambao wao ndio wasimamizi wa mali za chama na wamepewa mandate yote ya kuhoji pale wasiporidhishwa na mwenendo mzima wa fedha na mali zote za chama kwa ujumla?
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Pole sana Dr.Kitila

  Kwa hiyo unakiri wazi kabisa kuwa wenye fedha ndio wanaanzisha vyama

  1. Kwa nini vyama hivi vinakosa michango ya watu?
  2. Je ni mpaka lini Vyama hivi vitaendelea kuwategema viongozi tu wenye fedha , je wakifilisika chama ndio kimekufa?
  3. badala ya kusema tu kuwa 'mnawategema viongozi kifedha' je mmefanya juhudi gani kuepuka tegemezi hizi za viongozi? Obama ansema walichangiwa mpaka dola 1 na watoto wa shule ili washinde uchaguzi

  4. Je kama mnategema fedha za viongozi, lengo lao na dhumuni lao ni nini? maana kwa namna hii
  (a) Chama kinakuwa hakina demokrasia
  (b)kuwapinga kama wakikosea ni kazi..YES si watazira na kuondoka na fedha zao

  5.Hivi hao viongozi hizo fedha wanazokopesha wanapolipwa wanalipwa na Interest?


  6. Is this project of opposition parties is viable? to you?

  Kama mpaka leo ni miaka zaidi ya 15 bado hamjaweza kuwa na uhakika wa michango ya wanachama wanaokipenda, hauoni CHADEMA SIO CHAMA CHA WATU.. CHAMA CHA WAJASIRIAMALI WACHACHE WHICH IS WRONG!

  7.Ili nishike nafasi ya Mbowe ninatakiwa kuwa na Capital ya shiling ngapi Dr.??   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Kushinda uchaguzi wa US na ku-maintain au kuanzisha chama cha siasa Tanzania ni vitu viwili tofauti, au?

  Respect.

  FMEs!
   
 20. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  tusilaumu vyama kukopa kwa viongozi. inabidi tujiulize je sisi tunao
  utamaduni wa kuchangia vyama vya siasa? ndio vyama vya siasa kwani
  harusi tunachangia (labda kwa sababu tunatarajia kushiriki katika matunda
  ya uchangiaji wetu katika muda mfupi tofauti na tukichanga kwenye vyama).
   
Loading...