CHADEMA na Upungufu wa Mawakala Igunga

CUF Ngangari

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
273
51
ikiwa leo ndio siku ya kwanza ya kuapisha mawakala leo na kesho, viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo cdm wanahaha kila kona kuhakikisha wanatimiza idadi ya mawakala ambapo mpaka sasa mawakala walioletwa kuapa hapa ofisi ya tume wapo pungufu na wamerudi kutafuta wengine na kuahidi kuwaleta kesho, ni CUF na CCM pekee ndio waliotimiza idadi ya mawakala kwa siku ya leo, kwa upande wa CUF naona wakina mama ni wengi nilipowauliza wakanijibu kuwa wameamua kujitolea kulinda kura za kijana wetu Mahona na tutahakikisha anakuwa mbunge kwa tunampenda huyu kijana ni muadilifu na anatupenda tumesoma nae na kucheza nae walisema wakina mama hao ambao ni mawakala wa CUF.
 
Taarifa hii inahitaji verification hasa kwa sababu aliyeitoa anajiita CUF Ngangari. Kuna wakati tuliwekewa taarifa hapa na Julius Mtatiro kuwa CDM wamevamia msafara wa CUF wakati wa kurudisha kadi kuja kufuatilia taarifa ikawa kinyume.

Walioko Igunga, tafadhali mtujuze.
 
.........tutahakikisha anakuwa mbunge kwa tunampenda huyu kijana ni muadilifu na anatupenda tumesoma nae na kucheza nae walisema wakina mama hao ambao ni mawakala wa CUF.


Nimependa tu hapo kwenye red.....hawa wakina mama watamu sana, wana hadi kumbukumbu za kucheza wote enzi za shule (bila shaka vidudu na msingi, enzi za "kibaba na mamaa")...

Haya bwana hongera zenu japo by implication mawakala wa CUF ndio wa CCM, si ndio wale juu kijani na njano yenye kisu na umma, ooh sorry, jembe na nyundo na chini red and white yenye mizani
 
Lakini CUF kwanini mnakuwa na matumizi mabaya ya pesa? Kwanini msiwatumie Mawakala hao hao wa CCM! Cha Mumeo si chako jamani!
 
I can not buy this one........

Chadema mawakala wametimia hadi kuna reserve halafu mwanangunuri unataka kudanganya umma.
 
I can not buy this one........

Chadema mawakala wametimia hadi kuna reserve halafu mwanangunuri unataka kudanganya umma.

Mkuu, tena inabidi waingie kwenye usimamizi na vidumu vya lita tano kwa ajili ya kukojolea, maji lita tatu na mikate miwili. Hakuna kutoka kwenye chumba cha kupigia na kuhesabia kura, mpaka kieleweke.

Dawa ni kukaba hadi penati; si unaona CCM wanavyozusha vurumai? Wamekabwa pande zote.
 
CUF na CCM mna vituo hewa nini? Haiwezekani wakala wasitoshe kwa chama makini, safari hii tuko makini zaidi ya 2010.
 
Back
Top Bottom